Kutazama YouTube kwenye televisheni yako inayoweza kuunganisha kwenye intaneti kwa kuunganisha kwenye vifaa vyako

Kwa kutazama YouTube kwenye televisheni yako inayoweza kuunganisha kwenye intaneti, unaweza kufurahia video zenye ubora wa juu wa picha na sauti katika skrini kubwa zaidi. 

Jinsi ya Kuingia Kwenye YouTube katika Televisheni Yako

Katika makala haya, utajifunza jinsi ya kuunganisha vifaa vyako kwenye televisheni yako inayoweza kuunganisha kwenye intaneti kwa:

  • Kutuma maudhui: Tumia simu, kishikwambi au kompyuta yako kutuma video ya YouTube kwenye televisheni yako na uitazame kwenye skrini kubwa zaidi.
  • Kuoanisha: Huku ukitazama YouTube kwenye televisheni yako, oanisha simu na televisheni yako ili uendelee kudhibiti video kutoka kwenye simu yako.
  • Kutumia msimbo wa televisheni: Ikiwa simu na televisheni yako zimeunganishwa kwenye mitandao tofauti ya Wi-Fi, unaweza kuziunganisha ukitumia msimbo wa televisheni kisha utume video kwenye televisheni yako. 

Iwapo hutumii msimbo wa televisheni au kompyuta kuunganisha, hakikisha kuwa umepakua programu ya YouTube kwenye simu au kishikwambi chako.

Madokezo:
  • Iwapo wewe ni mwanachama wa YouTube TV unayetaka kutazama YouTube TV kwenye televisheni yako, angalia Kituo cha Usaidizi cha YouTube TV ili upate maelezo zaidi.
  • Huenda baadhi ya vipengele visipatikane kwenye akaunti zinazodhibitiwa kwenye YouTube.
  • Ikiwa umeingia katika akaunti ya Wasifu kwenye YouTube Kids ukitumia programu ya YouTube kwenye televisheni yako inayoweza kuunganisha kwenye intaneti, kifaa cha kutiririsha au kifaa cha michezo ya video, unaweza kupata ujumbe kuhusu hitilafu unapojaribu kutuma video. Ukipata hitilafu, badilisha utumie wasifu tofauti.

Kutuma YouTube kwenye kifaa cha kutiririsha au televisheni yako inayoweza kuunganisha kwenye intaneti

Kipengele cha Kutuma maudhui  kinakuwezesha utumie simu, kishikwambi au kompyuta yako kudhibiti hali ya utumiaji wako wa YouTube kwenye televisheni yako. Ili utume maudhui kutoka kwenye kifaa cha mkononi au kishikwambi, hakikisha kuwa umepakua programu ya YouTube. Huwezi kutuma maudhui kutoka youtube.com kwenye kivinjari cha kifaa cha mkononi.

 

Jinsi ya Kutuma YouTube kwenye televisheni inayoweza kuunganisha kwenye intaneti au Kifaa cha Kutiririsha

Kuanza kutuma maudhui

Ili uunganishe televisheni yako inayoweza kuunganisha kwenye intaneti au kifaa cha kutiririsha:

  1. Hakikisha iPhone au iPad na televisheni inayoweza kuunganisha kwenye intaneti au kifaa chako cha kutiririsha vimeunganishwa kwenye mtandao mmoja wa Wi-Fi.

  2. Fungua programu ya YouTube kwenye kifaa cha kutiririsha au televisheni yako inayoweza kuunganisha kwenye intaneti.

  3. Fungua programu ya YouTube kwenye iPhone au iPad yako.

  4. Nenda kwenye video ambayo unataka kutazama kisha uguse Tuma  kwenye kicheza video.

    • Kumbuka: Ikiwa kifaa chako kinatumia toleo la iOS 14 au matoleo mapya zaidi, ipatie YouTube ruhusa ya kuunganisha kwenye vifaa vyako vya kutiririsha katika mtandao wako wa karibu ili utume maudhui kwenye televisheni yako. 

  5. Chagua kifaa ambako ungependa kutuma maudhui na usubiri kiunganishwe. Baada ya kuunganishwa, video itacheza kwenye televisheni au kifaa chako cha kutiririsha.

Kuruhusu Ufikiaji wa Mtandao wa Karibu

Ikiwa iPhone au iPad yako inatumia toleo la iOS 14 au matoleo mapya zaidi, ni lazima uipate YouTube ruhusa ya kuunganisha kwenye vifaa vya kutiririsha katika mtandao wako wa karibu ili uweze kutuma maudhui kwenye televisheni yako. Iwapo unatumia zaidi ya programu moja ya YouTube, ni lazima uruhusu kila programu iunganishwe kwenye Mtandao wa Karibu (kwa mfano, YouTube, YouTube Music, YouTube TV, YouTube Kids). Wakati Mtandao wa Karibu umezimwa, huduma ya kutuma haitafanya kazi.

Fuata maagizo haya kwenye mipangilio ya kifaa chako au katika programu ya YouTube:

Kwenye iPhone au iPad yako:

  1. Nenda kwenye Mipangilio.
  2. Pitia orodha ya programu na uchague programu ya YouTube unayotumia kutuma maudhui (kwa mfano, YouTube, YouTube Music, YouTube TV, YouTube Kids).
  3. Washa Mtandao wa Karibu.

Katika YouTube:

  1. Fungua programu ya YouTube (kwa mfano, YouTube, YouTube Music, YouTube TV, YouTube Kids)
  2. Gusa Tuma .
  3. Fuata maagizo ili uruhusu programu ifikie Mtandao wako wa Karibu.
  4. Katika orodha ya vifaa vinavyopatikana, gusa jina la kifaa ambacho ungependa kuunganisha.

Kubadilisha kutoka kifaa kimoja hadi kingine huku ukituma video

Unaweza kutumia programu za YouTube na YouTube Music ili uhamishe video kwa urahisi kutoka kifaa kimoja hadi kingine. Ili ubadilishe kutoka kifaa kimoja hadi kingine wakati unatuma maudhui kutoka televisheni au kifaa kingine cha kutiririsha:

  1. Gusa Tuma  kwenye kicheza video. 
  2. Gusa kifaa ambako unataka kuhamishia video yako.
  3. Video yako itahamishiwa kwenye kifaa kilichochaguliwa.

Kutenganisha kwenye kifaa cha kutiririsha au televisheni yako inayoweza kuunganisha kwenye intaneti

  1. Gusa Tuma .
  2. Gusa Simu hii ili uache kutuma video kutoka kwenye kifaa cha kutiririsha au televisheni yako inayoweza kuunganisha kwenye intaneti.

Kuoanisha YouTube na simu au kishikwambi chako

Mchakato wa kuunganisha hukuwezesha kuunganisha YouTube kwenye televisheni yako inayoweza kuunganisha kwenye intaneti au kifaa chako cha kutiririsha na simu au kishikwambi chako. Ili uoanishe kifaa, ni lazima uingie katika Akaunti ile ile ya Google kwenye televisheni na simu au kishikwambi chako.

Jinsi ya kuoanisha simu na televisheni yako wakati unatazama YouTube

Kuoanisha

Ili uunganishe kifaa cha mkononi na televisheni inayoweza kuunganisha kwenye intaneti au kifaa chako cha kutiririsha:

  1. Washa televisheni yako inayoweza kuunganisha kwenye intaneti au kifaa chako cha kutiririsha.
  2. Kwenye kifaa cha mkononi au kishikwambi chako, fungua programu ya YouTube.
    • Kumbuka: Hakikisha umeingia katika Akaunti ile ile ya Google kwenye televisheni na kifaa chako cha mkononi.
  3. Unapoombwa kufanya hivyo, gusa Unganisha ili uoanishe kifaa chako cha mkononi na televisheni yako.
    • Iwapo hutapata dirisha ibukizi au umelifunga kimakosa, unganisha ukitumia kipengele cha Kutuma au msimbo wa televisheni.
  4. Kicheza video kitafunguka katika programu kwenye kishikwambi au simu yako, hali inayoonyesha kuwa umeunganisha kwenye televisheni au kifaa chako cha kutiririsha.

Kubatilisha uoanishaji

Ili ubatilishe uoanishaji wa kifaa chako cha mkononi na televisheni inayoweza kuunganisha kwenye intaneti au kifaa chako cha kutiririsha:

  1. Gusa Tuma .
  2. Kisha uguse TENGANISHA.

Kuunganisha YouTube kwenye televisheni yako ukitumia msimbo wa televisheni

Unapounganisha simu au kishikwambi chako na televisheni inayoweza kuunganisha kwenye intaneti au kifaa chako cha kutiririsha ukitumia msimbo wa televisheni, unaweza kutazama YouTube kwenye televisheni yako wakati hujaunganishwa kwenye Wi-Fi. Tumia simu au kishikwambi chako kucheza maudhui kwenye televisheni au kifaa chako cha kutiririsha.

Msimbo wa televisheni haupatikani ikiwa unatumia kompyuta. Ikiwa unatumia kompyuta kuunganisha kwenye televisheni au kifaa chako cha kutiririsha, ni lazima utumie kipengele cha Kutuma badala yake.

Jinsi ya Kuunganisha YouTube kwenye Televisheni yako ukitumia Msimbo

Kuunganisha vifaa ukitumia msimbo wa televisheni

  1. Fungua programu ya YouTube kwenye kifaa cha kutiririsha au televisheni yako inayoweza kuunganisha kwenye intaneti.
  2. Nenda kwenye Mipangilio .
  3. Nenda kwenye Unganisha ukitumia msimbo wa TV. Msimbo wa samawati wa televisheni utaonekana kwenye televisheni yako. Msimbo huu utakuwa nambari pekee.
  4. Fungua programu ya YouTube kwenye kishikwambi au simu yako.
  5. Gusa Tuma .
  6. Gusa Unganisha kwa kutumia msimbo wa televisheni .
Weka msimbo wa samawati wa televisheni unaoonyeshwa kwenye televisheni yako na uguse UNGANISHA.

Kutenganisha na kuunganisha upya vifaa vyako

Baada ya kuunganisha vifaa vyako ukitumia msimbo wa televisheni, unaweza kutenganisha na kuviunganisha tena ili kucheza maudhui yaliyo kwenye kifaa chako kwenye televisheni.

Kutenganisha kifaa kilichounganishwa kwenye televisheni yako

  1. Gusa Tuma .
  2. Gusa Tenganisha.

Kuunganisha upya kifaa kilichounganishwa kwenye televisheni yako

  1. Washa YouTube kwenye televisheni yako inayoweza kuunganisha kwenye intaneti.
  2. Fungua programu ya YouTube kwenye kishikwambi au simu yako.
  3. Gusa picha yako ya wasifu .
  4. Gusa Mipangilio .
  5. Gusa Jumla.
  6. Gusa Tazama kwenye televisheni..
  7. Tafuta kifaa cha televisheni kilichounganishwa awali na ubofye UNGANISHA

Kutenganisha vifaa ambavyo viliunganishwa kwa kutumia msimbo wa TV

Iwapo hungependa kutumia simu au kishikwambi chako tena kwenye televisheni yako inayoweza kuunganisha kwenye intaneti au kifaa cha kutiririsha, unaweza kuvitenganisha. Baada ya kifaa kuondolewa, ni lazima utumie msimbo mpya ili kuunganisha tena.

Unaweza kuondoa vifaa vilivyounganishwa kupitia:

  • Kifaa chako cha kutiririsha au televisheni yako inayoweza kuunganisha kwenye intaneti AU
  • Simu au kishikwambi

Huwezi kutenganisha kila kifaa kivyake. Hatua ya kutenganisha kifaa kimoja itaondoa vifaa vyote vilivyounganishwa.

Kutenganisha kwenye televisheni yako inayoweza kuunganisha kwenye intaneti au kifaa chako cha kutiririsha

  1. Kwenye kifaa cha kutiririsha au televisheni yako inayoweza kuunganisha kwenye intaneti, fungua programu ya YouTube.
  2. Nenda kwenye Mipangilio .
  3. Chagua Vifaa vilivyounganishwa.
  4. Chagua Tenganisha vifaa vyote ili utenganishe vifaa vyote mara moja.

Kutenganisha kishikwambi au simu yako

  1. Fungua programu ya YouTube kwenye kishikwambi au simu yako.
  2. Gusa picha yako ya wasifu .
  3. Gusa Mipangilio .
  4. Gusa Jumla.
  5. Gusa Tazama kwenye televisheni..
  6. Gusa Futa Vifaa.
  7. Gusa FUTA ili uondoe kifaa cha kutiririsha au televisheni iliyounganishwa inayoweza kuunganisha kwenye intaneti.

 Kuvinjari YouTube kwenye kifaa cha kutiririsha au televisheni yako inayoweza kuunganisha kwenye intaneti

Kutumia programu ya YouTube kama kidhibiti cha mbali

  1. Gusa Tuma .
  2. Gusa Kidhibiti cha mbali .
  3. Tumia kidhibiti cha mbali kwenye skrini kudhibiti hali yako ya kutuma.

Kutumia kidhibiti cha mbali cha televisheni yako inayoweza kuunganisha kwenye intaneti

  • Jaribu kutumia kidhibiti cha mbali cha televisheni yako ili kudhibiti hali yako ya kutuma. Vidhibiti vingi vya mbali vya televisheni vinatumika bila mipangilio ya ziada.
  • Ikiwa kidhibiti chako cha mbali hakifanyi kazi, angalia mwongozo wa maelekezo ya televisheni yako inayoweza kuunganisha kwenye intaneti ili kufahamu ikiwa inatumia huduma ya CEC. Ikiwa ni hivyo, fuata maelekezo kwenye mwongozo ili uwashe kipengele cha CEC na ujaribu kutumia kidhibiti chako cha mbali ili kudhibiti hali ya kutuma.

Kudhibiti kwa sauti maudhui unayotuma

  1. Fungua video kwenye programu ya YouTube.
  2. Gusa Tuma .
  3. Gusa maikrofoni .
  4. Zungumza kwenye kifaa chako ili udhibiti hali yako ya kutuma.

Kudhibiti kwa sauti hakupatikani katika vifaa vyote.

 

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
12159360814061816672
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false