Kuanza kutumia huduma ya YouTube BrandConnect

YouTube BrandConnect ni mfumo wa kujihudumia unaowaunganisha watayarishi na fursa za kushiriki kwenye kampeni za maudhui yaliyo na chapa. Biashara zinaweza kutumia dashibodi tunayomiliki ya ushawishi ili kutekeleza kampeni zao za maudhui ya kibiashara na kutambua watayarishi wa kufanya nao kazi.

Mfumo wa YouTube BrandConnect unaangazia:

  • Fursa za kuchuma mapato kwa kutumia kampeni za maudhui yaliyo na chapa zinazolingana na mapendeleo yako
  • Zana za kujihudumia ndani ya Studio ya YouTube ili kudhibiti kampeni
  • Muhtasari wa Kutangaza unaoweza kuwekwa mapendeleo, ulio na maarifa kuhusu hadhira iliyobuniwa kulingana na chaneli yako, ili uweze kujitambulisha kwa biashara na kupata ofa za kutangaza. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kutumia Muhtasari wako wa Kutangaza.
  • Mbinu na nyenzo bora za kusaidia kukuongoza

Ukiwa na huduma ya YouTube BrandConnect, unaweza kudhibiti kampeni zako ipasavyo, kuhifadhi udhibiti wa ubunifu na kuchagua wa kufanya naye kazi.

Upatikanaji na masharti ya kujiunga

Huduma ya YouTube BrandConnect ipo katika toleo la Beta na inapatikana tu kwa watayarishi wanaotimiza masharti katika mojawapo ya nchi au maeneo ambako huduma hii inapatikana kwa wakati huu.

Ili ushiriki kwenye mfumo wa YouTube BrandConnect, ni lazima chaneli yako itimize masharti haya ya msingi ya kujiunga:

Ni lazima chaneli yako pia ifuate sera za uchumaji wa mapato za YouTube, ikiwa ni pamoja na:

Upatikanaji

Huduma ya YouTube BrandConnect inapatikana kwa watayarishi wanaotimiza masharti katika nchi au maeneo yafuatayo:
  • Brazili
  • India
  • Indonesia
  • Uingereza
  • Marekani

Kuwasha huduma ya YouTube BrandConnect

Ili uwashe huduma ya YouTube BrandConnect kwenye Chaneli yako ukitumia kompyuta:

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, bofya Chuma mapato.
  3. Bofya kichupo cha BrandConnect. Kichupo hiki kitaonekana tu iwapo chaneli yako imetimiza masharti.
  4. Kwenye sehemu ya juu ya skrini, bofya Anza au katika sehemu ya chini ya skrini bofya Hebu tuanze.
  5. Kagua na ukubali Sehemu ya huduma ya YouTube BrandConnect.

Ili uwashe huduma ya YouTube BrandConnect kwenye chaneli yako ukitumia kifaa cha mkononi:

  1. Fungua programu ya vifaa vya mkononi ya Studio ya YouTube .
  2. Kwenye menyu ya chini, gusa Chuma mapato.
  3. Gusa kadi ya BrandConnect . Kadi hii itaonekana tu iwapo chaneli yako imetimiza masharti.
  4. Gusa Washa.
  5. Kagua na ukubali Sehemu ya huduma ya YouTube BrandConnect.
Kumbuka: Mitandao ya Chaneli Mbalimbali haiwezi kukubali Sehemu ya huduma ya YouTube BrandConnect.

Kudhibiti huduma ya YouTube BrandConnect

Weka mapendeleo yako

Baada ya kukubali Sehemu ya huduma ya YouTube BrandConnect, unaweza kupata fursa za maudhui ya kibiashara. Biashara sasa zinaweza kukugundua, lakini kujisajili hakukuhakikishii fursa za kupata maudhui ya kibiashara.

Fursa kutoka kwenye biashara zinaonyeshwa moja kwa moja kwenye Studio ya YouTube ambapo unaweza kukagua maelezo. Mapendeleo yako yatachuja kiotomatiki fursa ili kuhakikisha kuwa zinafaa na zina bei inayokubalika. Unaweza kubadilisha mapendeleo yako ili kuboresha maudhui yako yanayolingana ili yaendane na mahitaji yako:

  1. Nenda kwenye sehemu ya Kuchuma mapato ya Studio ya YouTube.
  2. Chagua huduma ya BrandConnect and then Weka mapendeleo.

Kudhibiti ofa

Unaweza kuangalia maelezo kwa kila fursa kwenye dashibodi yako kwa kubofya ANGALIA MAELEZO. Kila fursa inajumuisha muhtasari wa kiwango cha juu wa ratiba ya kampeni. Ratiba ya kampeni hukuruhusu ufanyie kazi mkataba na kuangalia mahali ulipo kwenye mchakato. Ratiba ya kampeni itajumuisha hatua tatu za kiwango cha juu: ofa, video ya kampeni na utendaji wa kampeni.

Ofa

Sehemu ya "Ofa" itaonyesha maelezo ya kampeni yako na itajumuisha maelezo zaidi kuhusu biashara:

Bei

Kiasi cha pesa unachoweza kupata kwenye ofa hii. Kiasi cha mwisho unachoweza kupata kutokana na ofa kitatofautiana kulingana na mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na, lakini si tu ukubwa wa kampeni na ufikiaji wa watayarishi. Unaweza kufanya majadiliano ya bei kwa kila fursa.

Muhtasari Muhtasari wa kampeni na bidhaa au huduma kutoka kwa biashara. Sehemu hii itajumuisha mawazo yoyote ambayo biashara ingependa utume kwa watazamaji na kitendo ambacho biashara ingependa uwahimize watazamaji watetekeleze.
Muhtasari wa yanayotarajiwa Unachopaswa kuwasilisha kwenye biashara kwa ajili ya kampeni.
Maelezo ya bidhaa Maelezo ya bidhaa au huduma uliyopewa na biashara kwa lengo la kupata huduma zako.

Kuhusu (biashara)

Muhtasari wa kiwango cha juu wa biashara na kiungo cha tovuti ya biashara.

Kujibu maombi ya Ofa 

Iwapo unaishi Marekani, hatua unazoweza kuchukua kwenye ofa zitategemea masharti yako na iwapo Google au biashara inatoa ofa hiyo. 

Iwapo umetia sahihi kwenye sheria na masharti ya Sehemu ya huduma ya YouTube BrandConnect na umepewa ofa moja kwa moja na biashara, unaweza kuchukua hatua zifuatazo kwenye ofa hiyo:

  • Ningependa kushiriki: Ukichagua ningependa kushiriki, tutatuma maelezo yako ya mawasiliano kwa biashara ili wawasiliane nawe na mjadiliane kuhusu ofa. Ofa hiyo itajumuisha masharti ya kulipa, bei na yaliyomo kwenye makubaliano. Ili uendelee na ofa, utatia sahihi kwenye makubaliano unayoingia moja kwa moja na biashara na utalipwa na biashara hiyo. Hakikisha kuwa unaelewa masharti ya makubaliano yoyote unayoingia na biashara.
  •  Ninakataa: Ukichagua Ninakataa, tutaifahamisha biashara kuwa hungependa kuendelea na makubaliano.

Iwapo umetia sahihi sheria na masharti ya toleo la Beta la Mfumo wa Kujihudumia wa YouTube BrandConnect, unaweza kupewa ofa kutoka Google, zinazojumuisha bei itakayolipwa na Google kwenye akaunti yako ya AdSense katika YouTube. Unaweza kuchukua hatua zifuatazo kwenye ofa kama hii: 

  • Kukubali: Ukichagua Kubali, utaombwa utie sahihi kwenye makubaliano unayoingia na biashara husika. Ukitimiza masharti ya makubaliano, utalipwa na Google kwa kushiriki. Hakikisha kuwa unaelewa masharti ya makubaliano yoyote unayoingia na biashara.
  • Kupendekeza bei tofauti: Ukichagua Pendekeza bei tofauti, unaweza kujadili bei mpya ili ushiriki kwenye fursa.  
  • Kujadili: Ukichagua Jadili, unaweza kuwasiliana na biashara ili upate maelezo zaidi kuhusu ofa.
  • Kukataa: Ukichagua Kataa, tutaifahamisha biashara kuwa hungependa kuendelea na makubaliano.

Video ya kampeni

Ukishakubali ufadhili wa kibiashara, unaweza kuandaa maudhui ya kampeni yako. Sehemu ya "Video ya kampeni" inabainisha hatua zinazofuata ili upakie maudhui yako, katika hali ya Hayajaorodheshwa na uyawasilishe kwa biashara ili yakaguliwe na yaidhinishwe. Ikiwa biashara ina maoni yoyote, utapokea barua pepe yenye maoni ya mshirika wa biashara yako.

Pamoja na ukaguzi wa biashara, maudhui yako pia yanakaguliwa kwa mujibu wa Sera za Google Ads na Mwongozo wa Jumuiya. Baada ya maudhui yako kuidhinishwa kikamilifu, unapokea barua pepe na arifa ya hali kwenye Studio ya YouTube. Unaweza kuchapisha maudhui yako papo hapo au kuratibu muda unaotaka yatiririshwe moja kwa moja. Hakikisha unachapisha kulingana na ratiba uliyokubaliana na biashara.

Utendaji wa kampeni

Sehemu ya “Utendaji wa kampeni” hukupa muhtasari wa kiwango cha juu wa utendaji wa maudhui yako, ikiwa ni pamoja na, lakini si tu:

  • Siku zilizosalia kwenye kampeni yako
  • Mara ambazo maudhui yako yametazamwa
  • Alama za nimeipenda

Unaweza pia kutazama maelezo zaidi kuhusu utendaji wa maudhui yako kwenye Takwimu za YouTube.

Maswali Yanayoulizwa Sana

Ninawezaje kushiriki kwenye huduma ya YouTube BrandConnect?

Kwa sasa, huduma ya YouTube BrandConnect iko kwenye toleo la Beta na inapatikana tu kwa kikundi kidogo cha watayarishi walio nchi au maeneo ambako huduma inapatikana. Ikiwa umetimiza masharti ya toleo la Beta, kichupo cha BrandConnect kitaonekana kwenye Studio ya YouTube. Tunatarajia kusambaza kipengele hiki kwa watayarishi na nchi au maeneo zaidi hivi karibuni.

Je, mawakala au wasimamizi wanaweza kutumia huduma ya YouTube BrandConnect kwa watayarishi wao?

Ndiyo. Tunatuma arifa za barua pepe kuhusu fursa mpya kwenye anwani ya barua pepe inayohusiana na chaneli. Ikiwa mtayarishi anataka upate arifa hizi za barua pepe, anaweza kubadilisha anwani ya barua pepe inayohusiana na chaneli yake. Mtayarishi wako anaweza pia kukuweka kama mtumiaji aliyeidhinishwa ili uweze kudhibiti ofa zake moja kwa moja kwenye Studio ya YouTube.

Je, ninaweza kuangalia wapi mapato yangu kutoka kwenye huduma ya YouTube BrandConnect?

Kwa ofa zinazotolewa moja kwa moja kutoka Google na kutegemea Sheria na Masharti ya toleo la Beta la Mfumo wa Kujihudumia wa huduma ya YouTube BrandConnect, unaweza kuangalia mapato yako kwenye Takwimu za YouTube. Chagua wakati unaofaa, na safu mlalo ya “mapato ya huduma ya YouTube BrandConnect” itaonekana kwenye kadi. Pata maelezo zaidi kuhusu vyanzo vya mapato yako.
Iwapo ulitia sahihi makubaliano moja kwa moja na biashara, mapato yako kutokana na ofa hiyo hayataonekana kwenye Takwimu za YouTube.
 

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
13447441316322437336
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false