Vipengele vinavyodhibitiwa kwenye baadhi ya video

YouTube hairuhusu matamshi ya chuki. Tunaondoa maudhui yanayotangaza vurugu au chuki dhidi ya watu binafsi au makundi kulingana na sifa fulani. YouTube pia hairuhusu maudhui yanayokusudiwa kusifu, kutangaza au kusaidia mashirika hatari ya uhalifu.

Maudhui ambayo hayakiuki sera zetu lakini yanakaribia kuwa na sifa zinazosababisha kuondolewa, au huenda yakawakera baadhi ya watazamaji, yanaweza kuzimiwa baadhi ya vipengele.

Maudhui yataendelea kupatikana kwenye YouTube, lakini ukurasa wa kutazama hautakuwa tena na:

  • Maoni
  • Video zilizopendekezwa
  • Imependwa mara

Ukurasa wa kutazama pia utawekwa nyuma ya ujumbe wa onyo. Video hizi pia hazistahiki kupata matangazo. Kuzima vipengele hakutaongeza onyo kwenye chaneli yako.

Ikiwa mojawapo ya video zako ina vipengele vimezimwa, tutakutumia barua pepe ili tukufahamishe. Unaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi moja kwa moja kutoka kwenye kiungo katika barua pepe utakayotumiwa au kwa kufuata mchakato wa rufaa.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
9238760367543735712
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false