Kuangalia Historia yako ya Kuripoti

YouTube hukagua ripoti za watumiaji ili kubaini ikiwa video zinakiuka Mwongozo wa Jumuiya yetu au la. Tembelea ukurasa wako wa Historia ya Kuripoti ili uangalie hali ya video ambazo umeziripoti kwenye YouTube:

  • Mubashara: Video ambazo bado hazijakaguliwa au ambazo tumeamua kwamba hazikiuki Mwongozo wa Jumuiya ya YouTube.
  • Zilizoondolewa: Video ambazo zimeondolewa kwenye YouTube.
  • Zilizozuiwa: Video ambazo zimewekwa katika hali ya kuzuiwa, kama vile mipaka ya umri au Vipengele Vichache.

Baadhi ya video pia zinaweza kuwa na maandishi ya “Maelezo kuhusu video hii hayapatikani”. Hii inaweza kutokea mtayarishi akiondoa video hiyo au video haipatikani kwenye YouTube kwa sababu nyinginezo. Kwa mfano, haipatikani katika nchi uliko.

Video ambazo zimeripotiwa zinaoorodheshwa kulingana na jinsi ulivyoziripoti, kuanzia ya mpya zaidi hadi ya zamani zaidi. Ukiripoti video zaidi ya mara moja, itaonyesha tu ripoti ya hivi punde zaidi.

Katika hali fulani, video uliyoiripoti huenda isiwe kwenye ukurasa wa Historia ya Kuripoti. Hii inaamanisha kwamba watu wengi tayari wameripoti video hiyo na tunaikagua kufuatia ripoti hizo. Tutaboresha kipengele hiki baadaye ili video zote unazoziripoti ziwe kwenye ukurasa huu, hata kama video fulani tayari imeripotiwa.

 

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
3549124209028317895
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false