Mwongozo wa aikoni ya uchumaji wa mapato kwa Studio ya YouTube

Mpango wa ugavi wa mapato ya matangazo katika Video Fupi ulianza tarehe 1 Februari, 2023. Ikiwa kuna aikoni za kijivu karibu na Video zako Fupi baada ya tarehe hiyo, inamaanisha kuwa hujakubali sehemu hiyo katika Studio ya YouTube.

Tumia makala haya ili upate maelezo kuhusu jinsi ya kuangalia hali ya uchumaji wa mapato ya video yako na uelewe maana ya kila aikoni ya uchumaji wa mapato. Unaweza pia kupata maelezo kuhusu maana ya aikoni ya uchumaji wa mapato iliyo karibu na video yako inapobadilika.

Kumbuka: Uwezo wako wa kuchuma mapato kwenye video unategemea vigezo kadhaa, ikijumuisha madai ya hakimiliki, ugavi wa mapato na ufaafu wa video kwa watangazaji. Ili upate maelezo zaidi, jifunze jinsi ya kupakia video ili kuchuma mapato kupitia matangazo.

Kuangalia hali ya uchumaji wa mapato ya video

Ili uangalie hali ya uchumaji wa mapato ya video yako:

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Katika menyu ya kushoto, chagua Maudhui .
  3. Katika safu wima ya Uchumaji wa mapato, unaweza kupata aikoni za uchumaji wa mapato. Ili upate maelezo kuhusu maana ya kila aikoni, unaweza kuwekelea kiashiria juu yake.

Ili uchuje orodha ya video zako kulingana na hali ya uchumaji wa mapato:

  1. Bofya upau wa kichujio kisha Uchumaji wa mapato.
  2. Ili uonyeshe video zenye aikoni za kijani, chagua Zinazochuma mapato. Ili uonyeshe video zenye aikoni za kijivu na nyekundu, chagua Zisizochuma mapato. Ili uonyeshe video zenye aikoni za njano, chagua Chache.
  3. Bofya TUMIA.

Mwongozo wa aikoni ya uchumaji wa mapato

Tumia jedwali hili kujifunza maana ya kila aikoni ya uchumaji wa mapato.

Aikoni na maelezo

Wakati aikoni inaonyesha

Maana ya aikoni kwa hali ya uchumaji wa mapato ya video yako Vidokezo kuhusu hali hii ya uchumaji wa mapato
 Inakagua Aikoni hii huonyeshwa karibu na video wakati mifumo yetu inakagua video ili kubaini ufaafu kwa matangazo. Wakati ukaguzi wa kubaini ufaafu kwa matangazo unaendelea, hatuonyeshi matangazo kwenye video yako.

Mifumo yetu hukagua video kubaini ufaafu kwa matangazo wakati wa mchakato wa upakiaji. Ukaguzi huu kwa kawaida huchukua chini ya dakika 20 na hauzidi saa 1.

Ukaguzi ukikamilika, rangi ya aikoni hubadilika na kuwa kijani, njano au nyekundu.

Ili uboreshe uwezo wa kuchuma mapato, tunapendekeza usubiri ukaguzi ukamilike kabla ya kuchapisha video yako hadharani.

 Yamewashwa Aikoni hii huonyeshwa karibu na video wakati imetimiza masharti yetu kwa mujibu wa mwongozo wa maudhui yanayofaa watangazaji. Video imetimiza masharti ya kuonyesha matangazo zaidi. Kumbuka kuwa huenda usipokee mapato yote ya matangazo kwenye video hii. Wakati mwingine, mapato yako yanaweza kuzuiwa kwa muda kwa sababu ya mzozo wa hakimiliki au chanzo cha hadhira kisicho sahihi.
 Hali zisizofuata kanuni Aikoni hii huonyeshwa karibu na video yako wakati hadhira yake imebainishwa kuwa inalenga watoto. Video hii imetimiza masharti ya matangazo ambayo hayawekewi mapendeleo pekee. -
 Yanagawanywa Aikoni hii huonyeshwa wakati umepakia video ya toleo lingine la wimbo (ulioimbwa na mtu mwingine) na mchapishaji wa muziki anaudai. Hapo awali mchapishaji huyu wa muziki alikubali kugawana mapato na watayarishi walio kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube wanaotayarisha matoleo mengine ya wimbo. Video hiyo inagawana mapato na mwenye hakimiliki za muziki. Unapata sehemu tu ya mapato, lakini si mapato yote kwa video hii. Pata maelezo zaidi kuhusu ugavi wa mapato pamoja na uchumaji wa mapato ya matoleo mengine ya nyimbo za video zinazostahiki.
 Yameshikiliwa Aikoni hii huonyeshwa karibu na video mapato yanaposhikiliwa kivyake mchakato wa kupinga dai la Content ID unapoendelea. Baada ya mzozo wa Content ID kutatuliwa, huwa tunalipa mapato hayo kwa mhusika anayefaa. Ikiwa maelezo ya hali yanasema “Madai ya hakimiliki”: Hii inamaanisha tulibaini kuwa video ina maudhui yenye hakimiliki na mwenye hakimiliki anakagua rufaa au mzozo wako. Pata maelezo zaidi kuhusu uchumaji wa mapato wakati wa mizozo ya Content ID.
 Yamedhibitiwa Aikoni hii huonyeshwa karibu na video wakati video haijatimiza masharti yote kwa mujibu wa mwongozo wetu wa maudhui yanayofaa watangazaji. Chapa zinaweza kuchagua kujiondoa kwenye maudhui ambayo hayajatimiza masharti kwa mujibu wa mwongozo wetu wa maudhui yanayofaa watangazaji. Kwa hivyo, video inaweza kuchuma mapato machache ikilinganishwa na maudhui yanayofaa watangazaji.

Ikiwa maelezo ya hali yanasema “Ufaafu kwa matangazo”: Maelezo haya yanamaanisha kuwa mifumo yetu ya kiotomatiki ilitathmini video hii. Unaweza kuomba ukaguzi, kumaanisha kuwa mtaalamu wa sera atakagua video tena na iwapo itafaa, anaweza kubadilisha hali ya uchumaji wa mapato ya video.

Ikiwa maelezo ya hali yanasema “Ufaafu kwa matangazo - Inakaguliwa”: Maelezo haya yanamaanisha kuwa mtaalamu wa sera anakagua video. Mtaalamu anaweza kudumisha au kubadilisha hali ya uchumaji wa mapato na uamuzi wake ni wa mwisho.

Ikiwa maelezo ya hali yanasema “Ufaafu kwa matangazo - Imethibitishwa kupitia ukaguzi”: Maelezo haya yanamaanisha kuwa wataalamu wetu wa sera walikagua video na wanaamini kuwa haitimizi masharti ya mwongozo wetu wa maudhui yanayofaa watangazaji. Hali ya aikoni ya njano haiwezi kubadilishwa.

Kumbuka: Ikiwa video ina chanzo cha hadhira kisicho sahihi, haitasababisha aikoni ya njano. Aikoni za njano zinatumika tu kwenye video kulingana na mwongozo wetu wa maudhui yanayofaa watangazaji.

 Haistahiki Mara nyingi, aikoni hii huonyeshwa karibu na video wakati kuna madai ya hakimiliki kwenye video. Video haiwezi kuwekewa mipangilio ya kuchuma mapato. Ikiwa maelezo ya hali yanasema “Hakimiliki”: Maelezo haya yanamaanisha kuwa mwenye haki amedai video yako kwa kutumia Content ID au amewasilisha ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki ambalo ni kamili na halali. Hali hii hutokea wakati video yako imetumia kazi inayolindwa kwa hakimiliki bila kupata idhini. Kwa hivyo, huchumi tena mapato ya video hiyo.
 Yamezimwa Kwa matangazo ya Ukurasa wa Kutazama, aikoni hii inamaanisha umechagua kutowasha kipengele cha uchumaji wa mapato ya video. Ukipata aikoni hii kwenye Video zako Fupi, inaamanisha kwamba hujakubali Sehemu ya Uchumaji Mapato katika Video Fupi katika Studio ya YouTube. Video hii haijawasha mipangilio ya kuchuma mapato. Ikiwa maelezo ya hali yanasema “Hakimiliki”: Hii inamaanisha kuwa mtu mwingine ana hakimiliki ya maudhui yaliyo kwenye video yako. Matangazo yanaonyeshwa na mapato yanatumwa kwa mwenye hakimiliki. Habari njema ni kwamba mwenye hakimiliki anaweza kuchagua kugawana mapato nawe. Ikiwa utabadilisha hali ya uchumaji wa mapato iwe “imewashwa,” utapata sehemu ya mapato kwa video hii.

Sababu inayoweza kufanya aikoni ya uchumaji wa mapato ibadilike rangi kutoka ya kijani kuwa njano

Wakati mwingine aikoni ya uchumaji wa mapato kwenye video hubadilika kutoka rangi ya kijani  hadi ya njano . Badiliko hili kwenye hali ya uchumaji wa mapato hutokea kwa sababu mifumo yetu huendelea kuchanganua video yako ili kubaini iwapo video imetimiza masharti kwa mujibu wa mwongozo wetu wa maudhui yanayofaa watangazaji. Tunaendelea kujitahidi ili kufanya mchakato huu uwe wa haraka na thabiti zaidi.

Unachoweza kufanya kuhusu mabadiliko ya aikoni

Kabla ya kuchapisha video yako

Katika mchakato wa kupakia, tunapendekeza kuwa usubiri na usichapishe video yako baada ya mchakato wa ukaguzi kukamilika.

Baada ya kuchapisha video yako

Baada ya kupakia video yako, hali ya uchumaji wa mapato ya video yako inaweza kubadilika katika muda wa saa 24 hadi 48 zijazo. Kwa kawaida huwa thabiti baada ya saa 48. Kumbuka kuwa inaweza kubadilika tena kulingana na jinsi watazamaji wanavyoshiriki kwenye video yako.

Ikiwa unafikiri kuwa aikoni ya njano iliyo kwenye video yako imewekwa kimakosa, unaweza kuomba ukaguzi ufanywe na binadamu. Baada ya mtaalamu wa sera kukagua video na kutoa uamuzi wa mwisho, aikoni ya uchumaji wa mapato haipaswi kubadilika.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
13553575426944439026
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false