Wasiliana na watazamaji kwenye Machapisho ya jumuiya

Baada ya kuweka machapisho kwenye kichupo cha Jumuiya kwenye kituo chako, watazamaji wanaweza kutoa maoni ili kujibu. Pata maelezo kuhusu jinsi watazamaji wanavyoweza kujibu machapisho yako.

Kumbuka: Ufikiaji wa Chapisho la jumuiya unaweza kubadilika kulingana na jukumu la chaneli yako. Pata maelezo zaidi kuhusu ruhusa za chaneli.

Tafuta Machapisho yako ya jumuiya

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui.
  3. Gusa kichupo cha Machapisho.

Kumbuka: Unaweza kuangalia machapisho yoyote ambayo muda wake umekwisha kwenye kumbukumbu yako. Nenda kwenye kichupo cha Jumuiya yako kisha uchague sehemu ya "Kumbukumbu".

Jibu maoni kwenye machapisho yako

Jibu maoni kwenye machapisho yako ili uanzishe mazungumzo na hadhira yako.

  1. Wekelea kiashiria juu ya chapisho kisha ubofye Maoni . Utaona ukurasa wa Maoni ya Chapisho.
  2. Chagua Jibu chini ya maoni yoyote.

Utapokea arifa mara kwa mara kuhusu maoni kwenye Machapisho yako ya jumuiya usipojiondoa. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kudhibiti arifa zako.

Kidokezo: Kujibu maoni ya hivi karibuni, bofya  Panga kulingana na kisha Mapya zaidi kwanza.

Badilisha mipangilio ya maoni ya Chapisho la jumuiya

Iwapo unataka kubadilisha mipangilio ya maoni kwa chapisho mahususi:

  1. Kwenye kompyuta yako, ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui.
  3. Chagua Machapisho.
  4. Tafuta chapisho ambalo ungependa kusasisha, kisha uchague Maelezo .
  5. Chagua mipangilio yako ya maoni.
  6. Chagua HIFADHI.

Pata maelezo zaidi kuhusu mipangilio ya maoni, ikijumuisha chaguo zako za kudhibiti maoni ikiwa kipengele cha maoni kimewashwa.

Kumbuka: Chaguo la “Sitisha” halipatikani kwa sasa kwa Machapisho ya jumuiya.

Bandika maoni kwenye machapisho yako

Unaweza kuchagua maoni (yako au ya mtazamaji) yabaki katika sehemu ya juu ya mipasho kwa kuyabandika. Kubandika maoni kunafanya yaonekane zaidi kwa hadhira yako.

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui.
  3. Chagua kichupo cha Machapisho.
  4. Wekelea kiashiria juu ya chapisho kisha ubofye Maoni .
  5. Wekelea kiashiria juu ya maoni ambayo ungependa kubandika.
  6. Bofya Zaidi Bandika. Iwapo tayari kuna maoni uliyobandika, yatabadilishwa, hatua hii itayabadilisha na kuweka mengine.
    Kumbuka: Unaweza Kubandua maoni wakati wowote na maoni hayo yatarejeshwa kwenye nafasi yake halisi.

Dhibiti maoni kwenye Machapisho ya jumuiya

Unaweza kuzuia maoni kwenye Machapisho yako ya jumuiya ili uyakague. Pata maelezo zaidi kuhusu kudhibiti maoni.

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Mipangilio.
  3. Chagua Jumuiya kisha Mipangilio chaguomsingi.
  4. Chini ya sehemu ya "Maoni kwenye chaneli yako," chagua mipangilio yako.
  5. Chagua Hifadhi.

Weka alama za mioyo kwenye machapisho

Unaweza kutumia alama ya moyo ili kuonyesha shukrani kwa maoni ya mtazamaji kwenye machapisho ya kichupo chako cha Jumuiya. Pata alama ya moyo karibu na alama ya kupenda na kutopenda.

Watazamaji wataona picha yako na alama ya moyo mdogo mwekundu katika sehemu ya chini kushoto ya maoni yao. Kulingana na mipangilio yao, wanaweza pia kupokea arifa ya kuwajulisha kuwa mmiliki wa kituo amependa maoni yao.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
14033624017558825159
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false