Kuwasha DVR kwenye mitiririko mubashara.

Kuwasha kipengele cha DVR cha YouTube huruhusu watazamaji wako kusitisha, kurudisha nyuma na kuendelea kutazama wakati mtiririko mubashara unaendelea. Pindi mtazamaji anapoendelea kucheza, mtiririko mubashara utaendelea kuanzia alikousitishia. Ili kuwasha DVR, fuata hatua hizi:

 
  1. Nenda kwenye Studio ya YouTube.
  2. Bofya Tayarisha kisha Tiririsha mubashara.
  3. Anzisha mtiririko mubashara sasa kwenye kichupo cha Mtiririko au uratibu mtiririko mubashara kwenye kichupo cha Dhibiti.
  4. Kwenye dashibodi ya mtiririko, bofya Washa DVR.

Vikomo

Ikiwa mtiririko wako mubashara utaendelea kwa muda mrefu sana, watazamaji wako wataweza tu kurudisha nyuma kwa kiasi fulani kwa kuwa uwezo wa Kirekodi Video cha Dijitali (DVR) unaweza kuwa umedhibitiwa au usipatikane kwa mitiririko inayozidi saa 12. Kutazama kwenye Apple TV, Apple AirPlay au matoleo ya awali ya programu kuna vikomo vya chini zaidi.

Vikomo hivi pia hutumika mtumiaji anapotumia kipengele cha kusitisha na kuendelea kucheza. Watazamaji hawawezi kusogeza nyuma hadi muda kabla uanze kutiririsha mubashara.

Kuzima DVR 

Ukichagua kuzima DVR, watazamaji hawawezi kusogeza nyuma wakati unatiririsha, lakini bado watazamaji wanaweza kurekodi mtiririko wako wote utakapopatikana. Kipengele cha kuzima DVR hakitumiki kwenye utiririshaji kupitia kamera ya wavuti na kwenye kifaa cha mkononi.

Ukibadilisha mawazo yako kuhusu DVR baada ya kuanza kutiririsha, bado unaweza kuwasha au kuzima wakati unatiririsha mubashara. Hata hivyo, mabadiliko yatatumika tu kwa watumiaji watakaoanza kucheza mtiririko wako baada ya wewe kufanya mabadiliko.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
12531581658185856611
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false