Kudhibiti matukio ya kujisajili zaidi ya mara moja

Tuna chaguo kadhaa za uanachama unaolipiwa wa YouTube. Baada ya kusasisha au kubadilisha kutoka chaguo moja la uanachama kwenda chaguo lingine, inaweza kutokea kuwa unalipishwa mara mbili. Pia, baadhi ya mipango yetu ya uanachama unaolipiwa hukuwezesha kupata usajili mwingine kiotomatiki, kwa hivyo unaweza kuokoa pesa kwa kukatisha usajili wa daraja la chini.

Pata maelezo kuhusu jinsi kila uanachama unaolipiwa unavyohusiana na usajili mwingine pia jinsi ya kurekebisha au kuzuia usajili unaolipishwa mara mbili.

Iwapo unatozwa mara mbili na unaamini kuwa utozaji huo hautokani na kuwa na usajili zaidi ya mmoja, tafadhali tembelea ukurasa huu. Huenda ukawa unaona ada ya muda ya kuidhinisha akaunti, malipo ambayo hayajashughulikiwa au aina nyingine ya malipo yasiyotarajiwa.

Chaguo za usajili na malipo

YouTube Premium:

  • Inakupa uwezo wa kufikia manufaa yote ya YouTube Premium pamoja na uwezo wa kufikia manufaa yote ya YouTube Music Premium.
  • Hulipiwa kupitia YouTube au Apple (ikiwa umejisajili kwenye iOS).

YouTube Music Premium:

  • Inakupa uwezo wa kufikia manufaa yote ya YouTube Music Premium.
  • Hulipiwa kupitia YouTube au Apple (ikiwa umejisajili kwenye iOS).

Jinsi ya kurekebisha usajili wa zaidi ya mara moja

Iwapo ulijisajili kwenye YouTube Premium na YouTube Music Premium bila kukusudia: Unaweza kuokoa pesa kwa kukatisha uanachama wako wa YouTube Music kwa sababu umejumuishwa katika uanachama wako wa YouTube Premium. Iwapo ulijisajili kwenye YouTube Music Premium ukitumia Apple, katisha uanachama wako kupitia Apple. Iwapo ulijisajili kupitia YouTube, pata maelezo kuhusu jinsi ya kukatisha uanachama wako.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
6280603652688267625
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false