Jinsi matangazo yanavyoonekana kwenye video unazochuma mapato

Tumerahisisha chaguo za miundo ya matangazo yanayoonyeshwa kabla au baada ya video yako kucheza ili kuongeza mapato ya mtayarishi. Tumeondoa chaguo za matangazo mahususi kwa matangazo yanayoonyeshwa kabla ya video kucheza au baada ya video kucheza, yanayoweza kurukwa na yasiyorukika. Sasa unapowasha matangazo kwenye video ndefu mpya, tunawaonyesha watazamaji wako matangazo yanayoonyeshwa kabla ya video kucheza au baada ya video kucheza, yanayoweza kurukwa na yasiyorukika panapofaa. Badiliko hili linafanya mbinu bora zinazopendekezwa za kuwasha miundo yote ya matangazo zifae kwa kila mtu. Chaguo zako za matangazo yanayochezwa katikati ya video hazijabadilika. Pia, tumehifadhi chaguo zako za matangazo katika video ndefu zilizopo, isipokuwa ukibadilisha mipangilio ya uchumaji wa mapato.

Unapowasha uchumaji wa mapato kwenye chaneli yako, unaweza kuchagua kugawana mapato yanayotokana na matangazo yanayoonyeshwa kwenye Ukurasa wa Kutazama au kwenye Mipasho ya Video Fupi. Matangazo yanaonyeshwa kupitia mnada wa matangazo, Kidhibiti cha Matangazo cha Google na vyanzo vingine vinavyouzwa na YouTube. Baada ya kuwasha uchumaji wa mapato, huenda ikachukua muda fulani kabla ya matangazo kuonekana.

Matangazo kwenye video zako huchaguliwa kiotomatiki kulingana na muktadha kama vile metadata ya video yako na ikiwa maudhui yanawafaa watangazaji.

Tunafuatilia na kusasisha mifumo yetu mara kwa mara ili kuonyesha matangazo yanayofaa zaidi kwenye video zako. Hata hivyo, hatudhibiti sisi wenyewe kila tangazo linaloonyeshwa kwenye video zako, hivyo hatuwezi kukuhakikishia kuwa tutacheza matangazo mahususi.

Matangazo hayataonyeshwa kila wakati kwenye video zinazochuma mapato. Huenda tangazo lisipatikane wakati wa muda wa kutazama. Ikiwa unafikiri kuna tatizo la matangazo, fahamu kwa nini matangazo yanaweza yasionyeshwe kwenye video zako.

Matangazo Yanayouzwa na Washirika ni nini?

Tangu mwaka 2010, YouTube imeruhusu washirika wachache kuuza matangazo ya maudhui wanayoweka YouTube. Matangazo haya yanaitwa "matangazo yanayouzwa na washirika". Ili kutimiza masharti ya matangazo yanayouzwa na washirika, ni lazima mashirika yasambaze maudhui kwenye mifumo mbalimbali na yawe na miundombinu ya kampuni (ikijumuisha timu ya mauzo) ili kuuza matangazo kwenye ya video zao.

Kwa matangazo yanayouzwa na washirika, washirika hufanya kazi moja kwa moja na watangazaji ili kuonyesha matangazo kwenye maudhui wanayomiliki. Watangazaji wananunua matangazo kutoka kwa washirika hawa ili matangazo yaonyeshwe kwenye maudhui mahususi. Hii ina maana kwamba matangazo yanayouzwa na washirika yanaweza kuonyeshwa hata kwenye video ambazo YouTube inaona kuwa "hazifai kwa watangazaji wengi". Washirika hawa wana wajibu kamili wa kuwekelea tangazo kwa kufanya kazi moja kwa moja na watangazaji. Wanachukua jukumu kamili la kuweka matangazo kwenye maudhui ambayo watangazaji wanafikiri kuwa si faafu kwa chapa.

Washirika hawawezi kuuza matangazo kwenye maudhui yanayohusiana na mikasa.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
14312045880224723848
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false