Mambo mapya kwenye Kidhibiti Maudhui cha Studio

Taarifa za hivi karibuni

Januari 2024
  • Utafutaji wa ISNI ya Msanii katika Ukurasa wa Metadata ya Kipengee: Kuweka jina la msanii kwenye ukurasa wa Metadata ya kipengee  katika kiolesura (UI) cha Kidhibiti Maudhui cha Studio huleta orodha ya majina yanayolingana yakiwa na Vitambulishi vyake vya Majina vya Kiwango cha Kimataifa (ISNI) kutoka hifadhidata ya ISNI. Tafadhali kumbuka kuwa hatua hii si ya lazima: kuandika jina la msanii na kubonyeza Enter bado hufungua kisanduku cha dirisha ibukizi ambapo unaweza kuhifadhi jina la msanii bila ISNI yake. Pata maelezo zaidi.

Oktoba 2023 

  • Mabadiliko kwenye Vidhibiti vya Muundo wa Utangazaji kwenye YouTube: Wakati wa upakiaji, Kuwasha matangazo sasa humaanisha matangazo ya kabla ya video kucheza, ya baada ya video kucheza, yanayoweza kurukwa na yasiyorukika yanaweza kuonekana kabla au baada ya video yako ndefu. Pata maelezo zaidi.
Septemba 2023
  • Kutojumuisha sehemu za marejeleo kupitia kiolezo cha Uwasilishaji wa Maudhui: Tunaweka kipengele kipya cha kutojumuisha sehemu za marejeleo kupitia kiolezo cha CSV cha “Marejeleo - Udhibiti” katika Uwasilishaji wa Maudhui ya Kidhibiti Maudhui cha Studio. Washirika sasa wanaweza kuweka, kubadilisha au kuondoa wenyewe sehemu za marejeleo ambazo hawataki zijumuishwe kwenye marejeleo yaliyopo kwa wingi. Pata maelezo zaidi.

Agosti 2023

  • Kichujio Kipya cha Idadi ya Wanaofuatilia katika Ukurasa wa Orodha ya Video Unazodai: Kichujio kipya katika ukurasa wa orodha ya Video Unazodai kwenye Kidhibiti Maudhui cha Studio sasa kinatoa uwezo wa kuchuja video unazodai kulingana na idadi ya wanaofuatilia chaneli.

    Chaguo za vichujio ni chaneli zilizo na idadi ya wanaofuatilia ya Chini ya Elfu 1, kati ya Elfu 1 na Laki 1, Laki 1 na Laki 5, Laki 5 na Milioni 5, Zaidi ya Milioni 5. Pata maelezo zaidi kuhusu kichujio cha idadi ya wanaofuatilia.
Juni 2023
  • Safu wima mpya ya Mmiliki katika uhamishaji wa vipengee: Upakuaji wa vipengee kwenye ukurasa wa Vipengee  sasa unajumuisha safu wima ya "Mmiliki" yenye maelezo ya kina kuhusu mmiliki wa kipengee. Pata maelezo zaidi kuhusu uhamishaji wa vipengee.

Aprili 2023

  • Kichujio kipya: Vipengee vilivyounganishwa: Kuna kichujio kipya cha "Vipengee vilivyounganishwa" kwenye ukurasa wa Vipengee  kinachokuwezesha kuangalia vipengee vilivyounganishwa au visivyounganishwa. Pata maelezo zaidi kuhusu kutumia vichujio kutafuta vipengee.
  • Sasa ripoti za vipengee zinapatikana kila siku: Sasa unaweza kupakua ripoti za vipengee kila siku. Unaweza kupakua ripoti za vipengee kwenye kichupo cha Vipengee katika ukurasa wa Ripoti  . Pata maelezo zaidi kuhusu ripoti zinazoweza kupakuliwa.

Februari 2023

  • Njia mpya za kutumia lebo za kipengee: Vipengele vipya vinapatikana ili kukusaidia utumie lebo za kipengee kwa ufanisi zaidi kwenye Kidhibiti Maudhui cha Studio. Sasa unaweza:
  • Vizuizi vya jukumu jipya huzuia uchezaji unaorejelewa: Unapounda jukumu jipya au kubadilisha jukumu lililopo, sasa unaweza kuchagua kizuizi, "Hakuna uchezaji wa marejeleo." Ikiwa jukumu linajumuisha kizuizi hiki, watumiaji waliokabidhiwa katika jukumu hilo hawataweza kucheza marejeleo ya sauti au video. Pata maelezo zaidi kuhusu kudhibiti majukumu.

Januari 2023

  • Mambo mapya katika kadi ya dashibodi ya Kidhibiti Maudhui cha Studio: Katika ukurasa wako wa Dashibodi,  kuna kadi mpya iitwayo "Mambo mapya katika Kidhibiti Maudhui cha Studio". Kadi hii itaonyesha masasisho ya haraka kuhusu vipengele na utendaji mpya katika Kidhibiti Maudhui cha Studio. Masasisho hayo yataunganisha kwenye makala haya ya Kituo cha Usaidizi kwa maelezo zaidi.

Taarifa za awali

2022

Tunafanya mabadiliko kadhaa ili kuboresha mchakato wa mizozo na ukataji rufaa kuhusu Content ID kwa walalamikaji na waliopakia. Maboresho haya yalitokana na maoni ambayo tumeyasikia kwa miaka mingi kuhusu mchakato huo. Mabadiliko haya yanaweza kuathiri baadhi ya taratibu zako za kazi kwenye Kidhibiti Maudhui cha Studio. Haya ndiyo mabadiliko:

1. Masharti thabiti zaidi ya kujiunga: Ili kupunguza uwezekano wa matumizi mabaya ya mchakato wa kukata rufaa, tunaongeza masharti yanayohitajika ili watumiaji waweze kutuma maombi ya kukata rufaa kuhusu Content ID. Kuanzia sasa, uwezo wa kukata rufaa utadhibitiwa na uwezo wa kufikia kipengele cha kina, kipengele ambacho tumekuwa tukizindua katika miaka michache iliyopita ambacho kinahitaji watumiaji watoe utambulisho au waimarishe historia ya chaneli zao kwa muda ili wapate uwezo wa kufikia.

Kwa sababu inawezekana kuwa hatua hii itasababisha kuwepo kwa rufaa chache na za ubora wa juu, pia tunafupisha muda wa kukagua rufaa zinazohusu Content ID kutoka siku 30 hadi siku 7. Muda wa kukagua rufaa utaisha kama kawaida hatua isipochukuliwa baada ya siku 7. Rufaa isipokaguliwa katika kipindi hicho cha siku 7, bado una uwezo wa kutuma ombi la kuondoa video wakati wowote. Unaweza kupata rufaa unazotakiwa kuzikagua kwenye ukurasa wako wa Matatizo na unaweza kuzipanga kulingana na tarehe ya mwisho ya kukagua rufaa hizo.  

2. Kuripoti ili ukate rufaa: Mabadiliko mengine tunayoanzisha kwa watumiaji walio na uwezo wa kufikia kipengele cha kina ni kipengele cha “Ripoti ili ukate rufaa”. Watumiaji waliotimiza masharti wanaotaka kupinga madai ya kuzuia kwenye video zao watakuwa na chaguo la kuruka hatua ya awali ya kupinga dai na wakate rufaa moja kwa moja. Kumbuka kuwa madai ya kuchuma mapato na kufuatilia hayajatimiza masharti ya kutumia kipengele cha “Ripoti ili ukate rufaa”, madai ya kuzuia pekee ndiyo yanatimiza masharti. 

Pia, kumbuka kuwa chaguo zako za kukata rufaa, k.m. kuondoa dai au kutuma ombi la kuondoa video, hazibadiliki. 

Chaneli unazodhibiti zinapaswa pia kunufaika kutokana na mabadiliko haya kwa kuwa sasa zitakuwa na njia za haraka za utatuzi za kutumia kwenye madai ambayo zinataka kupinga.

Mabadiliko haya yataanza kutekelezwa tarehe 18 Julai, 2022. Mabadiliko yatatumika tu kwenye mizozo na rufaa zitakazotumwa baada ya tarehe hiyo. Ili kukupa muda wa kurekebisha taratibu zako za kazi, mabadiliko haya yatatekelezwa hatua kwa hatua kadiri muda unavyosonga.

 

Maoni

Fuata hatua hizi ili ututumie maoni yako kuhusu vipengele vya Kidhibiti Maudhui cha Studio:

  1. Ingia katika akaunti ya Kidhibiti Maudhui cha Studio.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Tuma maoni .
  3. Weka maoni yako. Kadiri unavyotoa maoni mahususi, ndivyo unavyotusaidia kuelewa zaidi.
    • Kumbuka: Usijumuishe taarifa zozote nyeti (data yoyote inayopaswa kulindwa) kwenye maoni yako. Kwa mfano, usijumuishe manenosiri, namba za kadi za mikopo au taarifa binafsi.
  4. Chagua iwapo ungependa kujumuisha picha ya skrini. Unaweza kuangazia maelezo yoyote kwenye skrini au uondoe taarifa yoyote nyeti inayoonyeshwa.
  5. Ukimaliza kuweka maoni yako, bofya Tuma.

Kumbuka kwamba huwa tunasoma na kuzingatia maoni yote, lakini hatuwezi kujibu maoni yote yanayotumwa.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
6703461146741038260
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false