Masharti ya maombi ya kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki: Maudhui yasiyo ya video

Unaweza kuomba kuondolewa kwa maudhui yasiyo ya video, kama vile picha ya bango la chaneli, ikiwa unaamini kuwa maudhui haya yanakiuka hakimiliki yako. Maudhui hayo yakiondolewa, onyo la hakimiliki litawekwa kwenye chaneli ya aliyepakia maudhui.

Ili uwasilishe ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki kwa maudhui yasiyo ya video, ni lazima ujumuishe maelezo yanayotakiwa ambayo yameorodheshwa hapa chini. Bila maelezo haya, hatuwezi kuendelea kushughulikia ombi lako. 

Wasilisha maelezo haya kwenye maudhui ya barua pepe (si kwenye kiambatisho) kwa copyright@youtube.com au kupitia faksi au barua.

Kumbuka
  • Huwezi kuwasilisha ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki kwa ajili ya chaneli nzima. Lakini, ikiwa unaamini kuwa vipengee vya chaneli, kama vile maelezo ya chaneli, vinakiuka hakimiliki yako, unaweza kuwasilisha ombi la kuondoa vipengee hivyo kwa kufuata masharti yaliyo hapa chini.
  • Kwa video, njia rahisi zaidi ya kuomba kuondolewa kwa video unayoamini kuwa inakiuka hakimiliki yako ni kwa kutumia fomu yetu ya wavuti. Fomu yetu ya wavuti haikubali maombi ya kuondoa maudhui yasiyo ya video.
Usitume maelezo yasiyo sahihi. Utumiaji mbaya wa michakato yetu, kama vile kutuma hati za ulaghai, unaweza kusababisha kufungwa kwa akaunti yako au kuchukuliwa hatua nyingine za kisheria.

Tuma maelezo yafuatayo ya lazima kwenye maudhui ya barua pepe (si kama kiambatisho) kwa copyright@youtube.com au kupitia faksi au posta:

 1. Maelezo yako ya mawasiliano

YouTube na mpakiaji wa maudhui unayoomba yaondolewe wanaweza kuhitaji kuwasiliana nawe kuhusu ombi lako. Kwenye ombi lako, jumuisha mojawapo ya mambo yafuatayo: 

  • Anwani yako ya barua pepe
  • Anwani yako ya mahali halisi
  • Namba yako ya simu

2. Maelezo ya maudhui yako yaliyo na hakimiliki 

Kwenye ombi lako, hakikisha unaeleza kwa uwazi zaidi na kwa ukamilifu maudhui yako yasiyo ya video yaliyo na hakimiliki unayojaribu kulinda.

Ikiwa unaamini zaidi ya kazi yako moja iliyo na hakimiliki imekiukwa, sheria inaruhusu ujumuishe orodha wakilishi ya kazi hizi kwenye ombi lako.

3. URL maalum za maudhui husika

Ombi lako lazima lijumuishe viungo maalum vya kuelekeza kwenye maudhui yasiyo ya video unayoamini yanakiuka haki zako. Viungo lazima vitumwe katika muundo maalum wa URL. Maelezo ya jumla kama vile jina la chaneli au URL ya chaneli hayatoshi.

Tafuta miundo sahihi ya URL ya kuripoti maudhui yasiyo ya video ya ukiukaji yanayodaiwa hapa chini:

Aina ya maudhui Muundo sahihi wa URL Mahali pa kupata URL
Picha za bango la chaneli

www.youtube.com/channel/UCxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

AU

www.youtube.com/user/xxxxxxxxx

Nenda kwenye ukurasa wa chaneli kishabofya kulia kwenye sehemu ya anwani kisha Nakili.

Maelezo ya chaneli www.youtube.com/user/xxxxxxxxx/about

Nenda kwenye sehemu ya maelezo Kuhusu chaneli kisha bofya kulia kwenye sehemu ya anwani kisha Nakili.

Klipu www.youtube.com/clip/xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Bofya jina la klipu kisha bofya kulia kwenye sehemu ya anwani kisha Nakili.
Maoni ya Video www.youtube.com/watch?v=xxxxxxxxxx&lc=xxxxxxxxxxxxxxxxxx Bofya tarehe iliyochapishwa juu ya maoni (ukurasa utapakiwa upya) kisha bofya kulia kwenye sehemu ya anwani kisha Nakili.
Chapisha Maoni www.youtube.com/channel/xxxxxxxxxxx/community?lc=xxxxxxxxxxxx&lb=xxxxxxxxxxxx Bofya tarehe iliyochapishwa juu ya maoni (ukurasa utapakiwa upya) kisha bofya kulia kwenye sehemu ya anwani kisha Nakili.
Machapisho ya jumuiya https://www.youtube.com/post/xxxxxxxxxxxxxxxxxxx Bofya tarehe ya kuchapisha chapisho la jumuiya (ukurasa utapakiwa upya) kisha bofya kulia kwenye sehemu ya anwani kisha Nakili.
Maelezo ya beji za uanachama, emoji au manufaa ya mtayarishi Ukianza na yt3.ggpht.com/xxxxx Bofya kulia kwenye picha kisha Nakili Anwani ya Picha

Jumuisha pia URL ya chaneli:

www.youtube.com/channel/UCxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

AU

www.youtube.com/user/xxxxxxxxx

Nenda kwenye ukurasa wa chaneli kishabofya kulia kwenye sehemu ya anwani kisha Nakili.
Maelezo ya orodha ya video

www.youtube.com/playlist?list=xxxxxxxxxxxxxxxx

Bofya jina la orodha ya video kisha bofya kulia kwenye sehemu ya anwani kisha Nakili.

Picha za wasifu
Super Stickers Beginning with lh3.googleusercontent.com/xxxxx Bofya alama ya dola  kwenye gumzo la moja kwa moja kisha Super Sticker kisha bofya kulia kwenye picha kisha Nakili Anwani ya Picha.

Jumuisha pia URL ya chaneli:

www.youtube.com/channel/UCxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

AU

www.youtube.com/user/xxxxxxxxx

Nenda kwenye ukurasa wa chaneli kisha bofya kulia kwenye sehemu ya anwani kisha Nakili.

4. Kubali na ujumuishe taarifa mbili zifuatazo:

“Ninaamini kwa nia njema kuwa matumizi ya nyenzo kwa namna iliyolalamikiwa hayajaruhusiwa na mmiliki wa hakimiliki, wakala wake au sheria.”

"Maelezo yaliyo kwenye arifa hii ni sahihi, na chini ya adhabu ya kusema uongo, mimi ni mmiliki au mwakilishi rasmi niliyeidhinishwa kutenda kwa niaba ya mmiliki wa haki ya kipekee inayodaiwa kukiukwa.”

5. Sahihi yako

Maombi ya uondoaji yaliyokamilishwa yanahitaji sahihi halisi au ya kielektroniki ya mmiliki wa hakimiliki au mwakilishi rasmi aliyeidhinishwa kutenda kwa niaba yake.

Ili kutimiza masharti haya, mmiliki wa hakimiliki au mwakilishi rasmi aliyeidhinishwa anaweza kuweka jina lake rasmi kamili kama sahihi yake katika sehemu ya chini ya ombi. Jina rasmi kamili linapaswa kuwa jina la kwanza na la mwisho, si jina la kampuni.

Tuma maelezo yote ya lazima yaliyo hapo juu kwenye maudhui ya barua pepe (si kama kiambatisho) kwa copyright@youtube.com au uyatume kupitia faksi au posta.

Maelezo zaidi  

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
14305764505194830035
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false