Kupakia video ili uchume mapato kupitia matangazo

Kuna vigezo kadhaa vya kuzingatia unapopakia video unayotaka kutumia kuchuma mapato kupitia matangazo.

Kukagua ili kubaini ufaafu wa matangazo wakati wa kupakia video

Unaweza kutumia ukurasa wa Ukaguzi unapopakia video ili uikague kubaini ufaafu kwa matangazo na madai ya hakimiliki kabla ya kuichapisha. Ukaguzi huu unakusaidia upate maelezo kuhusu vikwazo ya uchumaji mapato vinavyoweza kuwepo ili uweze kurekebisha matatizo kabla ya video yako kuchapishwa.

"Ukaguzi" wa Hakimiliki na Ufaafu kwa Matangazo kwenye Mchakato wa Upakiaji

Jinsi Uthibitishaji Unaojifanyia unavyosaidia

Kupitia Uthibitishaji Unaojifanyia, watayarishi wote kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube wana udhibiti zaidi kuhusu maamuzi ya uchumaji mapato. Unaweza pia kuona hali ya uchumaji wa mapato inayotarajiwa na uwezekano wa mapato katika muda halisi.

Kwa watayarishi walio na historia ya ukadiriaji wenye usahihi wa hali ya juu: Tutatumia data yako ya ukadiriaji kufanya uamuzi wa mwanzo wa uchumaji wa mapato. Kisha unaweza kuchapisha na kuchuma mapato kupitia video yako mara tu baada ya kuipakia. Iwapo mifumo yetu itabaini tofauti yoyote katika ukadiriaji wako, kuna uwezekano mdogo kuwa utabadilika. Tofauti nyingi hubainika ndani ya saa moja.

Kwa watayarishi ambao ni mara yao ya kwanza kufanya Uthibitishaji Unaojifanyia au wana historia ya ukadiriaji wenye usahihi wa hali ya chini: Tutategemea zaidi mifumo yetu ya kiotomatiki kwa ajili ya maamuzi ya uchumaji wa mapato. Pia kuna aikoni ya 'inakagua' uchumaji wa mapato ili kuonyesha kwa udhahiri mchakato wa ukaguzi unapokuwa bado unaendelea. Video haziwezi kutumika kuchuma mapato kupitia matangazo hadi ukaguzi wa mfumo ukamilike.

Ili uone historia yako ya ukadiriaji, angalia Fahamu hali ya ukadiriaji wako.

Kuelewa aikoni zetu za uchumaji mapato

Ifuatayo ni maana ya aikoni tofauti:

 Ya kijani: Uchumaji wa mapato “umewashwa” na video iko tayari kuchapishwa.

 Ya njano: Maudhui yako yanaweza kuonyesha matangazo machache au huenda yasionyeshe kabisa matangazo kutoka kwa watangazaji wote. Unaweza kuchapisha, kuhariri video au kuipakia tena au kuomba maudhui yako yafanyiwe uhakiki na binadamu.

 Nyekundu: Umewasha uchumaji wa mapato lakini kwa sababu kuna madai ya hakimiliki kwenye video, video haiwezi kutumiwa kuchuma mapato. Wakati mwingine, unaweza kupinga dai.

 Ya kijivu: Umechagua kutowasha mipangilio ya uchumaji wa mapato kwenye video hii.

 Ukaguzi: Ukaguzi wa mifumo bado unaendelea. Bado unaweza kuifanya video ionekane hadharani wakati ukaguzi unaendelea, lakini tunapendekeza usubiri hadi ukaguzi ukamilike kabla ya kuichapisha. Ili kuongeza mapato, subiri hadi aikoni hii ibadilishwe na aikoni ya kijani, njano au nyekundu, hatua inayomaanisha kuwa ukaguzi umekamilika. Kumbuka kuwa watayarishi wengi hawataona aikoni hii kwa sababu mifumo yetu kwa kawaida huwa na kasi au tumetegemea data uliyoweka ya Uthibitishaji Unaojifanyia.

Pata maelezo zaidi kuhusu maana ya kila aikoni kwenye mwongozo wetu wa aikoni za uchumaji wa mapato.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
1640930889765097999
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false