Kuthibitisha utambulisho au maelezo yako ya malipo

Kwa shughuli mahususi za Akaunti ya Google, kama vile kujisajili kwa ajili ya bidhaa au huduma za Google, miamala au mabadiliko ya njia ya kulipa, unaweza kuhitaji kuthibitisha utambulisho au umiliki wako wa njia ya kulipa iliyotumiwa.
Kidokezo: Ili uthibitishe utambulisho wako kwenye programu ya Google Pay, fuata maagizo haya.

Kuhusu uthibitishaji

Sababu inayoweza kutufanya kukuomba uthibitishe
  • Ili kuthibitisha kuwa maelezo yako ni sahihi unapofikia maudhui mahususi.
  • Ili kuthibitisha utambulisho wako unapokamilisha muamala kupitia Google.
  • Tunapobaini shughuli au miamala isiyo ya kawaida.
  • Tunapohitaji maelezo zaidi kwa sababu za kisheria au kikanuni.

Muhimu: Tukikuomba uthibitishe akaunti yako, miamala yoyote ambayo haijashughulikiwa itaghairiwa. Utozaji unaoshughulikiwa kwenye taarifa yako ya benki utatoweka ndani ya siku 14 za kazi.

Maelezo ambayo huenda ukaombwa kutoa

Ili ukamilishe uthibitishaji, unaweza kuombwa uthibitishe kila njia ya kulipa. Ili ufanye hivyo, unaweza kuomba namba ya kuthibitisha.

Unaweza pia kuombwa utoe:

  • Jina la kisheria
  • Jina linalotumika kwenye Taarifa zako za malipo
  • Anwani
  • Tarehe ya kuzaliwa
  • Picha ya kitambulisho chako cha serikali
  • Ithibati ya anwani
  • Picha ya njia yako ya kulipa
Jinsi tunavyotumia maelezo yako

Google hutumia maelezo unayotoa:

  • Kuthibitisha utambulisho na njia yako ya kulipa.
  • Kukulinda dhidi ya ulaghai na matumizi mabaya.
  • Kuboresha huduma za uthibitishaji kwenye bidhaa za Google.

Maelezo yako yaliyothibitishwa, kama vile jina na anwani, yanahifadhiwa kwenye Akaunti yako ya Google. Unaweza kudhibiti maelezo yako yaliyothibitishwa katika payments.google.com.

Panapohitajika, maelezo unayowasilisha yanashughulikiwa kwa mujibu wa Sera ya Faragha ya Google na Ilani ya Faragha ya Google Payments.

Jinsi ya kukamilisha uthibitishaji

Ili uthibitishe maelezo yako, huenda ukahitaji kutuma hati au kuomba namba ya kuthibitisha. Baadhi ya njia za uthibitishaji huenda zisipatikane kulingana na bidhaa au shughuli unayotaka kukamilisha.

  1. Nenda kwenye payments.google.com.
  2. Ingia katika akaunti yako.
  3. Katika upande wa juu kulia, bofya Arifa AlertkishaThibitisha.
  4. Karibu na kadi ambayo lazima ithibitishwe, bofya Thibitisha.
  5. Fuata maagizo yaliyo kwenye skrini ili utumie njia yako ya uthibitishaji.
  6. Rudia hatua zilizo hapo juu kwa kila njia ya kulipa ambayo lazima ithibitishwe.

Njia za uthibitishaji

Ili ukamilishe uthibitishaji, utaombwa utumie mojawapo ya njia zifuatazo.

Kuomba namba ya kuthibitisha
  1. Bofya Pata namba ya kuthibitisha.
  2. Nenda kwenye tovuti ya kampuni iliyotoa njia yako ya kulipa kisha uingie katika akaunti yako.
  3. Katika historia yako ya miamala, tafuta gharama zinazotozwa kwa muda mfupi za chini ya USD $1.95 zinazoitwa "GOOGLE." Namba ya kuthibitisha ni tarakimu 6 za mwisho.
    • Kiasi cha gharama za muda mfupi hutofautiana kulingana na aina ya sarafu.
    • Unapaswa kupata namba ya kuthibitishwa papo hapo, lakini inaweza kuchukua hadi siku 7.
    • Kidokezo: Gharama au kiasi kinachotengwa kwenye akaunti yako ni cha muda tu. Gharama zinarejeshwa ndani ya siku 30.
  4. Weka namba ya kuthibitisha yenye tarakimu 6.
  5. Bofya Thibitisha.
Kupakia hati

Muhimu:

  • Maelezo unayopakia katika mchakato huu hutumiwa kwa madhumuni ya utambulisho pekee na hushughulikiwa kwa kufuata masharti ya udhibiti katika eneo ulipo.
  • Njia hii ya kupakia hati haipatikani kwa uthibitishaji wa ununuzi kwenye YouTube na Google Store.

Ili uthibitishe utambulisho na njia yako ya kulipa, tafuta ombi la uthibitishaji. Ili upate orodha ya hati na maagizo yanayokubaliwa, tumia kiungo kilicho kwenye ombi la uthibitishaji.

Hakikisha kuwa hati zako:

  • Zinatumia jina kamili lile lile kwenye hati zote unazowasilisha.
  • Zimesasishwa na muda wake haujaisha.
  • Zinasomeka.

Hakikisha kuwa picha unayopakia:

  • Ni picha ya hati na si kitu kingine
  • Inasomeka
  • Ina rangi, si rangi nyeusi na nyeupe
  • Haina ukungu, mweko au mwanga hafifu
  • Inaonyesha pembe zote 4 za hati nzima

Ikiwa utaondoa maandishi kwenye hati:

  • Kwa taarifa za benki, ondoa maandishi:
    • Kwenye namba za akaunti kamili ili tarakimu 4 tu za mwisho zionekane
    • Kwenye salio la akaunti au miamala yoyote. Salio la akaunti na miamala havihitajiki kwa madhumuni ya uthibitishaji
  • Ili uondoe maandishi, unaweza kuchora kisanduku cheusi ili ufunike taarifa nyeti kabla ya kuipakia.

Vidokezo:

  • Hakikisha jina, anwani na maelezo yako ya malipo yamesasishwa katika payments.google.com.
  • Baada ya kutuma hati zako, uthibitishaji unaweza kuchukua siku chache.

Kuthibitisha kwa taarifa ya benki (Wasanidi Programu wa Google Play pekee)

Katika nchi au maeneo fulani, Wasanidi Programu wa Google Play wanaweza kulazimika kuthibitisha njia yao ya kulipa kwa taarifa ya benki. Taarifa za benki unazopakia haziwezi kuwa za zaidi ya siku 180.

  1. Ingia katika akaunti ya payments.google.com.
  2. Bofya Usajili na Huduma.
  3. Chini ya "Programu za Google Play,” bofya Dhibiti.
  4. Chini ya “Jinsi utakavyolipwa,” bofya Weka njia ya kulipa.
  5. Tafuta akaunti ya benki uliyoweka kama njia yako ya kulipa.
  6. Bofya Thibitisha.
  7. Pakia nakala ya taarifa yako ya benki. Unaweza kupakia picha au PDF.
    • Ondoa taarifa nyeti kwenye taarifa za benki lakini hakikisha kuwa maelezo yaliyo hapa chini yanaonekana vizuri:
      • Tarakimu 4 za mwisho za namba ya akaunti ya benki
      • Jaza maelezo ya namba ya uelekezaji, namba maalum ya benki, msimbo wa IFSC, namba ya uelekezaji, msimbo wa SWIFT au kitambulisho kinachofanana.
      • Kulingana na mahaali uliko ulimwenguni, Msimbo wa Kutambulisha Benki unaweza kuwa na jina tofauti.

Baada ya kutuma taarifa yako ya benki, uthibitishaji unaweza kuchukua siku chache.

Kurekebisha hitilafu zinazotokana na uthibitishaji

Kurekebisha hitilafu zinazotokana na namba za kuthibitisha na pesa zinazotengwa kwa muda

Pata maelezo kuhusu jinsi ya kurekebisha hitilafu unapojaribu kuthibitisha njia za kulipa kwa kutumia namba ya kuthibitisha.

Kurekebisha hitilafu zinazotokana na uthibitishaji wa hati

Ili kutatua hitilafu:

  • Ukipokea barua pepe au ukipokea ujumbe kuhusu hitilafu: Fuata maagizo katika ujumbe.
  • Iwapo unahitaji usaidizi kutoka kwa timu yetu ili kukusaidia kutatua hitilafu hii: Tutawasiliana nawe baada ya kukagua maelezo yako.

Kushindwa kuthibitisha

Iwapo umeshindwa kuthibitisha, utapokea barua pepe muda mfupi baada ya uamuzi huo. Ili kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo, fuata maagizo katika barua pepe.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
2596546050121238442
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false