Maswali yanayoulizwa sana kuhusu "maudhui yanayolenga watoto"

COPPA and YouTube: Answering Your Top Questions

 

Bila kujali mahali ulipo, kisheria unatakiwa kutii Sheria ya Kulinda Faragha ya Watoto Mtandaoni na/au sheria zingine. Unatakiwa kutueleza kwamba video zako zinalenga watoto iwapo unatayarisha maudhui yanayolenga watoto. Mabadiliko haya ni kwa ajili ya kuwalinda vyema watoto, faragha yao, na pia kutii sheria. 

Kwa nini ni wajibu wa mtayarishi kutii sheria ikiwa YouTube ndiyo inayokusanya data (na si mtayarishi)?

YouTube na watayarishi wanashiriki wajibu wa kutii kanuni za faragha ya watoto chini ya sheria mbalimbali. Tunategemea utueleze ikiwa maudhui yako yanalenga watoto kwa sababu unajua maudhui yako vyema. Tunaamini kuwa utaweka mipangilio ya hadhira yako kwa usahihi na tutabatilisha mipangilio ya chaguo la hadhira yako katika hali ambapo kuna hitilafu au matumizi mabaya. Ukishaweka mipangilio ya hadhira yako, tutadhibiti jinsi tunavyotumia na kukusanya data kwenye maudhui hayo ili kuendana na mipangilio ya hadhira.
Nitajuaje kuwa maudhui yangu HAYALENGI watoto?
Kulingana na mwongozo wa Tume ya Biashara ya Marekani (FTC), ikiwa video yako ina waigizaji, wahusika, shughuli, michezo, nyimbo, hadithi au mada nyinginezo ambazo zina lengo la kufikia watoto, kuna uwezekano kwamba ni "maudhui yanayolenga watoto." Ikiwa sivyo, hakuna uwezekano mkubwa kwamba maudhui yako yanahitaji kutiwa alama kuwa "maudhui yanayolenga watoto."
Si lazima video iwe inalenga watoto kwa sababu tu:
  • Ni salama au inafaa kutazamwa na kila mtu (yaani "inafaa kutazamwa na familia")
  • Inajumuisha shughuli ambayo kwa kawaida inahusiana na watoto
  • Watoto wanaweza kuiona kwa bahati mbaya

Ifuatayo ni baadhi ya mifano ya aina za video zinazoweza kutambuliwa kuwa "hadhira ya jumla", ikiwa hakuna maelezo yanayofafanua kuwa zina maudhui yanayolenga watoto:

  • Video ya vitu vya kujifanyia mwenyewe inayofundisha watu wanaopenda midoli jinsi ya kuitengeneza au kutengeneza vitu vya udongo
  • Blogu ya video za familia kuhusu ziara katika bustani ya burudani 
  • Video iliyo na maagizo ya kina kuhusu jinsi ya kutengeneza vifaa vya kuchezea watoto 
  • Video za utani zenye watu wazima wakiimba pamoja nyimbo za watoto 
  • Kipindi kilichohuishwa kinachomvutia kila mtu
  • Video ya mchezo wa Minecraft inayojumuisha vichekesho vya watu wazima 

Kumbuka kuzingatia kwa umakini wale unaojaribu kuwafikia kupitia video zako unapotathmini maudhui pamoja na vigezo vilivyobainishwa hapo juu. 

Je, maudhui ya "hadhira ya jumla" ni sawa na "hadhira mseto"?
Hapana. Maudhui ya hadhira ya jumla ni maudhui ambayo yanaweza kumvutia kila mtu, lakini si mahususi kwa watoto au maudhui ambayo yanalenga hadhira ya vijana au watu wenye umri mkubwa. Maudhui ya hadhira ya jumla yanapaswa kubainishwa kuwa “hayalengi watoto.”  

Ifuatayo ni baadhi ya mifano ya aina za video zinazotambuliwa kuwa "hadhira ya jumla", ikiwa hakuna maelezo yanayofafanua kuwa zina maudhui yanayolenga watoto.  
  • Video ya vitu vya kujifanyia mwenyewe inayofundisha watu wanaopenda midoli jinsi ya kuitengeneza au kutengeneza sanamu za udongo
  • Blogu ya video za familia inayoeleza wazazi wengineo kuhusu ziara katika bustani ya burudani 
  • Video iliyo na maagizo mahususi kuhusu jinsi ya kutengeneza michezo ya watoto au ishara
  • Maudhui yaliyohuishwa yanayomvutia kila mtu
  • Video ya michezo inayojumuisha vichekesho vya watu wazima 
Kwa upande mwingine maudhui ya hadhira mseto yanatambuliwa kuwa aina ya maudhui yanayolenga watoto. Haya ni maudhui ambayo yanalenga watoto kama mojawapo ya hadhira yake, hata kama watoto si hadhira kuu au ya msingi na hubainishwa kuwa maudhui yanayolenga mtoto baada ya kuendana na vigezo vilivyobainishwa hapo juu.

Je, ninaweza kuweka tu kanusho kwamba maudhui yangu hayalengi watoto?

Kuweka kanusho linaloeleza kwamba maudhui yako yanalenga hadhira zenye umri wa miaka 13 na zaidi hakumaanishi kuwa FTC itazingatia kiotomatiki kwamba maudhui yako hayalengi watoto. Kwa hakika ni kigezo ambacho kinaweza kusaidia kutambua hadhira uliyoilenga, lakini FTC itailinganisha dhidi ya vigezo vinginevyo vya Sheria ya Kulinda Faragha ya Watoto Mtandaoni (COPPA) kama vile: 
  • Uwepo wa wahusika, shughuli, michezo, vinyago, nyimbo, hadithi au vipengele vingine ambavyo hasa vinawavutia watoto
  • Taarifa zingine ambazo huenda umetoa maelezo kuhusu hadhira inayokusudiwa kwenye maudhui yako ambazo ni tofauti na kanusho (kama vile, zilizotolewa kwenye tovuti binafsi)

Je, ninahitaji kuthibitisha umri wa hadhira yangu ikiwa sina zana za kufanya hivyo? Je, FTC inazingatia kitu gani kama ushahidi kwamba watoto wanatazama maudhui yangu? 

Ushahidi wowote unaoweza kuwa nao kuhusu umri wa watazamaji wako ni mojawapo tu ya mambo ambayo unapaswa kuzingatia katika kuteua maudhui yako kuwa "yanalenga watoto". Kwa bahati mbaya, kipengele cha Takwimu za YouTube (YTA) hakiwezi kukusaidia kubaini ikiwa watoto wanatazama maudhui yako. FTC imeshauri uzingatie data, kama vile matokeo yanayotokana na utafiti kuhusu umri wa watumiaji wako, yanayoweza kukusaidia kubaini ikiwa maudhui yako yanalenga watoto.
Kwa nini YouTube haikuweka chaguo la mipangilio ya "hadhira mseto?" 
Katika kusanifu kipengele cha mipangilio ya hadhira, tumerahisisha chaguo za watayarishi kwa kuunda aina moja ya "maudhui yanayolenga watoto" ili kuepusha mkanganyiko zaidi. Kuna changamoto katika aina ya maudhui yanayolenga hadhira mseto na tumewasilisha maoni ya umma kwa FTC ili kutusaidia kutafuta suluhisho bora kwa watayarishi, ikiwa ni pamoja na watayarishaji wa maudhui yanayolenga hadhira mseto. 

Ni vipengele vipi ambavyo havipatikani kwenye maudhui yanayolenga watoto, na kwa nini vipengele hivyo havipatikani? 

Unaweza kupata orodha ya vipengele ambavyo kwa sasa havipatikani kwenye maudhui yanayolenga watoto hapa. Vipengele vyote au sehemu ya vipengele hivi vinaweza kutegemea data ya mtumiaji. Ili kusaidia kulinda faragha ya watoto na kukidhi mahitaji ya kisheria, tunapaswa kudhibiti ukusanyaji na matumizi ya data kwenye video ambazo zimebainishwa kuwa "zinalenga watoto."

Je, mapendekezo yatatumikaje kwa maudhui yanayolenga au yasiyolenga watoto? Je, ugunduzi wa video zangu utaathiriwa?

Lengo la mifumo ya mapendekezo ya YouTube ni kuwasaidia watumiaji kutafuta video wanazotaka kutazama na kuwaunganisha na maudhui yanayopenda, ikiwa ni pamoja na maudhui yaliyobainishwa kuwa "yanalenga watoto". Tunajitahidi kuwapa watumiaji maudhui yanayowavutia na kuwapa hali bora ya utumiaji kwenye YouTube. Video ambazo zimebainishwa kuwa "zinalenga watoto" zina uwezekano zaidi wa kupendekezwa pamoja na video zingine za watoto. Ili kuhakikisha kuwa maudhui yako yanafikia hadhira husika, ni muhimu kubainisha kwa usahihi maudhui yako kuwa "yanalenga watoto" au "hayalengi watoto."

Video hii inaonekana kuwa haifai. Kwa nini imebainishwa kuwa "inalenga watoto?"

Video au hadhira ya kituo inapobainishwa kuwa "inalenga watoto," inaonyesha kuwa watoto ndio watazamaji wakuu wa maudhui au kwamba video hiyo inalenga watoto. Uwezo wa kuweka hadhira ya maudhui kuwa "inalenga watoto" ni kwa ajili ya kuwasaidia watayarishi kutii vyema Sheria ya Kulinda Faragha ya Watoto Mtandaoni (COPPA).

Pia, tuna mifumo inayotumika kubaini ikiwa maudhui yanafaa kuchapishwa kwenye YouTube. Mwongozo wa Jumuiya ya YouTube unabainisha maudhui yanayoruhusiwa na yasiyoruhusiwa kwenye YouTube. Tunawekeza katika teknolojia na timu zinazosaidia kuwapa watoto na familia ulinzi bora zaidi iwezekanavyo kwenye YouTube. Kwa mfano, tunaweka mipaka ya umri kwenye maudhui yanayolenga hadhira ya watu wazima lakini yanaweza kuchanganywa na maudhui ya familia kwa urahisi. Pia, tunaondoa maudhui haya ikiwa kichwa, maelezo au lebo zinaonyesha kuwa yanalenga watoto na familia kwa njia dhahiri. Iwapo kuna maudhui ambayo unadhani yanakiuka Mwongozo wa Jumuiya ya YouTube, unaweza pia kutumia kipengele cha kuripoti ili kuyawasilisha yakaguliwe na wafanyakazi wa YouTube.

Iwapo maudhui yamebainishwa kuwa "yanalenga watoto," je, inamaanisha kuwa yatajumuishwa kwenye programu ya YouTube Kids?

Video zilizobainishwa kuwa "zinalenga watoto" hazijumuishwi kiotomatiki kwenye programu ya YouTube Kids. Sera zetu za maudhui zinahakikisha kuwa maudhui kwenye YouTube Kids yanaambatana na umri, yanatii kanuni zetu za ubora, na yanakidhi mambo mbalimbali yanayowavutia watoto kote duniani. Tunatumia mseto wa vichujio vya kiotomatiki, maoni ya watumiaji na ukaguzi unaofanywa na binadamu ili kuamua kama maudhui yanafaa kuwekwa katika programu ya YouTube Kids.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
9091608641297976850
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false