Kugundua kichupo cha Wasifu

Tembelea kichupo chako cha Wasifu ili uone kila kitu ulichotazama, kupakua au kununua kwenye YouTube. Unaweza pia kupata mipangilio inayohusiana na akaunti na maelezo ya kituo kwenye ukurasa huu.

Explore the You tab on your mobile device

Ili upate kichupo cha Wasifu, gusa picha yako ya wasifu . Kwenye ukurasa huu unaweza:

 Kubadilisha akaunti

Ili ubadilishe akaunti unayotumia, gusa Badilisha akaunti. Unaweza kupata chaguo hili kwenye sehemu ya jina la kituo chako. Utapata pia chaguo hili unapogusa mipangilio kwenye sehemu ya juu kulia ya ukurasa.

 Akaunti ya Google

Ili uende kwenye Akaunti yako ya Google, gusa Akaunti ya Google. Unaweza kupata chaguo hili kwenye sehemu ya jina la kituo chako. Utapata pia chaguo hili unapogusa mipangilio kwenye sehemu ya juu kulia ya ukurasa.

 Kuwasha Kipengele cha Hali Fiche

Ili uvinjari YouTube kwa faragha, gusa Washa Kipengele cha Hali Fiche. Unaweza kupata chaguo hili kwenye sehemu ya jina la kituo chako.

Historia

Video ambazo umetazama hivi majuzi zinapatikana kwenye sehemu ya Historia. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kudhibiti historia ya video ulizotazama.

  Orodha za kucheza

Unaweza kupata orodha ya kucheza ya Tazama baadaye na orodha za kucheza ulizounda, ikijumuisha orodha za kucheza za umma, za faragha na ambazo hazijaorodheshwa, kwenye sehemu ya Orodha za kucheza. Video zisizozidi 5,000 zinaweza kuonyeshwa kwenye orodha ya kucheza. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kudhibiti orodha zako za kucheza.

 Vipakuliwa

Video ulizopakua ili uzitazame baadaye zinaweza kupatikana kwenye sehemu ya Vipakuliwa.

Video zako

Video ulizopakia awali zinaweza kupatikana kwenye sehemu ya Video zako.

Filamu na vipindi vyako vya televisheni

Video ulizonunua zinaweza kupatikana kwenye sehemu ya Filamu na vipindi vyako vya televisheni. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kununua filamu na vipindi.

 Beji

Angalia beji ambazo umepata. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kupata na kudhibiti beji.

 Klipu zako

Unapotengeneza klipu ya sehemu za video ili uzihifadhi kwa ajili ya kutazama baadaye au kushiriki na wengine, klipu hizo huhifadhiwa hapa. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kushiriki klipu.

 Kikapu

Angalia bidhaa ulizoweka kwenye kikapu chako.

 Orodha ya matamanio ya ununuzi

Ikiwa umehifadhi bidhaa kwenye orodha yako ya matamanio, unaweza kuzipata hapa.

 Manufaa yako ya Premium

Iwapo wewe ni Mwanachama wa Premium, unaweza kuangalia manufaa yanayopatikana kwako kupitia uanachama wako. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuweka mipangilio ya Uanachama wa Premium.

 Usaidizi na maoni

Gusa Usaidizi na maoni ili upate nyenzo katika Kituo chetu cha Usaidizi au ututumie maoni.

 Mipangilio

Gusa Mipangilio  katika kona ya juu kulia ya skrini yako ili uone chaguo za ziada za mipangilio, ikiwa ni pamoja na mipangilio ya ufikivu, faragha na kushiriki.

Kumbuka: Huenda usione sehemu hizi zote. Kwa mfano, ikiwa hujaweka vipengee vyovyote kwenye kikapu chako, sehemu ya Kikapu haitaonekana.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
12508824787956526430
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false