Kutaja vituo katika majina na maelezo ya video

Mitajo hukuruhusu kujumuisha jina au kitambulishi cha kituo kingine katika kichwa au maelezo ya video yako. Unapotaja kituo kingine, kitapata arifa kwenye kikasha chake– pata maelezo zaidi.

Kutajwa kwa jina au kitambulishi cha kituo chako kwenye video ya mtu mwingine hakuongezi uwezekano wa video yake kuonekana kwa mashabiki wako.

Mtaje mtayarishi mwingine

Ili kuongeza mtajo unapounda au kuhariri kichwa au maelezo ya video:

  1. Andika alama ya "@" ikifuatiwa na jina la kituo au kitambulishi.
  2. Chagua kitambulishi au jina la kituo kwenye orodha iliyopendekezwa.

Unaweza kutaja watayarishi wengi unavyotaka mradi tu majina yao yawe ndani ya kikomo cha idadi ya juu ya herufi.

Watazamaji wanapogusa jina la mtayarishi, kidirisha cha maelezo kuhusu mtayarishi kitafunguka sehemu ya chini ya skrini. Kidirisha hiki kitaonyesha maelezo kuhusu kituo, ambayo ni pamoja na maelezo na video zake za hivi karibuni.

Kuona waliotaja kituo chako

  1. Fungua programu ya YouTube .
  2. Gusa kengele ya Arifa katika sehemu ya juu ya skrini yako.
  3. Bofya kichupo cha Kutaja.
Pata vidokezo vya ushirikiano kwa ajili ya watayarishi.

Badilisha arifa za kutajwa

Hutapokea arifa kila wakati unapotajwa. Utapokea tu arifa ikiwa ni muhimu, kwa mfano tutakuarifu unapotajwa na mtayarishi mwenye idadi sawa ya wanaofuatilia.

Ili upate maelezo zaidi kuhusu kudhibiti arifa, angalia sehemu ya Kudhibiti arifa za YouTube.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
11847456759235712744
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false