Mitajo hukuruhusu kujumuisha jina au kitambulishi cha kituo kingine katika kichwa au maelezo ya video yako. Unapotaja kituo kingine, kitapata arifa kwenye kikasha chake– pata maelezo zaidi.
Kutajwa kwa jina au kitambulishi cha kituo chako kwenye video ya mtu mwingine hakuongezi uwezekano wa video yake kuonekana kwa mashabiki wako.
Mtaje mtayarishi mwingine
Ili kuongeza mtajo unapounda au kuhariri kichwa au maelezo ya video:
- Andika alama ya "@" ikifuatiwa na jina la kituo au kitambulishi.
- Chagua kitambulishi au jina la kituo kwenye orodha iliyopendekezwa.
Unaweza kutaja watayarishi wengi unavyotaka mradi tu majina yao yawe ndani ya kikomo cha idadi ya juu ya herufi.
Kuona waliotaja kituo chako
- Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
- Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maoni.
- Bofya kichupo cha Kutaja.
Badilisha arifa za kutajwa
Hutapokea arifa kila wakati unapotajwa. Utapokea tu arifa ikiwa ni muhimu, kwa mfano tutakuarifu unapotajwa na mtayarishi mwenye idadi sawa ya wanaofuatilia.
Ili upate maelezo zaidi kuhusu kudhibiti arifa, angalia sehemu ya Kudhibiti arifa za YouTube.