Kununua bidhaa kwenye YouTube

 

Unaweza kuvinjari na kununua bidhaa zinazoangaziwa katika maudhui kutoka kwa watayarishi unaowapenda au kununua bidhaa zinazohusiana na mambo yanayokuvutia.

Unakoweza kupata bidhaa kwenye YouTube

Bidhaa kwenye maelezo

Unaweza kuvinjari bidhaa moja kwa moja katika maelezo ya video huku ukitazama maudhui. Katika maelezo ya video, unaweza kupata orodha ya  vipengee vya mauzo na bei. Ukichagua kipengee, utaelekezwa kwingine kwenye duka rasmi la muuzaji wa rejareja. YouTube haiwajibikii shughuli au ununuzi unaofanywa kupitia wauzaji wengine wa rejareja.
 

Kumbuka: Huenda utatozwa katika sarafu ya kigeni na huenda kiasi utakacholipa kikabadilika kulingana na viwango vya ubadilishaji wa sarafu za kigeni na ada za benki. Kagua bei ya bidhaa kwenye tovuti ya muuzaji wa rejareja kabla ya kununua. 

Kwa chaguomsingi, mpangilio wa bidhaa unaoonyeshwa huwekwa kiotomatiki kulingana na vigezo mbalimbali, kama vile bei, umaarufu na upatikanaji. Watayarishi wanaweza pia kuchagua wenyewe vipengee mahususi vya kuonyeshwa katika maelezo ya video kwenye kituo au video yao nzima.

Rafu ya bidhaa

Katika sehemu ya chini au karibu na video na mitiririko mubashara inayotimiza masharti, utaona rafu ya bidhaa itakayokusaidia ukague vipengee ambavyo mtayarishi anaangazia katika video yake. Katika rafu ya bidhaa, unaweza kupata bidhaa za kuuzwa na bei zake. Ukichagua kipengee, unaweza kupata onyesho la kukagua kipengee hicho moja kwa moja kwenye YouTube. Vinginevyo, unaweza kuelekezwa kwenye duka rasmi la muuzaji wa rejareja. 

Kuangalia bidhaa zilizo kwenye video, Video fupi au mtiririko mubashara

Unapotazama maudhui, unaweza kuvinjari bidhaa zinazoangaziwa. Ili ununue au upate maelezo zaidi, bofya kitufe cha ununuzi au uchague Ununuzi shopping bag icon. Orodha ya bidhaa ambazo mtayarishi amewekea lebo kwenye maudhui yake itaonyeshwa, pamoja na viungo unavyoweza kutumia kununua kutoka duka lake. Mtayarishi anaweza pia kubandika bidhaa kwenye mitiririko yake mubashara ili aziangazie zaidi.

  

Vichezaji vya mitiririko mubashara vya kawaida na vilivyo na mipangilio ya kina

Duka la kituo

Kichupo cha duka la kituo huonyesha bidhaa zote zinazouzwa na watayarishi katika maduka yao binafsi. Unaweza kuangalia kichupo cha Duka la mtayarishi kwenye ukurasa wa kwanza wa chaneli yake.

Viungo vya maelezo ya duka

Mtayarishi anaweza kujumuisha kiungo cha URL cha duka lake katika maelezo ya video yake. Chagua URL hiyo ili upate onyesho la kukagua bidhaa moja kwa moja kwenye YouTube, wakati video inacheza. Kisha, unaweza kuchagua tena bidhaa ili uende kwenye duka rasmi la kituo na uinunue.

Kuvinjari na kununua bidhaa kutoka kwa Watayarishi

Iwapo unaishi katika mojawapo ya maeneo haya, unaweza kuwasaidia baadhi ya watayarishi wa YouTube uwapendao kwa kununua bidhaa zao. Watayarishi waliotimiza masharti wanaweza kuonyesha bidhaa zao kwenye YouTube katika:

  • Duka la kituo cha mtayarishi
  • Bidhaa zilizo katika maelezo ya video
  • Rafu ya bidhaa chini au karibu na video au mtiririko mubashara
  • Mitiririko mubashara ambako bidhaa zimebandikwa
  • Maelezo ya video yenye viungo vya maelezo ya duka
  • Kitufe cha ununuzi kwenye video ndefu, Video Fupi au mitiririko mubashara

Watayarishi wanaweza kufanya kazi na mojawapo ya mifumo yetu au wauzaji wa rejareja wanaostahiki kuonyesha bidhaa zao, kama vile bidhaa za chapa rasmi, kwenye YouTube. Ukichagua bidhaa yake moja kwenye YouTube, itafunguka katika kichupo kipya kwenye tovuti ya muuzaji wa rejareja. Unaweza kuvinjari na kununua bidhaa za mtayarishi na bidhaa rasmi kutoka kwa muuzaji huyo wa rejareja. Pata maelezo zaidi kuhusu sera zinazoongoza ununuzi wako.

Kuvinjari na kununua bidhaa zenye lebo katika YouTube

Baadhi ya watayarishi wanaweza pia kuweka lebo kwenye bidhaa kutoka kwenye chapa zingine katika Video Fupi, mitiririko mubashara na video zao za YouTube. Iwapo unaishi katika mojawapo ya maeneo haya, unaweza kuvinjari na kununua bidhaa zilizowekwa lebo. Ununuzi shopping bag icon unaweza kuonekana kwenye ukurasa wa kutazama wa baadhi ya video, Video Fupi na mitiririko mubashara inayoashiria kuwa angalau bidhaa moja imewekewa lebo. Ukichagua Ununuzi shopping bag icon, utaonyeshwa bidhaa zilizowekwa lebo.

Iwapo unatumia kifaa cha mkononi, unaweza kuona rafu ya bidhaa chini ya maudhui katika matokeo ya utafutaji, mipasho ya kutazama au mipasho yako ya ukurasa wa kwanza. Rafu ya bidhaa itaonyesha bidhaa ambazo mtayarishi amewekea lebo kwenye video yake. Ukigusa bidhaa, utaelekezwa kwenye ukurasa wa kutazama, ambako unaweza kuona maelezo kuhusu bidhaa katika kidirisha cha shughuli. Iwapo huvutiwi na bidhaa zinazoonyeshwa, unaweza kuondoa kipengele hiki kwa kugusa Funga .

Unaweza kuchagua bidhaa ili uende kwenye ukurasa wa maelezo ya bidhaa hiyo mahususi au moja kwa moja kwenye tovuti ya muuzaji wa rejareja ili upate maelezo zaidi kuihusu. Kwenye ukurasa wa maelezo ya bidhaa, unaweza pia kupata:

  • Picha za bidhaa
  • Maelezo ya bidhaa
  • Aina za bidhaa kama vile vipimo na rangi tofauti
  • Maelezo ya bei kutoka kwa muuzaji mmoja wa rejareja au zaidi
  • Chaguo za kuhifadhi na kushiriki
  • Ukadiriaji wa bidhaa
  • Bidhaa na video zinazohusiana

Unapochagua bidhaa itafungua tovuti ya muuzaji wa rejareja, itakayokuelekeza kwingine kutoka YouTube. Pata maelezo zaidi kuhusu sera zetu za ununuzi kwenye tovuti za nje za wauzaji wa rejareja.

Kumbuka:  Unapotumia Akaunti ya Biashara, huwezi kufanya ununuzi kwa niaba ya Akaunti ya Biashara. Ununuzi wako unaunganishwa kwenye akaunti yako ya binafsi badala ya Akaunti ya Biashara.

Njia nyingine za kununua bidhaa kwenye YouTube

Unapotazama video, unaweza kutambua sehemu ya bidhaa zinazozalishwa kiotomatiki katika mipasho ya kutazama ambayo inahusiana na unachotazama. Kipengele hiki kinapatikana tu katika programu ya YouTube kwenye vifaa vya Android au iPhone nchini Marekani, India, Brazil, Australia, Kanada, Ufilipino na Malesia.

Unapotafuta bidhaa kwenye YouTube, unaweza kupata chaguo la kuvinjari na kununua bidhaa hiyo. Ukibofya bidhaa hiyo, unaweza kwenda kwenye ukurasa wa maelezo ya bidhaa hiyo na upate maelezo zaidi. Kipengele hiki kinapatikana katika programu ya YouTube kwenye vifaa vya Android au iPhone nchini Marekani, India na Brazil.

Unaweza kutambua sehemu ya bidhaa inayozalishwa kiotomatiki katika mipasho ya ukurasa wa kwanza inayohusiana na video ambazo tayari umetazama. Kipengele hiki kinapatikana katika programu ya YouTube kwenye vifaa vya Android au iPhone nchini Marekani, India au Brazil.

Upatikanaji katika nchi au maeneo

Unaweza kununua bidhaa kutoka kwa watayarishi au chapa zingine wanazoangazia katika maudhui yao. Upatikanaji unatofautiana kulingana na:

  • Iwapo unatazama video, mtiririko mubashara au Video Fupi
  • Nchi au eneo uliko
  • Iwapo bidhaa inatoka kwa Mtayarishi au chapa nyingine

Ikiwa unatazama video, Video Fupi au mtiririko mubashara katika mojawapo ya nchi/maeneo haya, unaweza kununua bidhaa kutoka kwa Watayarishi, kama vile bidhaa za chapa zingine ambazo zinaangaziwa:

  • Aljeria
  • Ajentina
  • Australia
  • Austria
  • Bahareni
  • Bangladeshi
  • Ubelgiji
  • Brazili
  • Kambodia
  • Kanada
  • Chile
  • Kolombia
  • Kostarika
  • Jamhuri ya Zechia
  • Denmaki
  • Jamhuri ya Dominika
  • Ekwado
  • Misri
  • Elsavado
  • Ufini
  • Ufaransa
  • Jojia
  • Ujerumani
  • Ghana
  • Ugiriki
  • Gwatemala
  • Hong Kong
  • Hangaria
  • India
  • Indonesia
  • Jamhuri ya Ayalandi
  • Israeli
  • Italia
  • Japani
  • Yordani
  • Kazakstani
  • Kenya
  • Kuwaiti
  • Lebanoni
  • Malesia
  • Meksiko
  • Moroko
  • Nepali 
  • Uholanzi
  • Nyuzilandi 
  • Nikaragwa
  • Naijeria
  • Norwe
  • Omani
  • Pakistani 
  • Panama
  • Paragwai
  • Peru
  • Ufilipino 
  • Polandi
  • Ureno
  • Pwetoriko
  • Romania
  • Saudia
  • Senegali
  • Singapoo
  • Slovakia
  • Afrika Kusini
  • Korea Kusini
  • Uhispania
  • Srilanka 
  • Uswidi
  • Uswizi
  • Taiwani 
  • Tanzania
  • Tailandi 
  • Tunisia
  • Uturuki
  • Uganda
  • Falme za Kiarabu
  • Uingereza
  • Marekani
  • Urugwai
  • Vietnamu
  • Zimbabwe

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
3035211341995566953
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false