Tembelea kichupo chako cha Wasifu ili uone kila kitu ulichotazama, kupakua au kununua kwenye YouTube. Unaweza pia kupata mipangilio inayohusiana na akaunti na maelezo ya kituo kwenye ukurasa huu.
Explore the You tab on your mobile device
Ili upate kichupo cha Wasifu, nenda kwenye mwongozo kisha ubofye Wasifu. Kwenye sehemu hiyo, unaweza:
Kubadilisha akaunti
Ili ubadilishe akaunti unayotumia, bofya Badilisha akaunti. Unaweza kupata chaguo hili kwenye sehemu ya jina la kituo chako. Pia, utapata chaguo hili unapobofya picha yako ya wasifu kwenye sehemu ya juu kulia ya ukurasa.
Akaunti ya Google
Ili uende kwenye Akaunti yako ya Google, bofya Akaunti ya Google. Unaweza kupata chaguo hili kwenye sehemu ya jina la kituo chako. Pia, utapata chaguo hili unapobofya picha yako ya wasifu kwenye sehemu ya juu kulia ya ukurasa.
Historia
Video ambazo umetazama hivi majuzi zinapatikana kwenye sehemu ya Historia. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kudhibiti historia ya video ulizotazama.
Vituo vya Primetime
Tazama Vituo vya Primetime ulivyonunua.
Tazama baadaye
Video ulizohifadhi kwenye orodha yako ya kucheza ya Tazama baadaye zinaweza kupatikana hapa.
Orodha za kucheza
Orodha za kucheza ulizounda, ikijumuisha orodha za kucheza za umma, za faragha na ambazo hazijaorodheshwa, zinaweza kupatikana kwenye Orodha za kucheza. Video zisizozidi 5,000 zinaweza kuonyeshwa kwenye orodha ya kucheza. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kudhibiti orodha zako za kucheza.
Video ulizopenda
Video ulizopenda hapo awali zinaweza kupatikana kwenye sehemu ya Video ulizopenda.
Video zako
Video ulizopakia awali zinaweza kupatikana kwenye sehemu ya Video zako.
Beji
Angalia beji ambazo umepata. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kupata na kudhibiti beji.
Klipu zako
Unapotengeneza klipu ya sehemu za video ili uzihifadhi kwa ajili ya kutazama baadaye au kushiriki na wengine, klipu hizo huhifadhiwa hapa. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kushiriki klipu.