Nimeshindwa kutazama video niliyopakua

Pata maelezo kuhusu jinsi ya kupakua video na ukague hatua zilizo hapa chini ili utatue tatizo lako.

Kama hatua ya kwanza inayotatua matatizo mengi yanayotokea mara kwa mara, funga programu ya YouTube au dirisha la kivinjari kisha ulifungue tena. Kisha, jaribu kuzima kisha uwashe kifaa chako.

Pakua upya video kwenye vifaa vipya

Iwapo ulinunua kifaa kipya hivi karibuni, utahitaji kupakua tena video zozote ambazo ungependa kutazama. Video hazihamishwi kwenda kwenye vifaa vingine, hata kama umeingia katika akaunti hiyohiyo. Video ulizopakua ni mahususi kwa kila kifaa.

Hakikisha kuwa muda wa uanachama wako haujaisha

Hakikisha kuwa muda wa uanachama wako wa YouTube Premium haujaisha.

Katika programu ya YouTube, gusa picha yako ya wasifu kisha Uanachama unaolipiwa na uende chini hadi kwenye sehemu ya Dhibiti.

  • Iwapo ulipoteza uwezo wa kufikia YouTube Premium hivi majuzi na ukajisajili tena, inaweza kuchukua saa kadhaa kabla ya video ulizohifadhi kuonekana ukishajisajili tena.
  • Iwapo unahitaji kutazama video sasa hivi, gusa Menyu Three-dot menu vertical kisha uchague Jaribu tena kupakua.
  • Iwapo muda wa uanachama wako wa YouTube Premium utaisha, hutaweza tena kufikia video ulizopakua. Ili uweze kufikia vipakuliwa vyako tena, jisajili kwenye Uanachama wa Premium.

Hakikisha kuwa umeingia katika YouTube Premium

Hakikisha kuwa umeingia katika akaunti ya Google inayohusishwa na uanachama wako wa YouTube Premium:

  • Jaribu kuondoka kisha uingie tena katika akaunti inayohusishwa na YouTube Premium.
  • Hakikisha kuwa unaona nembo ya YouTube Premium (badala ya nembo ya YouTube). Katika programu ya YouTube ya vifaa vya mkononi au kwenye kompyuta yako, unapaswa kuona nembo ya YouTube Premium katika kona ya juu kushoto ya programu au kivinjari chako.
Je, unatumia YouTube katika televisheni inayoweza kuunganisha kwenye intaneti?
  • Hakikisha kuwa umeingia katika akaunti kwenye televisheni yako inayohusishwa na uanachama wako wa YouTube Premium.
  • Iwapo unatuma maudhui kwenye televisheni, hakikisha kuwa umeingia katika akaunti kwenye televisheni na kompyuta au kifaa unachotumia. 
  • Iwapo unatumia Google Home, hakikisha kuwa umeingia katika akaunti sahihi kwenye programu ya Google Home.

Wasiliana na timu ya usaidizi na utume maoni kuhusu bidhaa

Iwapo bado unatatizika, wasiliana na timu ya usaidizi. Unapowasiliana na timu ya usaidizi, taja yafuatayo:

  • Je, unaona ujumbe kuhusu hitilafu?
  • Unaonekana wapi na maandishi halisi ni yapi? Jumuisha picha ya skrini, ikiwezekana.
Kutuma maoni kuhusu bidhaa kwenye YouTube:
  • Unaweza pia kutuma maoni kuhusu tatizo lako. Hutapata jibu, lakini maoni yako yatashirikiwa na YouTube.
  • Ili utume maoni kuhusu bidhaa, chagua picha yako ya wasifu kisha Maoni Feedback katika YouTube.
  • Hakikisha kuwa unachagua kisanduku cha "Kumbukumbu za mfumo" ili utusaidie kufahamu tatizo lako vyema.

Rudi kwenye Tatua matatizo yanayohusu manufaa ya uanachama wa YouTube Premium.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
14633458704066128678
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false