Maswali Yanayoulizwa Sana Kuhusu Maonyo

Nini kitafanyika iwapo nitapata onyo?

Ukipokea onyo la Hakimiliki au onyo kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya, tutakufahamisha kupitia barua pepe, kupitia arifa kwenye kifaa cha mkononi na kompyuta ya mezani na katika chaneli yako ya YouTube. Tutakufahamisha kwa nini ulipokea onyo na hatua utakayochukua baadaye kulihusu.

Kwa nini tuna mifumo 2 tofauti?

Tuna mifumo 2 kwa sababu tunaona maonyo kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya na maonyo ya Hakimiliki kama masuala tofauti.

Ukiukaji wa hakimiliki na wa Mwongozo wa Jumuiya hufanyika kwa sababu tofauti. Mwongozo wa Jumuiya yetu ni kanuni ambazo tungependa watayarishi na watazamaji wafuate ili kufanya Jumuiya ya YouTube iwe salama. Kanuni za hakimiliki zimewekwa ili kuhakikisha kuwa haki za watayarishi zinalindwa na kuwa kila mtu anafuata sheria wakati anatumia maudhui katika video, mitiririko mubashara na hadithi zao.

Huenda unafahamu vikwazo vya hakimiliki, lakini hufahamu sera yetu kuhusu maudhui ya ngono na uchi. Au, huenda unafahamu sera zetu kuhusu vijipicha, lakini hufahamu kuwa kutumia wimbo wa mtu mwingine katika video yako kunaweza kusababisha onyo la hakimiliki. Tungependa kukupa fursa ya kupata maelezo kuhusu sera zetu zote.

Iwapo ungependa kupata maelezo zaidi kuhusu aina za matukio yanayochukuliwa kuwa ukiukaji wa hakimiliki, unaweza kusoma:

Iwapo ungependa kupata maelezo zaidi kuhusu Mwongozo wa Jumuiya yetu, unaweza kutazama video hii au kukagua sera mahususi katika Kituo cha Usaidizi.

Kwa nini matokeo ya kila aina ya onyo ni tofauti?

Tumeweka adhabu za maonyo ya hakimiliki na maonyo kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya kwa njia ambayo huwasaidia watumiaji wajifunze zaidi kutokana na hali zao na waendelee kufurahia YouTube. Kuhusu maonyo kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya, tulibaini kuwa mara nyingi watumiaji wanaweza kuelewa kwa haraka ni kwa nini maudhui yao yalikiuka kanuni baada ya kupata tahadhari na kutembelea ukurasa wa sera husika.

Iwapo ni onyo lako la kwanza, utahitaji kukamilisha Mafunzo ya Hakimiliki.

Ni kwa nini huwa hupokei tahadhari kila wakati?

Iwe unapokea au hupokei tahadhari, hutegemeana na mambo machache, kama vile iwapo ulikiuka Mwongozo wa Jumuiya au Hakimiliki au ni mara yako ya kwanza kukiuka.

Tunafahamu kuwa makosa hufanyika. Ndiyo maana mara ya kwanza maudhui yako yasipofuata mojawapo ya Mwongozo wetu wa Jumuiya, tutakupa tahadhari. Ili muda wa tahadhari kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya uishe baada ya siku 90, unaweza kushiriki katika mafunzo ya sera. Tunatumai kuwa hatua hii itakupa fursa ya kupata maelezo kuhusu sera zetu na kuepuka ukiukaji tena. Ukiuka sera tofauti baada ya kukamilisha mafunzo, utapewa tahadhari nyingine. Huenda tukazuia watu wanaorudia kufanya makosa wasishiriki katika mafunzo siku zijazo.

Hata hivyo, tukipokea ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki, tutaondoa video na tutatoa Onyo la hakimiliki hata kama ni mara yako ya kwanza. Tunafanya hivyo ili kutii sheria. Ili tuondoe video, lazima mwenye hakimiliki atume ombi kamili na halali la kisheria.

Kumbuka: Madai ya Content ID hayasababishi kupokea onyo.

Nitajuaje aina ya onyo niliyopokea?

Tunapokufahamisha kuhusu onyo, tutakujulisha aina ya onyo ambalo umepokea. Iwapo ni onyo kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya, tutakufahamisha pia sera ambayo maudhui yako yalikiuka.

Maonyo kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya na ya Hakimiliki yataonekana kwenye dashibodi yako ya Studio au kwenye kichupo cha Maudhui.

Ninaweza kuchukua hatua gani iwapo nitapata onyo?

Tunafahamu kuwa makosa hufanyika na watu hawakiuki sera zetu au kukiuka hakimiliki ya mtu mwingine kimakusudi. Tunafahamu kuwa kupokea onyo kunaweza kutisha, lakini kuna hatua unazoweza kuchukua ili kuepuka athari mbaya zinazodumu kwenye chaneli yako.

Ukipata onyo kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya, tunapendekeza ufanye yafuatayo:

  1. Pata maelezo kuhusu Mwongozo wa Jumuiya yetu ili uhakikishe kuwa maudhui yako yanafuata sera zetu.
  2. Baada ya kukagua sera zetu, wasiliana nasi iwapo unafikiri kuwa tumekosea. Unaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo hapa.

Ukipata Onyo la hakimiliki, una chaguo zifuatazo:

  • Kusubiri muda wake uishe: Muda wa maonyo ya hakimiliki huisha baada ya siku 90. Iwapo ni onyo lako la kwanza, utahitaji kukamilisha Mafunzo ya Hakimiliki.
  • Kuomba dai lifutwe: Unaweza kuwasiliana na mtu aliyedai video yako na umwombe afute dai lake la ukiukaji wa hakimiliki.
  • Kutuma arifa ya kukanusha: Iwapo video yako iliondolewa kimakosa kwa sababu ilitambuliwa kimakosa kuwa imekiuka au imetimiza masharti ya uwezekano wa matumizi ya haki, huenda ungependa kutuma arifa ya kukanusha.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
10290460235496725414
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false