Arifa

Our teams are currently experiencing high support volumes. Please expect longer than usual wait times for responses to questions from email, chat, and @TeamYouTube on Twitter

Pata maelezo zaidi kuhusu maombi yaliyoratibiwa ya kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki

Mwenye hakimiliki akipata maudhui yake yanayolindwa kwa hakimiliki kwenye YouTube bila idhini yake, anaweza kutuma ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki

Kama sehemu ya mchakato huu, anaweza kuteua chaguo la kuratibu kuondolewa kwa maudhui yanayolindwa kwa hakimiliki. Hii inamaanisha, baada ya YouTube kuthibitisha ombi la kuondolewa, aliyepakia anapewa siku 7 kuchukua hatua kabla ya chaneli yake kupewa onyo la hakimiliki. Katika kipindi hiki cha siku 7, aliyepakia anaweza kuchukua hatua mbalimbali zifuatazo:

  • Kufuta video: Aliyepakia video akiiondoa kwenye YouTube kabla ya muda wa siku 7 kuisha, chaneli yake haitapokea onyo la hakimiliki.
    • Baada ya kipindi cha siku 7 kukamilika, hatua ya kuondoa video haitatatua onyo la hakimiliki. 
  • Wasiliana na mlalamikaji: Wapakiaji wanaweza kuwasiliana na mtu aliyewasilisha ombi la kuondoa video (mlalamikaji) na kumwomba afute ombi lake la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki.
  • Kughairi rufaa: Ikiwa ombi lililoratibiwa la kuondoa video lilitokana na aliyepakia kukata rufaa kufuatia dai la Content ID, aliyepakia anaweza kughairi rufaa yake ndani ya kipindi hicho cha siku 7.
  • Usifanye lolote: Waliopakia wanaweza kusubiri ombi la kuondoa litekelezwe baada ya kipindi cha siku 7 kukamilika. Hapo, maudhui yataondolewa kwenye YouTube na onyo la hakimiliki litatolewa kwa chaneli ya aliyepakia. Kisha, aliyepakia anaweza kuchagua kama na namna anavyotaka kutatua onyo la hakimiki.
    • Maudhui yanaweza kuathiriwa na zaidi ya dai moja la Content ID au ombi la kuondoa, lakini yanaweza kupata tu onyo moja la hakimiliki kwa wakati mmoja.

Hapo, ikiwa aliyepakia anaamini kuwa video yake iliondolewa kimakosa, anaweza kuwasilisha arifa ya kukanusha. Pata maelezo zaidi kuhusu mchakato wa ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
5408406373128425675
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false