Habari kwenye YouTube

Hapa YouTube, tunajitahidi kukuunganisha na maudhui kutoka vyanzo vya habari vya kuaminika ili uendelee kupata taarifa kuhusu matukio ya hivi karibuni. Ili kukusaidia uendelee kupata taarifa, tunakuza vyanzo vya habari vya kuaminika katika vipengele vyetu vya habari, kama vile rafu yetu ya Habari Zinazojiri. Hapa chini, unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu jinsi tunavyobainisha vyanzo vya habari vinavyoaminika na jinsi tunavyoangazia maudhui yake kupitia vipengele vyetu vya habari.

Ikiwa unatafuta maelezo kuhusu njia nyinginezo tunazotumia kuangazia vyanzo vya habari vya kuaminika, unaweza kusoma zaidi hapa.

Vyanzo vya Habari vya Kuaminika

Ili kusaidia kubainisha vyanzo vya habari vya kuaminika, vyenye ubora wa juu vya kuonyesha kwenye vipengele vyetu vya habari, mifumo yetu hutumia viashiria mbalimbali vinavyoweza kujumuisha ubora wa kituo na jinsi kituo kilivyoangazia matukio ya habari yanayofaa na ya hivi karibuni. Pia, ni lazima vituo vifuate sera za vipengele vya huduma ya Tafuta na Google na sera za maudhui za Google News

Tunatumia mbinu za mashine kujifunza ili kutoa viashiria mbalimbali vinavyotumiwa kubainisha vyanzo vya habari kwa ajili ya vipengele vyetu vya habari. Data kutoka kwa wakaguzi wengine hufunza, hutathmini na kuboresha viashiria hivi mara kwa mara.

Vipengele vya Habari vya YouTube

Tumebuni vipengele kadhaa vya kukusaidia kupata habari za hivi punde kwenye YouTube. Vipengele hivi hutumia viashiria kutoka Google News kutambua matukio ya habari na habari kuu za siku.  

Maudhui katika vipengele vya habari vya YouTube hutoka kwenye vyanzo vya habari vya kuaminika. Video mahususi zinazoonyeshwa huzalishwa kupitia algoriti maalum kulingana na viashiria kadhaa, ikiwa ni pamoja na, lakini si tu:

  • Ufaafu kulingana na eneo ulipo na lugha
  • Ufaafu kulingana na mada ya habari au tukio
  • Upya wa maudhui
  • Mitiririko mubashara
  • Nia ya kuripoti au video zenye muktadha wa uandishi wa habari 
  • Viashiria vya mapendekezo vya kawaida kwenye YouTube
  • Ushirikiano na tovuti ambazo maudhui yake huonyeshwa katika Google News

Huenda vipengele mahususi vya habari vya YouTube vilivyo hapa chini visipatikane katika nchi au maeneo yote na kwa lugha zote. Tunajitahidi kutoa vipengele hivi katika nchi au maeneo na lugha zaidi.

Rafu ya habari zinazojiri kwenye ukurasa wa kwanza

Kunapokuwa na tukio kubwa la habari, huenda ukaona rafu ya habari zinazojiri kwenye ukurasa wa kwanza wa YouTube. Mifano ya matukio makubwa ya habari inaweza kujumuisha misiba mikubwa au matukio muhimu sana ya kisiasa. Rafu itaonyeshwa kwa watumiaji walioingia katika akaunti ambao wana umri wa miaka 18 na zaidi. Ikiwa huvutiwi na rafu hii, unaweza kuondoa rafu ya habari zinazojiri kwenye ukurasa wa kwanza. 

Rafu ya habari kuu katika huduma ya Tafuta

Ukitafuta habari mahususi kwenye YouTube, huenda ukaona rafu ya habari kuu katika matokeo yako ya utafutaji. Ikiwa ni mojawapo ya habari kuu za siku, rafu ya habari kuu itaonyesha maudhui yanayohusiana na habari husika. Rafu ya Habari Kuu itaonyeshwa bila kujali umri na haiwezi kuondolewa.  

Rafu ya habari kuu kwenye ukurasa wako wa kwanza

Ikiwa mara nyingi unatazama au kutafuta habari kwenye YouTube, rafu ya habari kuu inaweza kuonyeshwa kwenye ukurasa wako wa kwanza. Rafu ya habari kuu inajumuisha maudhui yanayohusiana na habari kuu za siku. Rafu hii itaonyeshwa kwa watumiaji walioingia katika akaunti bila kujali umri.

YouTube.com/news

YouTube.com/news huangazia video na habari kuu za siku. Kwenye youtube.com/news, unaweza pia kuona vipengele fulani vya majaribio. Majaribio haya yanaweza kukuunganisha na maudhui kutoka vyanzo mbalimbali vya habari katika miundo mbalimbali. 

Kidirisha cha maelezo ya habari zinazochipuka katika huduma ya Tafuta

Unapotafuta tukio muhimu la habari zinazojiri, unaweza kuona kidirisha cha maelezo kinachoangazia habari zinazochipuka kutoka vyanzo mbalimbali vya habari. Pia, kidirisha cha maelezo kitaunganisha kwenye tovuti ya habari, ili uweze kufikia kwa urahisi na kusoma makala kamili kuhusu tukio husika. Tovuti hizi za habari lazima ziwe zinahusishwa na kituo cha YouTube ambacho kinatimiza masharti ya kujiunga yaliyoainishwa hapo juu.

Ukurasa wa kutazama habari

Ukurasa wa kutazama habari utaleta pamoja habari kutoka vyanzo mbalimbali vya kuaminika kwenye YouTube, ili kuwasaidia watazamaji kupata maelezo ya kina na kugundua pande tofauti za habari.

Ukurasa wa kutazama utaangazia habari katika miundo mbalimbali ikijumuisha: 

  • Taarifa za Hivi Karibuni, zenye video ya hivi karibuni inayohusu habari husika. 
  • Maelezo na Maoni, yenye muktadha wa ziada kuhusu mada ya habari.
  • Habari Mubashara, zenye mitiririko mubashara inayoonyesha kinachoendelea kwa wakati huo.
  • Video Fupi, ili kupata maelezo ya hivi karibuni ya taarifa ya habari kwa haraka.

Unaweza kufungua ukurasa wa kutazama wa taarifa mahususi ya habari kwa kubofya video iliyo na aikoni ya gazeti kwenye ukurasa wa kwanza wa YouTube, ukurasa wa habari au katika matokeo ya utafutaji.

Kumbuka: Hili ni onyesho la jaribio na limetumika kwa madhumuni ya kutoa mfano pekee.

Kuwasilisha maoni

Ikiwa una maoni au mapendekezo yoyote kuhusu vipengele vya habari kwenye YouTube, unaweza:

  • Kutuma maoni kupitia sehemu ya Zaidi '' katika vidirisha au
  • Kututumia maoni ukitumia Menyu iliyo kwenye picha yako ya wasifu.
     

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
14820976121958939750
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false