Ufafanuzi wa mifumo ya uchumaji wa mapato au ‘algoriti ya matangazo’

YouTube ni mahali pa watu kote ulimwenguni kushiriki hadithi zao. Zaidi ya saa 400 za video hupakiwa kila dakika kwenye YouTube, mamia ya mamilioni ya saa hutazamwa kila siku na mabilioni ya watumiaji hutembelea YouTube kila mwezi.
Ili kuhakikisha kuwa jumuiya yetu ni salama kwa watayarishi, watazamaji na watangazaji, tulibuni mifumo ya kiotomatiki ya kutusaidia kuchuja maudhui yote kwenye YouTube. Wakati mwingine, mifumo hii huitwa “algoriti ya matangazo” au “mifumo.”

Jinsi mifumo yetu inavyoathiri watayarishi wanaochuma mapato

Mifumo yetu huangalia maudhui na chaneli zako kwa njia tofauti na katika hatua tofauti. Kwa watayarishi katika Mpango wa Washirika wa YouTube, mifumo yetu ya uchumaji wa mapato inaweza kuathiri maudhui yako na chaneli yako.

Athari kwenye maudhui

Ukiwasha kipengele cha matangazo kwenye maudhui, mifumo yetu huyakagua kwa njia 2:

  • Maudhui yanayofaa watangazaji. Video yoyote ambapo unachuma mapato kwa kutumia matangazo ni lazima ifuate mwongozo wetu wa maudhui yanayofaa watangazaji. Mifumo yetu hukagua jina la video, kijipicha, maelezo, lebo na video yenyewe ili kuona kama inatimiza masharti ya mwongozo wetu. Unaweza kuona matokeo ya ukaguzi huu kupitia aikoni ya uchumaji wa mapato.
  • Kushiriki kwa watazamaji. Mifumo yetu pia itakagua hali ya kushiriki kwa watazamaji. Hii inamaanisha kuwa tunaangalia vitu kama vile maoni, idadi ya waliopendezwa na iwapo video inatazamwa yote. Pia tunaangalia aina nyingine za maudhui ambayo hadhira yako hutazama. Baada ya hapo mifumo yetu inaweza kufanya tathmini nyingine ya uchumaji wa mapato inayoweza kubadilisha hali ya uchumaji wa mapato ya video yako.

Pata maelezo zaidi kuhusu mabadiliko ya hali ya aikoni ya uchumaji wa mapato na hatua unazoweza kuchukua.

Athari kwenye chaneli

Mifumo yetu pia huangalia kama unafanya maamuzi sahihi mara kwa mara kuhusu uchumaji wa mapato kwenye chaneli yako. Kumbuka, unapaswa tu kuwasha matangazo kwenye video zinazotimiza mwongozo wetu wa maudhui yanayofaa watangazaji. Ukiwasha matangazo mara kwa mara kwenye video zinazokiuka mwongozo wetu, mifumo yetu inaweza kuripoti chaneli yako. Katika hali za ukiukaji uliopita kiasi, tunaweza kuondoa uwezo wako wa kuchuma mapato kwa kutumia matangazo au tukuondoe kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube.

Hatua unazoweza kuchukua kuhusu mfumo

Mifumo yetu si sahihi kila wakati. Kwa sababu hiyo, unaweza kutuma ombi la ukaguzi wa hali ya uchumaji wa mapato ya video yako wakati wowote. Unapotuma ombi la ukaguzi, mtaalamu wa sera aliyepewa mafunzo huangalia maudhui yako ili kuona kama yanatimiza masharti ya mwongozo wetu. Mkaguzi wetu asipokubaliana na mfumo wetu wa kiotomatiki, tutachukulia uamuzi wa mkaguzi kama wa mwisho.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
7647046869627018719
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false