Kipengele cha uchezaji wa chinichini hakifanyi kazi

Kipengele cha uchezaji wa chinichini hufanya kazi tu katika programu ya YouTube ya vifaa vya mkononi na kinahitaji Uanachama wa YouTube Premium. Baadhi ya video haziwezi kuchezwa chinichini au kupakuliwa nje ya mtandao, hata kama una uanachama katika chaneli. Kagua hatua zilizo hapa chini ili upate usaidizi wa kusuluhisha tatizo lako.

Hatua za kawaida za utatuzi

 Zima kisha uwashe programu ya YouTube au uwashe kifaa chako tena

Iwapo programu ya YouTube au kifaa chako cha mkononi kimekuwa kikitumika kwa muda, huenda hamna nyenzo za kutosha kwa uchezaji wa chinichini kufanya kazi vizuri. Jaribu kufunga programu ya YouTube au kuwasha simu yako tena.

Hakikisha kuwa muda wa uanachama wako haujaisha

Hakikisha kuwa muda wa uanachama wako wa YouTube Premium haujaisha. Katika programu ya YouTube, gusa picha ya wasifu wako kisha Uanachama unaolipiwa na uende chini kwenye sehemu ya Dhibiti.

Iwapo ulipoteza uwezo wa kufikia YouTube Premium na kisha ukajisajili tena, kumbuka kuwa inaweza kuchukua saa kadhaa kabla ya video ulizohifadhi kupatikana tena ukishajisajili tena. Iwapo unahitaji kutazama video sasa hivi, gusa Zaidi ''na uchague Jaribu kupakua tena.

Jaribu kuingia katika akaunti ya YouTube Premium tena

Hakikisha kuwa umeingia katika akaunti inayohusishwa na uanachama wako wa YouTube Premium.

  • Jaribu kuondoka kisha uingie tena katika akaunti inayohusishwa na YouTube Premium.
  • Hakikisha kuwa unaona nembo ya YouTube Premium (badala ya nembo ya YouTube) katika YouTube.

Angalia upatikanaji wa YouTube Premium katika eneo uliko

Manufaa ya YouTube Premium hutumiwa tu katika nchi ambako YouTube Premium inapatikana. Hakikisha kuwa uko katika eneo ambako YouTube Premium imezinduliwa.

Angalia mipangilio yako ya uchezaji wa chinichini

Angalia mipangilio yako ya uchezaji wa chinichini katika programu ya YouTube ili uhakikishe kuwa hujazima mipangilio hiyo.

Kusasisha programu yako ya YouTube

Hakikisha kuwa unatumia toleo jipya la programu ya YouTube. Tembelea duka la programu la kifaa chako na uangalie iwapo una masasisho yoyote yanayosubiri ya programu ya YouTube.

Iwapo una simu mpya, au umerejesha simu yako hivi majuzi, inaweza kuwa na toleo la zamani la programu ya YouTube (k.m., matoleo ya chini ya 12.0 huchukuliwa kuwa yamepitwa na wakati).

Kuangalia mipangilio ya data ya mtandao wa simu yako

Angalia mipangilio kwenye kifaa chako cha mkononi ili uhakikishe kuwa umewasha data ya chinichini kwenye YouTube.

Hatua za ziada unazoweza kujaribu

Thibitisha kuwa hamna programu nyingine zinazocheza sauti

Kagua programu nyingine zozote ambazo umefungua ili uhakikishe hamna inayocheza sauti. Uchezaji wa chinichini hautafanya kazi wakati programu nyingine zinacheza sauti.

Kuangalia uthabiti wa muunganisho wako wa intaneti

Upakuaji wa video unahitaji muunganisho thabiti wa intaneti. Hakikisha kuwa kifaa chako kimeunganishwa kwenye mtandao wa Wi-Fi yenye kasi ya Mbps 3 au haraka zaidi au mtandao wa simu wenye mpango wa data unaoruhusu mfumo wa 3G, 4G, au LTE. Iwapo huna uhakika kuhusu kasi ya sasa ya intaneti yako, unaweza kujaribu kasi yako mtandaoni.

Angalia mipangilio ya arifa ya simu yako

Hakikisha kuwa hujazuia arifa zote za programu ya YouTube. Unaweza kuthibitisha hili katika mipangilio ya kifaa chako. Iwapo umezuia arifa, huenda programu ya YouTube isiweze kufanya kazi vizuri na/au kufikia intaneti chinichini.

Iwapo hali hii itafanyika, utahitaji kuwasha upya arifa za YouTube katika kiwango cha mfumo wa uendeshaji na iwapo bado hungependa kupokea arifa, unaweza kuzizima kwenye mipangilio ya programu ya YouTube.

Wasiliana na timu ya usaidizi na utume maoni kuhusu bidhaa

Iwapo bado unatatizika, wasiliana na timu ya usaidizi. Unapowasiliana na timu ya usaidizi, taja yafuatayo:
  • Tafadhali bainisha iwapo sauti itakoma mara tu utakapoondoka kwenye programu au iwapo itacheza kwa muda kisha ikome bila kutarajiwa.
  • Tafadhali bainisha ujumbe wowote kuhusu hitilafu unaoona unaporudi kwenye programu.
  • Tafadhali tuma maoni ndani ya programu.
Kutuma maoni kuhusu bidhaa kwenye YouTube:
  • Unaweza pia kutuma maoni ndani ya bidhaa. Hutapata jibu, lakini maoni yako yatashirikiwa na timu za Bidhaa za YouTube.
  • Ili ufanye hili, chagua picha yako ya wasifu kisha Maoni Feedback.
  • Hakikisha kuwa unachagua kisanduku cha "Kumbukumbu za mfumo." Hatua hii hutusaidia tufahamu tatizo lako vyema. 

 

Rudi kwenye Tatua matatizo kuhusu manufaa ya wanachama wa YouTube Premium  

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
6561330390043884851
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false