Kutayarisha mtiririko mubashara kwenye kifaa cha mkononi

Ili utiririshe mubashara kwenye kifaa cha mkononi, unapaswa:

Ikiwa una watu wanaofuatilia zaidi ya 50 na wasiozidi 1,000

Ili kuisaidia kufanya YouTube iwe jumuiya salama kwa kila mtu, huenda tukaweka kikomo cha idadi ya watazamaji katika mtiririko mubashara kwenye kifaa chako cha mkononi. Pia, mtiririko mubashara uliohifadhi kwenye kumbukumbu utawekwa katika hali ya faragha kwa chaguomsingi. Inaweza kuchukua wiki chache ili mabadiliko haya yaonekane kutokana na uchakataji.

Kwa nini hadhira ya mtiririko wangu mubashara kwenye vifaa vya mikononi imewekewa kikomo?

Ili kuwasaidia watayarishi chipukizi huku tukilinda jumuiya, tumeweka ulinzi ili punguza kusambaa kwa maudhui yanayoweza kuwa hatari.

Ni nini kitafanyika nikifikisha wafuatiliaji 1,000?

Baada ya kufikisha wafuatiliaji 1,000, inaweza kuchukua wiki kadhaa ili kuondoa kikomo cha hadhira ya mtiririko mubashara kwenye kifaa cha mkononi. Ikiwa idadi ya wafuatiliaji itapungua katika muda huu, basi inaweza kuchukua muda hata zaidi.

Idadi ya wanaofuatilia kituo chako ikiwa chini ya 1,000, utawekewa kikomo cha hadhira sawa na ilivyokuwa kituo chako kilipokuwa na chini ya wafuatiliaji 1,000. Hutapoteza idhini ya kufikia mtiririko mubashara kwenye kifaa cha mkononi isipokuwa idadi ya wanaofuatilia kituo chako iwe chini ya wafuatiliaji 50.

Kutayarisha na kuratibu mtiririko mubashara kwenye kifaa cha mkononi

  1. Fungua programu ya YouTube kwenye simu au kompyuta kibao yako.
  2. Katika sehemu ya chini, gusa Tayarisha kisha Tiririsha mubashara.
    • Kwa mtiririko wako mubashara wa kwanza kwenye kifaa cha mkononi: Shughuli ya kuanzisha mtiririko wako wa kwanza mubashara inaweza kuchukua hadi saa 24. Baada ya kuruhusiwa, unaweza kutiririsha mubashara papo hapo.
  3. Fuata hatua ili uanzishe mtiririko mubashara.
    • Kwa watumiaji wa YouTube walio na umri wa miaka 13 hadi 17, mipangilio chaguomsingi ya faragha ya mtiririko mubashara kwenye kifaa cha mkononi huwekwa katika hali ya haijaorodheshwa. Ikiwa una umri wa miaka 18 au zaidi, mipangilio chaguomsingi ya faragha ya mtiririko mubashara kwenye kifaa cha mkononi huwekwa katika hali ya umma. Unaweza kubadilisha mipangilio hii ili ufanye mtiririko wao mubashara uwe wa umma, wa faragha au ambao haujaorodheshwa.
    • Ili uratibu kwa ajili ya baadaye, gusa Chaguo zaidi.
    • Ili uweke chaguo za gumzo la moja kwa moja, mipaka ya umri, uchumaji wa mapato na zaidi, gusa Chaguo zaidi kisha Onyesha zaidi. Kisha uguse Endelea.
    • Ili utiririshe skrini ya simu yako, gusa Fungua kituo kisha Shiriki skrini .
  4. Gusa Tiririsha mubashara.
  5. Ili ukamilishe mtiririko wako, gusa Kamilisha. Kumbukumbu ya mtiririko wako itabuniwa kwenye kituo chako. Unaweza kubadilisha mipangilio ya faragha au kufuta kumbukumbu wakati wowote.

Kuanzisha mtiririko mubashara ulioratibiwa kwenye kifaa cha mkononi

  1. Fungua programu ya YouTube kwenye simu au kompyuta kibao yako.
  2. Gusa Tayarisha  kisha Tiririsha mubashara.
  3. Gusa Kalenda kisha Chagua mtiririko wako mubashara.
    Kumbuka: Unaweza kufuta mitiririko mubashara iliyoratibiwa kwa kubonyeza kitufe cha kufuta.
  4. Gusa Tiririsha mubashara.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
4428479360701657150
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false