Pata mpango wa wanafunzi wa YouTube Premium

Ikiwa wewe ni mwanafunzi, unaweza kustahiki kupata mpango wa YouTube wa wanafunzi. Pata maelezo kuhusu anayestahiki kupata mpango wa wanafunzi na jinsi ya kujisajili.

Ikiwa una usajili unaotumika kwenye uanachama unaolipiwa wa YouTube (isipokuwa NFL Sunday Ticket kwenye YouTube au YouTube TV) na ungependa kubadilisha ili utumie mpango wa wanafunzi, ghairi kwanza usajili wako unaotumika. Baada ya kughairi uanachama wako unaotumika, unaweza kujisajili kwenye mpango wa YouTube wa wanafunzi.

Ustahiki wa Kujiunga na Mpango wa YouTube wa Wanafunzi

Ili ujisajili kwenye mpango wa YouTube wa wanafunzi, ni lazima:

 • Uwe umesajiliwa kuwa mwanafunzi katika taasisi ya elimu ya juu katika eneo ambapo huduma ya mpango wa YouTube wa wanafunzi inatolewa.
 • Taasisi husika ya elimu ya juu inapaswa kuwa imeidhinishwa na SheerID. Ustahiki wa taasisi hubainishwa na mpango wa SheerID .

  Ili kuhakikisha ikiwa chuo chako kina mipango ya wanafunzi inayopatikana:
  1. Nenda kwenye ukurasa wa kutua wa Mpango wa Wanafunzi wa YouTube Premium au YouTube Music Premium.
  2. Chagua Pata Premium
  3. Andika jina la chuo chako kwenye fomu ya SheerID. Ikiwa chuo chako kipo kwenye orodha, basi ina mipango ya wanafunzi.
 • Thibitishwa kuwa mwanafunzi na SheerID. Kwa usaidizi kuhusu mchakato wa uthibitishaji, tuma barua pepe kwa SheerID kupitia customerservice@sheerid.com.

Ikiwa unatimiza masharti ya kujiunga kuwa mwanachama, utastahiki kupata mpango wa uanachama wa wanafunzi kwa kipindi cha hadi miaka 4 mfululizo. Utatakiwa kuthibitisha upya ustahiki wako kila mwaka.

Maeneo ambapo huduma ya uanachama wa wanafunzi inapatikana

Huduma ya YouTube uanachama wa wanafunzi inapatikana katika maeneo yafuatayo kwa sasa:

 • Aljeria
 • Australia
 • Austria
 • Azabajani
 • Bahareni
 • Bangladeshi
 • Ubelgiji
 • Bolivia
 • Brazili
 • Bulgaria
 • Kambodia
 • Kanada
 • Chile
 • Kolombia
 • Kostarika
 • Kuprosi
 • Jamhuri ya Zechia
 • Denmaki
 • Jamhuri ya Dominika
 • Ekwado
 • Misri
 • Elsavado
 • Ufini
 • Ufaransa
 • Guyana ya Ufaransa
 • Polinesia ya Ufaransa
 • Jojia
 • Ujerumani
 • Ghana
 • Ugiriki
 • Gwatemala
 • Hondurasi
 • Hong Kong
 • Hangaria
 • India
 • Indonesia
 • Iraki
 • Israeli
 • Ayalandi
 • Italia
 • Jamaika
 • Japani
 • Jordani
 • Kazakstani
 • Kenya
 • Kuwaiti
 • Laosi
 • Lebanoni
 • Libya
 • Lasembagi
 • Malesia
 • Malta
 • Meksiko
 • Moroko
 • Nepali
 • Uholanzi
 • Nyuzilandi
 • Nikaragua
 • Masedonia Kaskazini
 • Norwe
 • Omani
 • Pakistani
 • Panama
 • Paragwai
 • Peru
 • Ufilipino
 • Polandi
 • Ureno
 • Katari
 • Riyunioni
 • Romania
 • Urusi
 • Saudia
 • Senegali
 • Singapoo
 • Slovakia
 • Afrika Kusini
 • Uhispania
 • Sirilanka
 • Uswidi
 • Uswizi
 • Taiwani
 • Tanzania
 • Tailandi
 • Tunisia
 • Uturuki
 • Uganda
 • Ukraini
 • Muungano wa Falme za Kiarabu
 • Uingereza
 • Marekani
 • Urugwai
 • Vietinamu
 • Yemeni
 • Zimbabwe

Chaguo za Mpango wa Wanafunzi

Tunatoa chaguo kadhaa za kufurahia zaidi hali yako ya utumiaji wa YouTube. Unaweza kujisajili kwa uanachama wa YouTube Music Premium au YouTube Premium kama mwanafunzi. Utapata manufaa sawa kwa ada iliyopunguzwa. Pata maelezo kuhusu chaguo zetu za uanachama unaolipiwa ili uteue chaguo linalokufaa.

Anza kutumia mpango wa wanafunzi unaolipiwa

YouTube Premium

Ukiwa mwanachama wa YouTube Premium, unaweza kutumia manufaa yako kwenye YouTube, YouTube Music na YouTube Kids.
 1. Kwenye kivinjari cha kompyuta au kifaa chako cha mkononi, nenda kwenye youtube.com/premium/student.
 2. Chagua Pata Premium
 3. Fuata hatua ili ukamilishe uthibitishaji wa SheerID. Ikiwa SheerID inaweza kuthibitisha ustahiki wako, utaelekezwa kwenye YouTube ili uendelee na mchakato wa kujisajili.
  • Ikiwa SheerID inaweza kuthibitisha ustahiki wako, utaelekezwa kwenye YouTube ili uendelee na mchakato wa kujisajili.
  • Ikiwa hutathibitishwa moja kwa moja, utaombwa kupakia hati zaidi ili kuthibitisha ustahiki wako. Hati hizi zitakaguliwa na mtu. Utapokea barua pepe ya kukujulisha kuhusu hali yako ya ustahiki ndani ya kipindi cha dakika 20 nchini Marekani.. Kwa maeneo mengine ya nje ya Marekani, arifa ya barua pepe inaweza kuchukua kipindi cha hadi saa 48 kutumwa.
  • Ikiwa ustahiki wako utathibitishwa kupitia hatua za ziada za uthibitishaji, utahitaji kuingia tena katika akaunti yako. Nenda kwenye wasifu wako kwa kugusa picha yako ya wasifu. Chagua Uanachama unaolipiwa kisha utapokea arifa inayokuomba ukamilishe kujisajili ukitumia hatua zilizo hapa chini.
 4. Chagua njia ya kulipa ambayo ungependa kutumia au weka njia mpya ya kulipa.
 5. Bofya Nunua ili ukamilishe shughuli ya malipo.

Nenda kwenye http://youtube.com/purchases wakati wowote ili uone maelezo kuhusu uanachama wako.

YouTube Music Premium

Kuwa mwanachama wa YouTube Music Premium ili ufurahie mamilioni ya nyimbo na video za muziki bila matangazo. Pakua nyimbo na video uzipendazo ili uzisikilize nje ya mtandao na zaidi.
 1. Kwenye kivinjari cha kompyuta au kifaa chako cha mkononi, nenda kwenye youtube.com/musicpremium/student.
 2. Chagua Pata Premium
 3. Fuata hatua ili ukamilishe uthibitishaji wa SheerID. Ikiwa SheerID inaweza kuthibitisha ustahiki wako, utaelekezwa kwenye YouTube ili uendelee na mchakato wa kujisajili.
  • Ikiwa SheerID inaweza kuthibitisha ustahiki wako, utaelekezwa kwenye YouTube ili uendelee na mchakato wa kujisajili.
  • Ikiwa hutathibitishwa moja kwa moja, utaombwa kupakia hati zaidi ili kuthibitisha ustahiki wako. Hati hizi zitakaguliwa na mtu. Utapokea barua pepe ya kukujulisha kuhusu hali yako ya ustahiki ndani ya kipindi cha dakika 20 nchini Marekani. Kwa maeneo mengine yote ya nje ya Marekani, arifa ya barua pepe inaweza kuchukua kipindi cha hadi saa 48 kutumwa.
  • Ikiwa ustahiki wako utathibitishwa kupitia hatua za ziada za uthibitishaji, utahitaji kuingia tena katika akaunti yako. Nenda kwenye wasifu wako kwa kugusa picha yako ya wasifu. Chagua Uanachama unaolipiwa kisha utapokea arifa inayokuomba ukamilishe kujisajili ukitumia hatua zilizo hapa chini.
 4. Chagua njia ya kulipa ambayo ungependa kutumia au weka njia mpya ya kulipa.
 5. Bofya Nunua ili ukamilishe shughuli ya malipo.

Nenda kwenye http://youtube.com/purchases wakati wowote ili uone maelezo kuhusu uanachama wako.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Kompyuta Android
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Programu za Google
Menyu kuu