Kudhibiti vizuizi katika maudhui yako

Vizuizi vinaweza kuwazuia watazamaji kutazama video zako au kuona Machapisho yako ya jumuiya. Vizuizi pia vinaweza kuathiri uchumaji wa mapato kupitia video unapokuwa umejiunga kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube. Kwa mfano, video inaweza kuwa isiyofaa kwa watazamaji walio na umri wa chini ya miaka 18 au huenda kukawa na tatizo la hakimiliki ambalo halijatatuliwa.

Kuangalia vizuizi kwenye video yako

Ili kuangalia iwapo vizuizi vinaathiri video yako:

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui.
  3. Katika kichupo cha Video, tafuta video yako kwenye orodha na uangalie safu wima ya “Vizuizi”. Ili kuchuja video zako, bofya Chuja chuja matokeokisha uchague kichujio/vichujio vyako: 
    • Mipaka ya umri: Watazamaji walio na umri unaozidi miaka 18 au pasiwepo.
    • Hakimiliki: Madai ya Content ID au maonyo ya hakimiliki.
    • Zinazolenga watoto: Zinazolenga Watoto (ulizobainisha), Zilizobainishwa kuwa zinalenga watoto (zilizobainishwa na YouTube), Zisizolenga watoto au Ambazo hazijabainishwa.
  • Ikiwa kizuizi kimeorodheshwa, unaweza kuwekelea kiashiria juu yake ili upate maelezo zaidi na uombe ukaguzi.

Kuangalia vizuizi kwenye chapisho lako

Ili uangalie iwapo vizuizi vinaathiri chapisho lako:

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui.
  3. Kwenye kichupo cha Machapisho, tafuta chapisho lako kwenye orodha na uangalie safu wima ya "Vizuizi".

Ikiwa kizuizi kimeorodheshwa, unaweza kuwekelea kiashiria juu yake ili upate maelezo zaidi na uombe ukaguzi.

Aina za vizuizi

Hakimiliki

Ikiwa umepakia video iliyo na maudhui yanayolindwa na hakimiliki, video yako inaweza kupata madai ya Content ID au onyo la hakimiliki.

Sheria na masharti na sera

Ikiwa video au chapisho lako limeondolewa, limewekewa mipaka au limefanywa kuwa la faragha na YouTube kwa sababu ya tatizo la sheria na masharti, utaona “Sheria na masharti” katika safu wima ya “Vizuizi”. Kwa mfano, unaweza kuona tatizo la sheria na masharti ikiwa:

Mipaka ya umri

Ikiwa video yako haifai kwa watazamaji walio chini ya umri wa miaka 18, inaweza kuchukuliwa kuwa maudhui yenye mipaka ya umri.

Inalenga watoto

Ikiwa hadhira ya maudhui yako imewekwa kuwa inalenga watoto, tutazuia vipengele fulani ili kutii sheria zinazotumika.

Ufaafu kwa matangazo

Ikiwa umejiunga kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube na maudhui yako yametambuliwa kama yasiyofaa kwa watangazaji wengi, video yako inaweza kuonyesha matangazo machache au isionyeshe tangazo lolote.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
5009170440288076531
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false