Muziki ulio katika video hii

Vipengele hivi vinapatikana tu kwa washirika wanaotumia Kidhibiti Maudhui cha Studio ya YouTube.

Unapotazama video iliyo na muziki, huenda kukawa na sehemu katika maelezo ya video inayoitwa “Muziki.” Sehemu hii inaonyesha maelezo kuhusu muziki unaosikika kwenye video, kama vile majina ya wasanii na nyimbo.

YouTube huweka maelezo haya kiotomatiki kwenye baadhi ya video wakati:

Sehemu ya “Muziki” inaweza kuonyesha viungo vya video za muziki au maudhui mengine rasmi ili uweze kugundua nyimbo na wasanii ambao hujawahi kuwasikia.

Maswali Yanayoulizwa Sana

Kwa nini baadhi ya maelezo hayapo katika sehemu ya “Muziki?”

Ikiwa hakuna maelezo katika sehemu ya "Muziki" au yamekosewa, wasiliana na lebo au msambazaji wako. Wanaweza kututumia sasisho la metadata lililo na maelezo sahihi.

Tunashirikiana na washirika wetu wa sekta ya muziki ili kuongeza data zaidi na kuimarisha ubora na usahihi wa maelezo tuliyo nayo.

Kwenye video zilizo na nyimbo nyingi, maelezo kuhusu nyimbo kumi za kwanza yataonekana katika sehemu ya “Muziki”.

Itakuwaje ikiwa nitasikia wimbo wangu katika video, lakini sioni maelezo ya “Muziki”?

Huenda sehemu ya "Muziki" isionekane kwa sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na:

  • YouTube haina data ya kutosha kutoka kwa mwenye hakimiliki.
  • Bado muziki wako haujatambulishwa.
  • Video ilidaiwa hivi karibuni na bado maelezo hayajawekwa.
  • Video hiyo iliwekewa alama kuwa "inalenga watoto."
Je, unashirikiana na studio ya kurekodia, mchapishaji wa muziki au jamii ya kukusanya mirabaha ambayo hudhibiti hakimiliki kwa niaba yako? Huenda ungependa kuwasiliana nao ili uthibitishe maelezo yaliyotumwa kwenye YouTube. Maelezo haya yanapaswa kujumuisha vitambulishi kama vile ISRC, ISWC, UPC na ISNI.

Itakuwaje ikiwa wimbo wangu utaorodheshwa, lakini maelezo ya waliohusika katika wimbo au sanaa ya albamu si sahihi?

Ikiwa wewe ni msanii unayerekodi au mwandishi wa nyimbo na wimbo wako umetambuliwa kuwa na maelezo yasiyo sahihi au yasiyo kamili, tafadhali hakikisha kuwa wewe pamoja na nyimbo zako zimesajiliwa na Mamlaka ya ISNI. Kujisajili kunaweza kutusaidia kuthibitisha kuwa tuna data bora zaidi ya kukuwakilisha pamoja na muziki wako.

Je, unashirikiana na studio ya kurekodia, mchapishaji wa muziki au jamii ya kukusanya mirabaha ambayo hudhibiti hakimiliki kwa niaba yako? Huenda ungependa kuwasiliana nao ili uthibitishe maelezo yaliyotumwa kwenye YouTube. Maelezo haya yanapaswa kujumuisha vitambulishi kama vile ISRC, ISWC, UPC na ISNI. Lebo au wasambazaji wa muziki wanaweza kututumia faili za maudhui za kazi ya sanaa pamoja na metadata iliyosasishwa.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
13607020829362602282
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false