Kuelewa takwimu za mapato ya matangazo

Unaweza kuangalia mapato yako kwenye YouTube na utendaji wa chaneli yako kupitia vipimo vinavyopatikana katika sehemu ya Takwimu za YouTube. Baadhi ya vipimo vinaonekana kufanana, lakini tofauti zao ni muhimu katika kuelewa mapato yako ya matangazo kwenye YouTube.

RPM

Mapato kwa Kila Mara Elfu Moja za Kutazamwa (RPM) ni kipimo kinachoonyesha kiasi cha pesa ulichopata video ilipotazamwa kila mara elfu 1,000. RPM inategemea vyanzo kadhaa vya mapato ikijumuisha: Matangazo, Uanachama katika kituo, mapato ya YouTube Premium, Super Chat na Super Stickers.

Je, kwa nini RPM yangu iko chini ikilinganishwa na CPM?

RPM iko chini kuliko CPM kwa sababu RPM:
  • inakokotolewa baada ya ugavi wa mapato kwenye YouTube.
  • inajumuisha mara zote ambazo video imetazamwa, ikiwemo mara ambazo video ilitazamwa bila kuchuma mapato.
Kiasi cha mapato yako hakijabadilishwa kama sehemu ya nyongeza ya kipimo cha RPM.

Je, kuna tofauti gani kati ya RPM na CPM?

CPM ni gharama kwa maonyesho 1000 ya matangazo kabla ya ugavi wa mapato kwenye YouTube. RPM ni mapato yako ya jumla (baada ya ugavi wa mapato kwenye YouTube) kwa kila mara 1000 ambapo video inatazamwa.

RPM

CPM

  • Kipimo kinacholenga watayarishi
  • Inajumuisha mapato ya jumla yaliyoripotiwa kwenye Takwimu za YouTube ikiwemo matangazo, YouTube Premium, Uanachama katika Chaneli, Super Chat na Super Stickers.
  • Inajumuisha mara zote ambazo video zako zimetazamwa, ikiwemo mara ambazo video ilitazamwa bila kuchuma mapato.
  • Kiasi halisi ulichopata baada ya ugavi wa mapato.
  • Kipimo kinacholenga watangazaji
  • Inajumuisha tu mapato kutoka kwa matangazo na YouTube Premium
  • Inajumuisha tu mara ambazo video zinazochuma mapato zilitazamwa (yaani matangazo yalionyeshwa)
  • Kiasi ulichopata kabla ya ugavi wa mapato

Je, kwa nini RPM ni muhimu?

RPM hukuwezesha kuona pesa unazopata video inapotazamwa kila mara 1,000. Pia, hukuwezesha kufahamu ufanisi wa uchumaji wako wa mapato kwa ujumla.

Je, ninawezaje kuongeza RPM yangu?

Ili kuboresha RPM yako, unapaswa kuboresha mapato yako ya jumla. Zifuatazo ni baadhi za hatua unazoweza kuchukua kuboresha RPM:
  • Washa uchumaji wa mapato kwenye video zote.
  • Washa matangazo yanayochezwa katikati ya video.
  • Washa vipengele vya AltMon (kwa mfano, uanachama, Super Chat) ili uwe na vyanzo anuwai vya mapato.

Kumbuka kuwa kila kipengele kina masharti na mwongozo wake.

Je, kupanda au kushuka kwa RPM kunamaanisha nini?

RPM ni muhtasari wa kiwango chako cha uchumaji wa mapato kwenye YouTube. Ikiongezeka, inamaanisha unapata pesa zaidi video inapotazamwa kila mara 1000 , na ikishuka inaonyesha mapato yako yamepungua. Kumbuka, RPM yako huenda ikapungua iwapo video inatazamwa mara nyingi bila kuchuma mapato, hata ikiwa kiasi cha mapato yako hakijabadilika.
Kupanda na kushuka RPM kunadhihirisha ufanisi au udhaifu wa mikakati yako wa uchumaji wa mapato. Kuelewa yanayoathiri RPM kunaweza kukusaidia kufahamu jinsi ya kuboresha mikakati yako ya uchumaji wa mapato.

Je, RPM inaonyesha nini kuhusu mapato yangu?

RPM ni kipimo muhimu cha uchumaji wa mapato kwa watayarishi, lakini haionyeshi hali ya mapato kwa kina. Haijumuishi yafuatayo:

  • Mapato yanayotokana na uuzaji wa bidhaa au matumizi ya rafu ya bidhaa.
  • Mapato yanayotokana na ufadhili wa kibiashara na wa kawaida (bila kujumuisha YouTube BrandConnect).
  • Mapato mengine yoyote yanayotokana na YouTube kwa njia isiyo ya moja (ada za ushauri, huduma, kuzungumza).

RPM haibainishi chanzo cha mapato kinachosababisha kubadilika kwa mapato yako kwa ujumla

Kwa sababu RPM inajumuisha vipimo kadhaa, haibainishi chanzo cha mapato kinachosababisha kubadilika kwa kiwango cha mapato yako.

Kwa mfano, RPM yako inaweza kupungua licha ya kuongezeka kwa mara ambazo video imetazamwa kwa sababu matangazo hayakuonyeshwa kila wakati video ilipotazamwa. Au, RPM yako inaweza kuongezeka licha ya kutoongezeka sana kwa mara ambazo video imetazamwa kwa sababu watazamaji wanajisajili kwa Uanachama katika Kituo.

Tunapendekeza utumie takwimu zote zinazotolewa na YouTube ili uelewe kikamilifu mabadiliko ya RPM yako.

CPM

Gharama kwa kila maonyesho 1,000 (CPM) ni kipimo kinachoonyesha kiasi cha pesa ambacho watangazaji hulipa kuonyesha matangazo kwenye YouTube. Utaona vipimo kadhaa tofauti vya CPM kwenye Takwimu za YouTube:

  • CPM: Gharama ambayo mtangazaji hulipia maonyesho 1,000 ya tangazo. Onyesho la tangazo hukokotolewa kila wakati tangazo linapoonyeshwa.
  • CPM kulingana na uchezaji: Gharama ambayo mtangazaji hulipia ili tangazo lake lionyeshwe video inapochezwa mara 1,000.

Je, kuna tofauti gani kati ya CPM na CPM kulingana na uchezaji?

Video kwenye YouTube zinaweza kuwa na zaidi ya tangazo moja. CPM inaangazia gharama ambayo mtangazaji hulipia maonyesho ya tangazo. CPM kulingana na uchezaji inaangazia gharama ambayo mtangazaji hulipia maonyesho ya tangazo moja au zaidi video inapochezwa. Mara nyingi, CPM yako inayolingana na uchezaji huwa juu kuliko CPM.
Kwa mfano, chukulia kuwa video yako imetazamwa mara 5,000. Tangazo moja lilionyeshwa watu 1,000 wakitazama video, nayo matangazo mawili yakaonyeshwa watu wengine 500 wakitazama video, hivyo matangazo yalionyeshwa mara 1,500 video ikitazamwa. Hii inamaanisha kulikuwa na maonyesho 2,000 ya matangazo, lakini uchezaji wa video uliochuma mapato ulikuwa 1,500 pekee.
Hebu tuchukulie mtangazaji alilipa jumla ya $7. Gharama ya video kwa kila onyesho itakuwa gharama ya mtangazaji ambayo ni $7 kisha igawanywe kwa maonyesho 2,000 ya matangazo, au, $0.0035. CPM, au gharama kwa kila maonyesho 1000, basi itakuwa $0.0035 mara 1,000, au, $3.50. CPM kulingana na uchezaji itakuwa $7 kisha igawanywe kwa uchezaji 1,500 wa uchumaji mapato, halafu izidishwe mara 1,000, au $4.67.

Je, CPM ina umuhimu gani?

Inakuwezesha kufahamu kiwango ambacho watangazaji hulipia tangazo kuonyeshwa kwenye video yako. Kadri mtangazaji anavyolipia tangazo kiwango cha juu, ndivyo unavyopata pesa nyingi. CPM yako ni kiashirio kizuri cha ufaafu wa video zako na hadhira yako katika kuwawezesha watangazaji kufikia malengo yao ya biashara.
Mapato yako hayatokani na kuzidisha CPM yako na mara ambazo video zimetazamwa, kwa sababu CPM haionyeshi mapato yako bali kiasi walicholipa watangazaji. Pia, matangazo yanaweza kukosa kuonyeshwa kila wakati video inapotazamwa. Endapo video ina maudhui yasiyowafaa watangazaji, haistahiki kuonyesha matangazo kabisa. Wakati mwingine, huenda kusiwepo na tangazo la kuonyeshwa video inapochezwa. Utazamaji video unaojumuisha matangazo unajulikana kama uchezaji wa video unaochuma mapato

Je, kwa nini CPM yangu inabadilika?

Ni kawaida kwa CPM kubadilika baada ya muda fulani, na hili hutokana na sababu kadhaa, kama vile:
  • Wakati wa mwaka: Bei za watangazaji huwa juu au chini kulingana na wakati wa mwaka. Kwa mfano, watangazaji wengi hutoa bei ya juu kabla ya kipindi cha likizo.
  • Mabadiliko ya mahali watazamaji waliko: Watangazaji wanaweza kubainisha maeneo ambako wangependa matangazo yao yaonyeshwe. Katika utangazaji, kiwango cha ushindani ni tofauti katika maeneo mbalimbali, kwa hivyo CPM zitatofautiana kulingana na eneo la kijiografia. Iwapo watazamaji wengi wako kwingine, huenda CPM ikabadilika. Kwa mfano, ikiwa hapo awali utazamaji ulikuwa juu katika eneo lenye CPM za juu, lakini kwa sasa utazamaji umeongezeka katika maeneo yenye CPM za chini, huenda CPM yako ikapungua.
  • Mabadiliko katika usambazaji wa miundo inayopatikana ya matangazo: Aina tofauti za matangazo huwa na CPM tofauti. Kwa mfano, iwapo kuna matangazo mengi yasiyoweza kurukwa kwenye orodha ya matangazo, huenda CPM ikawa juu.

Makadirio ya mapato ikilinganishwa na mapato ya matangazo

  • Makadirio ya mapato: Mapato yote kwa ujumla ikijumuisha uanachama katika kituo, mapato ya YouTube Premium na Super Chat. Utaona kipimo hiki kwenye kichupo cha Mapato.
  • Makadirio ya mapato ya matangazo: Mapato yanayotokana tu na matangazo kwenye video zako. Utaona kipimo hiki kwenye ripoti ya vyanzo vya mapato.

Mara ambazo video ilitazamwa, maonyesho ya matangazo na makadirio ya uchezaji wa video unaochuma mapato

  • Mara za kutazamwa: Mara ambazo video yako ilitazamwa.
  • Maonyesho ya matangazo: Mara ambazo matangazo mahususi yalitazamwa kwenye video zako.
  • Kadirio la uchezaji wa video unaochuma mapato: Mara ambazo matangazo yalionyeshwa kwenye video yako.

Video yako ikitazamwa mara 10, na mara 8 kati ya hizo matangazo yaonyeshwe, video itakuwa imetazamwa mara 10 na imechuma mapato mara 8. Endapo kati ya mara hizo nane za video kuchuma mapato kulikuwa na matangazo 2, utakuwa na maonyesho 9 ya matangazo.

Matangazo hayaonyeshwi kila wakati video inapotazamwa. Huenda video isionyeshwe ikiwa:

  • Video ina maudhui yasiyowafaa watangazaji.
  • Matangazo yamezimwa kwenye video hiyo.
  • Hakuna tangazo linalopatikana kwa kikundi mahususi cha watazamaji. Mtangazaji anaweza kuamua kulenga watumiaji wa vifaa mahususi, demografia maalum na mambo fulani mahususi. Huenda tangazo hilo lisimfae mtazamaji husika. Pata maelezo zaidi kuhusu mbinu za kuonyesha matangazo ya video kwa hadhira lengwa.
  • Vigezo vingine mbalimbali, kama vile mahali mtazamaji aliko, mara ya mwisho kuona tangazo, usajili wa Premium, na kadhalika.

Kwa sababu hizi, huenda mara ambazo video imetazamwa ikawa juu kuliko uchezaji wa video unaochuma mapato.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
12353587567291034267
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false