Kuongeza wimbo wa sauti kwenye video yako

Huwezi tena kubadilisha wimbo wa sauti wa video yako kwenye programu ya YouTube ya vifaa vya mkononi. Tumia kompyuta kubadilisha wimbo wa sauti kwenye Studio ya YouTube.

Kihariri cha video cha Studio ya YouTube hukuwezesha kuongeza muziki kwenye video yako kutoka katika maktaba ya nyimbo zilizopewa leseni. Nyimbo hizi zinapatikana kwenye Maktaba ya Sauti ya YouTube. Unaweza kutumia nyimbo zilizo kwenye Maktaba ya Sauti katika video zinazotumika kuchuma mapato.

Pata maelezo kuhusu jinsi ya kupakia nyimbo za sauti zenye lugha nyingi kwenye video zako.

Kumbuka:
  • Ikiwa video yako imetazamwa zaidi ya mara 100,000, huenda usiweze kuhifadhi mabadiliko kwenye video zako. Kikwazo hiki hakitumiki kwa watumiaji walio katika Mpango wa Washirika wa YouTube.
  • Kipengele hiki kinatumika tu kwa video zisizozidi saa 6.

Ongeza wimbo wa sauti kwenye video yako

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui.
  3. Bofya video ambayo ungependa kuhariri.
  4. Kwenye menyu ya kushoto, bofya Kihariri.
  5. Chagua Sauti  kisha utumie vichujio vya utafutaji kutafuta wimbo mpya wa sauti. Bofya Cheza ili uone onyesho la kukagua nyimbo.
  6. Unapopata wimbo unaopenda, bofya ONGEZA. Wimbo utaonekana kwenye kihariri katika kisanduku cha buluu.
    • Buruta kisanduku ili ubadilishe mahali pa wimbo kuanzia.
    • Buruta kingo za kisanduku ili ubadilishe urefu wa wimbo.
    • Tumia chaguo za kukuza Zoom in ili urekebishe kwa usahihi zaidi.
  7. Ukikamilisha, bofya HIFADHI.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
2310284808771494266
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false