Nunua Shukrani Moto

Kumbuka: Baadhi ya Super Chat, Super Stickers, au Shukrani Moto mpya zinazonunuliwa kwenye programu ya YouTube katika Android zitatozwa kupitia Google Play. Mabadiliko haya hayaathiri bei au gharama, yanaathiri tu sehemu ambako ununuzi unatozwa. Unaweza kwenda kwenye pay.google.com ili uangalie gharama mpya na jinsi unavyotozwa.

Unaweza kununua Shukrani Moto kwenye video za watayarishi zinazoshiriki na utoe mchango wako kwenye vituo vya YouTube. Unaponunua Shukrani Moto, unanunua uhuishaji wa mara moja utakaoonyeshwa tu kwako kwenye sehemu ya juu ya video. Kama bonasi ya ziada, pia utapata maoni ya kipekee, yenye rangi na yanayoweza kuwekewa mapendeleo katika sehemu ya maoni ya video.

How to buy Super Thanks

Maeneo ambapo Shukrani Moto zinapatikana

Unaweza kununua Shukrani Moto kwenye vifaa vya mkononi au kompyuta katika maeneo yafuatayo:
  • Aljeria
  • Samoa ya Marekani
  • Ajentina
  • Aruba
  • Australia
  • Austria
  • Bahareni
  • Belarusi
  • Ubelgiji
  • Bermuda
  • Bolivia
  • Bosnia na Hezegovina
  • Brazili
  • Bulgaria
  • Kanada
  • Visiwa vya Cayman
  • Chile
  • Kolombia
  • Kostarika
  • Korasia
  • Kuprosi
  • Jamhuri ya Zechia
  • Denmaki
  • Jamhuri ya Dominika
  • Ekwado
  • Misri
  • Elsavado
  • Estonia
  • Ufini
  • Ufaransa
  • Guyana ya Ufaransa
  • Polinesia ya Ufaransa
  • Ujerumani
  • Ugiriki
  • Guadalupe
  • Guam
  • Gwatemala
  • Hondurasi
  • Hong Kong
  • Hangaria
  • Aisilandi
  • India
  • Indonesia
  • Jamhuri ya Ayalandi
  • Israeli
  • Italia
  • Japani
  • Yordani
  • Kenya
  • Kuwaiti
  • Lativia
  • Lebanoni
  • Lishenteni
  • Litwania
  • Lasembagi
  • Malesia
  • Malta
  • Meksiko
  • Moroko
  • Uholanzi
  • Nyuzilandi
  • Nikaragua
  • Naijeria
  • Masedonia Kaskazini
  • Visiwa vya Mariana Kaskazini
  • Norwe
  • Omani
  • Panama
  • Papua
  • Paragwai
  • Peru
  • Ufilipino
  • Polandi
  • Ureno
  • Pwetoriko
  • Katari
  • Romania
  • Saudia
  • Senegali
  • Sabia
  • Singapoo
  • Slovakia
  • Slovenia
  • Afrika Kusini
  • Korea Kusini
  • Uhispania
  • Uswidi
  • Uswizi
  • Taiwani
  • Tailandi
  • Uturuki
  • Visiwa vya Turks na Caicos
  • Uganda
  • Falme za Kiarabu
  • Uingereza
  • Marekani
  • Urugwai
  • Visiwa vya Virgin vya Marekani
  • Vietnamu

Nunua Shukrani Moto

  1. Tumia kompyuta au kifaa cha mkononi ili kufungua video.
  2. Chini ya video, chagua Shukrani Moto.
    • Katika dirisha ibukizi, utapata chaguo tofauti za bei za Shukrani Moto katika nchi au eneo uliko.
  3. Ili ukamilishe ununuzi, fuata maagizo yaliyo kwenye skrini.

Maelezo ya ununuzi

Kuna uhuishaji mwingi unaoweza kununua. Kila mojawapo ina bei tofauti. Ukilipia zaidi, utapata uhuishaji dhahiri zaidi wa Shukrani Moto.
Unaweza kununua Shukrani Moto mara nyingi unavyopenda kwenye video sawa, kwa kutegemea vikomo vya ununuzi vilivyoshirikiwa hapa chini.

Watayarishi hupokea asilimia 70 ya mapato ya Shukrani Moto yanayotambuliwa na Google baada ya kodi ya mauzo na ada zinazotumika za App Store kutozwa kwenye iOS. Kwa sasa gharama za muamala, ikiwa ni pamoja na ada za kadi za mikopo zinashughulikiwa na YouTube.

Maoni

Maoni yanayoonekana kwa umma yatachapishwa katika sehemu ya maoni kwenye video ambako ulinunua Shukrani Moto. Maoni haya ya kipekee, maridadi na yanayoweza kuwekewa mapendeleo yanajumuishwa kwenye ununuzi wako. Ili uwekee mapendeleo maoni yako ya Shukrani Moto, bofya kisanduku cha maandishi au uguse Badilisha karibu na maandishi chaguomsingi. Kumbuka kuwa maoni ya Shukrani Moto yanategemea Mwongozo wa Jumuiya yetu.

Baada ya kukamilisha ununuzi wako, maoni yako yatachapishwa katika sehemu ya maoni ya video yakiwa na chipu maridadi kando yayo. Gharama yako itaweza kuonwa hadharani katika maoni yako.
Jina la kituo chako, picha ya wasifu na gharama ya Shukrani Moto inaweza pia kupatikana kwenye kituo kupitia Huduma ya API ya Data kwenye YouTube. Kituo kinaweza kuchagua kushiriki maelezo haya na huduma za wengine.

Vikomo vya ununuzi

Unaweza kutumia hadi USD $500 kwa siku au USD $2,000 (au kiasi sawa cha sarafu ya nchi ulimo) kila wiki kwenye:

  • Super Chats
  • Super Stickers
  • Shukrani Moto
  • Zote 3 pamoja

Kudhibiti maoni

Lazima maoni yatii Mwongozo wa Jumuiya ya YouTube. Watayarishi na YouTube wanaweza kudhibiti ujumbe wa maoni, ikiwa ni pamoja na maandishi na picha. Maoni yanayodhibitiwa yanaweza kuondolewa yasionekane wakati wowote, kwa sababu yoyote na bila ilani.
Iwapo maoni yaliyochapishwa kupitia ununuzi wa Super Thanks yatafutwa, kudhibitiwa au kuondolewa, hutarejeshewa pesa. Lazima maoni yatii Mwongozo wa Jumuiya ya YouTube. Iwapo maoni yako ya Super Thanks yataondolewa kwa kukiuka sera zetu, YouTube itatoa mchango wa mgawo wetu wa mapato kwa shirika la misaada.

Unaweza kufuta maoni yako baada ya kuchapishwa. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kufuta maoni.

Kurejesha pesa

Malipo ya hiari ya Shukrani Moto hayawezi kurejeshwa. Angalia sera za kurejesha fedha kwenye YouTube ili upate maelezo zaidi. Iwapo unatatizika au una maswali kuhusu malipo, wasiliana na timu yetu ya usaidizi.
Iwapo maoni yaliyochapishwa kupitia ununuzi wa Super Thanks yatafutwa, kudhibitiwa au kuondolewa, hutarejeshewa pesa. Lazima maoni yatii Mwongozo wa Jumuiya ya YouTube.

Stakabadhi za malipo

Baada ya kununua Shukrani Moto, utatumiwa barua pepe yenye stakabadhi ya malipo kama rekodi ya ununuzi.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
13439694052286177517
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false