Kuwasha au kuzima Super Chats na Super Stickers

Super Chats na Super Stickers ni njia za kuchuma mapato kwenye kituo chako. Vipengele hivi huwawezesha watazamaji wako kununua ujumbe wa gumzo wa kipekee na wakati mwingine, kuubandika juu ya mipasho ya gumzo. Pata maelezo zaidi kuhusu ustahiki.

Kumbuka kuwa una wajibu wa kutii sheria zote zinazotumika wakati unapotumia Super Chat na Super Stickers. Sheria hizi zinaweza kunaini kama unaweza kuwasha, kutoa, kutuma na kupata pesa kutoka kwenye Super Chats na Super Stickers.

Super Chat na Super Stickers: Mipangilio na Vidokezo vya Kuzitumia

 

Kuwasha au kuzima Super Chat au Super Stickers kwenye kituo chako

Kuwasha Super Chat au Super Stickers

Ili kuchuma mapato kutokana na Super Chat au Super Stickers, ni lazima wewe (na Mtandao wako wa Vituo Mbalimbali) kwanza mkubali Sehemu ya Bidhaa za Biashara (CPM). Ili upate maelezo zaidi kuhusu CPM, angalia sera zetu za uchumaji wa mapato katika Bidhaa za Biashara kwenye YouTube.

Iwapo ungependa kutumia kompyuta ili uwashe vipengele vya Super Chat na Super Stickers:

  1. Kwenye kompyuta, ingia katika akaunti kwenye Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, bofya Chuma mapato.
  3. Bofya kichupo cha Supers . Kichupo hiki kitaonekana tu iwapo kituo chako kimetimiza masharti.
  4. Bofya Anza kisha ufuate maagizo yaliyo kwenye skrini.
  5. Iwapo ni mara yako ya kwanza katika sehemu ya Supers, fuata maagizo yaliyo kwenye skrini ili utie sahihi kwenye Sehemu ya Bidhaa za Biashara (CPM).
  6. Baada ya kukamilisha maagizo yote, utapata chaguo 2:
    • “Super Chat” karibu na swichi unayoweza kuwasha na kuzima.
    • “Super Stickers” karibu na swichi unayoweza kuwasha na kuzima.

Iwapo ungependa kutumia kifaa chako cha mkononi kuwasha vipengele vya Super Chat na Super Stickers:

  1. Fungua programu ya Studio ya YouTube ya vifaa vya mkononi .
  2. Katika sehemu ya chini ya skrini, gusa Chuma mapato.
  3.  Gusa kadi ya Supers. Iwapo kadi ya Supers haitaonekana, gusa Anza katika sehemu ya “Supers” kisha Washa.
  4. Iwapo ni mara yako ya kwanza katika sehemu ya Supers, fuata maagizo yaliyo kwenye skrini ili utie sahihi kwenye Sehemu ya Bidhaa za Biashara (CPM).
  5. Ukishakamilisha maagizo yote, bidhaa zote za Supers zitaonyeshwa kwenye ustahiki wako:
    • Mitiririko mubashara na Maonyesho ya Kwanza (Super Chat na Super Stickers)
    • Video ndefu na Video Fupi (Shukrani Moto)

Madokezo:

  • Iwapo mshirika mwingine anasimamia haki zako, wasiliana naye kwanza kabla ya kuwasha Super Chat au Super Stickers.
  • Ikiwa ungependa kuzima vipengele fulani vya Supers, unaweza kutumia kompyuta kuingia katika akaunti ya Studio ya YouTube. Nenda kwenye kichupo cha Supers ili uzime Supers husika.

Kuzima Super Chat au Super Stickers

  1. Kwenye kompyuta, ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, bofya Chuma mapato.
  3. Bofya kichupo cha Supers .
  4. Teua chaguo moja au zote mbili kati ya zifuatazo:
    • Zima swichi iliyo karibu na "Super Chat."
    • Zima swichi iliyo karibu na "Super Stickers."
  5. Kwenye dirisha ibukizi, bofya kisanduku cha kuteua kilicho karibu na "Ninaelewa athari za kitendo hiki."
  6. Bofya Zima.

Washa Super Chat au Super Stickers kwenye mtandao wako

Ruhusu mtandao uwashe Super Chat au Super Stickers

Ili uchume mapato kutoka kwenye Super Chat au Super Stickers, ni lazima mitandao ikubali kwanza Sehemu ya Bidhaa za Biashara (CPM). Ili upate maelezo zaidi kuhusu CPM, angalia sera zetu za uchumaji wa mapato katika Bidhaa za Biashara kwenye YouTube.

  1. Kwenye kompyuta, ingia katika akaunti kwenye Studio ya YouTube.
  2. Nenda kwenye Mipangilio.
  3. Bofya "Makubaliano" kisha ukubali Sehemu ya Bidhaa za Biashara.

Kuwasha Super Chat na Super Stickers kwenye Maonyesho ya Kwanza

Super Chat na Super Stickers hufanya kazi kwenye Maonyesho ya Kwanza katika YouTube. Iwapo umewasha Super Chats na Super Stickers kwenye kituo chako, zitawashwa kiotomatiki utakapozindua onyesho la kwanza la video. Fuata maagizo haya ili uzindue onyesho la kwanza la video lenye Super Chat au Super Stickers:

  1. Kwenye kompyuta, ingia katika akaunti ya YouTube yenye kituo ambako umewasha Super Chat au Super Sticker.
  2. Katika sehemu ya juu ya ukurasa, bofya Pakia  , au nenda kwenye youtube.com/upload.
  3. Bofya Imeratibiwa katika menyu kunjuzi.
    • Kumbuka kuwa hatua ya kuchagua "Umma" itasababisha onyesho la kwanza lifunguke pindi baada ya video kumaliza kupakiwa.
    • Video ambazo hazijaorodheshwa haziwezi kuzinduliwa kama onyesho la kwanza.
  4. Bofya video ambayo ungependa kupakia kutoka kwenye kompyuta yako.
  5. Kwenye ukurasa unaofuata, washa Onyesho la Kwanza.
  6. Chagua tarehe na saa za kuzindua onyesho lako la kwanza.
  7. Wakati video imemaliza kuchakatwa, bofya Onyesho la Kwanza katika kona ya juu kulia.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
232511364556231559
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false