Historia ya video ulizotazama kwenye YouTube hufanya iwe rahisi kupata video ulizotazama hivi karibuni na ikiwashwa, hukuwezesha kupata mapendekezo ya video zinazokufaa. Unaweza kudhibiti historia ya video ulizotazama kwa kufuta au kuzima kipengele cha historia. Ukifuta baadhi au historia yote ya video ulizotazama, mapendekezo ya video ambayo YouTube itafanya baadaye hayatatokana na maudhui hayo. Video zozote unazotazama wakati historia imezimwa hazitaonekana katika historia yako.
Kuangalia historia ya video ulizotazama
- Ingia katika Akaunti yako ya Google.
- Nenda kwenye myactivity.google.com.
- Bofya Historia ya YouTube.
- Bofya Dhibiti historia ili uone video ulizotazama.
Kufuta historia ya video ulizotazama
- Ingia katika Akaunti yako ya Google.
- Nenda kwenye myactivity.google.com.
- Bofya Historia ya YouTube.
- Bofya Dhibiti historia.
- Bofya FUTA ili uchague muda wa video ambazo ungependa kufuta.
Ukitembelea kichupo cha Historia moja kwa moja kwenye YouTube, huenda pia ukaona chaguo hili likiwa limewasilisha kama uwezo wa kufuta historia ya video ulizotazama.
Kuwasha au kuzima historia ya video ulizotazama
- Ingia katika Akaunti yako ya Google.
- Nenda kwenye myactivity.google.com.
- Bofya Historia ya YouTube.
- Bofya Washa au Zima..
Kwenye ukurasa huu, unaweza pia kuchagua kitu unachopenda kujumuisha kwenye historia ya video ulizotazama wakati imewashwa. Kwa kuchagua kwenye orodha ya chaguo, unaweza kuchagua:
- Kujumuisha video za YouTube unazotazama.
- Kujumuisha mambo unayotafuta kwenye YouTube
- Kujumuisha shughuli za sauti na kutamka kwenye YouTube.
Kuondoa video kwenye historia ya video ulizotazama
- Ingia katika Akaunti yako ya Google.
- Nenda kwenye myactivity.google.com.
- Bofya Historia ya YouTube.
- Bofya Dhibiti historia.
- Bofya kitufe cha kufuta kilicho kando ya video unayotaka kuondoa.
Kutafuta kwenye historia ya video ulizotazama
- Ingia katika Akaunti yako ya Google.
- Nenda kwenye myactivity.google.com.
- Bofya Historia ya YouTube.
- Bofya Dhibiti historia.
- Bofya Tafuta .
Kufuta historia yako ya YouTube kiotomatiki
- Ingia katika Akaunti yako ya Google.
- Nenda kwenye myactivity.google.com.
- Bofya Historia ya YouTube.
- Bofya Dhibiti historia.
- Bofya Futa kiotomatiki.
- Chagua kipindi unachopendelea cha wakati, kisha ubofye Endelea.
- Bofya Thibitisha unapokamilisha.
Televisheni, kifaa cha michezo ya video au kifaa cha kutiririsha maudhui
Kusitisha historia ya video ulizotazama
- Katika Menyu iliyo mkono wa kushoto, nenda kwenye Mipangilio .
- Chagua Kusitisha historia ya video ulizotazama.
- Chagua kitufe cha Kusitisha historia ya video ulizotazama.
Futa historia ya video ulizotazama
- Katika Menyu iliyo mkono wa kushoto, nenda kwenye Mipangilio .
- Chagua kufuta historia ya video ulizotazama.
- Chagua kitufe cha kufuta historia ya video ulizotazama .
Kusimamisha na kufuta historia ya video ulizotazama ukiwa umeondoka kwenye akaunti
Hata kama umeondoka kwenye akaunti, YouTube huboresha mapendekezo yako kulingana na video unazotazama kwenye kifaa hicho.
Kuzima au kufuta historia ya video ulizotazama ukiwa umeondoka kwenye akaunti:
- Nenda kwenye YouTube.
- Chagua Historia.
- Chagua Futa historia ya video zote nilizotazama au Simamisha historia ya video nilizotazama.