Unaweza kudhibiti na kupata maelezo zaidi kuhusu mipangilio yako ya faragha na vidhibiti chini ya "Data yako kwenye YouTube". Ukurasa huu unajumuisha muhtasari wa maudhui yako na data ya shughuli, mipangilio ya kusimamia data hii na maelezo ya jinsi data yako inavyotumika kuboresha hali yako ya utumiaji wa YouTube.
Kumbuka: Kipengele hiki kwa sasa kinapatikana tu kwenye kompyuta ya mezani na wavuti wa vifaa vya mkononi.
Ili kufikia “Data yako kwenye YouTube”:
- Ingia kwenye YouTube.
- Chagua picha ya wasifu wako .
- Chagua “Data yako kwenye YouTube.”
Kwenye “Data yako kwenye YouTube”, unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kudhibiti:
- Mipangilio ya faragha ya video
- Mipangilio ya faragha ya orodha ya kucheza
- Mipangilio ya faragha ya Usajili
- Video zilizonunuliwa
- Maoni
Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi data yako inavyosaidia kuboresha hali yako ya utumiaji kwenye YouTube.