Kubadilisha ubora wa video yako

Ili kukupa hali bora ya utazamaji, YouTube hubadilisha ubora wa video unayotiririsha kulingana na hali zako za utazamaji. Hali hizi ndizo husababisha uweze kugundua kuwa ubora wa video yako unabadilika unapotazama video.

Vifuatavyo ni baadhi ya vigezo vinavyobainisha ubora wa video:

  1. Kasi ya muunganisho wako wa intaneti.
  2. Ukubwa wa skrini/kicheza video: Video za ubora wa juu kwa kawaida hucheza vizuri sana kwenye skrini kubwa.
  3. Ubora wa video halisi iliyopakiwa: Iwapo video ilirekodiwa katika hali ya ubora wa wastani, haitacheza katika ubora wa juu.
  4. Kivinjari chako: Baadhi ya vivinjari havitumii miundo mipya zaidi ya video au chaguo za ubora.
Kumbuka: Ukiwa na YouTube Premium, unaweza kutazama video katika ubora wa 1080p Premium kwenye simu na kompyuta kibao za Apple. Kuwa mwanachama wa YouTube Premium au pata maelezo zaidi kuhusu manufaa ya YouTube Premium.

Kubadilisha ubora wa video

Unaweza kubadilisha mwenyewe ubora wa video yoyote unayotazama kwenye kompyuta, televisheni, au kifaa cha mkononi.

Jinsi ya kubadilisha ubora wa video unayotazama

Fuatilia chaneli ya Watazamaji ya YouTube ili upate habari, taarifa na vidokezo vipya.

Kubadilisha ubora wa video kwenye televisheni yako:

  1. Kwenye kicheza video, chagua Mipangilio .
  2. Chagua Ubora.
  3. Chagua ubora wa video unaopendelea.
Kumbuka: Baadhi ya miundo ya ubora wa juu (kwa mfano, 1080p, 4K) inaweza isipatikane kwenye vifaa vyote, kwa sababu huenda havitumii teknolojia mpya zaidi ya kubana video (VP9).

Ili ubadilishe ubora wa picha ukiwa unatazama kwenye kompyuta yako:

  1. Kwenye kicheza video, chagua Mipangilio .
  2. Bofya Ubora.
  3. Chagua ubora wa video unaopendelea.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
10544142000262722823
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false