Kurekebisha matatizo ya arifa za wanaofuatilia

Ili kutii Sheria ya Kulinda Faragha ya Watoto Mtandaoni (COPPA) na sheria zingine, arifa huzimwa kwenye maudhui yaliyowekwa kuwa “Yanalenga watoto.” Pata maelezo zaidi kuhusu kuweka mipangilio ya hadhira yako, a kwa nini ni muhimu kufanya hivyo kwa usahihi.

Kutatua tatizo la arifa

  1. Waombe watazamaji wakague mipangilio yao. Mipangilio ya watazamaji ya arifa husababisha karibu matatizo yote ya arifa. Waombe watazamaji watumie kitatuzi cha arifa ikiwa hawapokei arifa.
  2. Wajulishe wanaofutilia unapopakia video. Unapopakia video, weka kisanduku karibu na “Chapisha kwenye Mpasho wa wanaofuatilia na uwajulishe wanaofuatilia” kwenye kichupo cha “Mipangilio ya kina” kikiwa kimechaguliwa.
  3. Angalia ni mara ngapi umechapisha maudhui ndani ya saa 24 zilizopita. Watazamaji wanaweza kupokea arifa za hadi video mpya 3 kutoka kila kituo ndani ya kipindi cha saa 24. Pata maelezo zaidi kuhusu vikomo vya arifa hapo chini.
  4. Epuka kuchapisha video kwa wingi. Ukichapisha zaidi ya video 3 ndani ya kipindi kifupi, tunaweza kuacha kwa muda kutuma arifa kwa saa 24. Kuchapisha video kwa wingi kunaweza kuwachosha watazamaji na mifumo yetu ya arifa. Hatua hii ya kusimamishwa hufanyika hata ikiwa video zote isipokuwa 1 imeondolewa kwenye kutuma arifa. Ukipakia video chache kwa wakati mmoja, jaribu kuzipakia kuwa “Za Faragha” kwanza. Kisha, unaweza kuchapisha kila video wakati tofauti.
  5. Weka mipangilio ya video kuwa za umma baada ya kuzichapisha. Kwa kawaida, huchukua dakika 10 hadi 20 ili arifa zote zitumwe. Ukibadilisha kwa haraka mipangilio ya faragha ya video yako kuwa “Ya Faragha” baada ya kuchapisha, tutaacha kutuma arifa. 
  6. Angalia ikiwa idadi ya wanaofuatilia ilibadilika sana kabla ya kuchapisha video yako. Katika hali hizi, tutawaarifu wafuatiliaji wote wanaostahiki, lakini inaonekana kuwa chini ya asilimia 100 ya wanaofuatilia walipewa arifa kutokana na kucheleweshwa kwa ripoti.
  7. Angalia matatizo yanayojulikana. Katika hali chache, kunaweza kuwa na matatizo ya kuwasilisha arifa. Ili upate maelezo ikiwa matatizo haya yanatokea, angalia Sehemu ya Matatizo yanayojulikana ya Kituo cha Usaidizi au kitambulishi cha Twitter cha TeamYouTube.
  8. Tuma maoni. Ikiwa umeshughulikia mambo yote yaliyoainishwa hapo juu na bado wanaofuatilia hawapati arifa, tutumie maoni.

Notification - Backstage at YouTube

Fuatilia chaneli ya Watazamaji ya YouTube ili upate habari, taarifa na vidokezo vipya.

Maswali Yanayoulizwa Sana

Ni mara ngapi ninaweza kuwaarifu wanaofuatilia?

  • Watazamaji wanaweza kupokea arifa zisizozidi 3 kutoka kila kituo ndani ya kipindi cha saa 24. Arifa hizi zinajumuisha upakiaji wa video, mitiririko mubashara na maonyesho ya kwanza.
  • Unaweza kutuma tu arifa 1 ya Chapisho la jumuiya ndani ya kipindi cha siku 3.

Kwanini kuna vikomo vya arifa kwenye video mpya?

Arifa zinawasaidia watazamaji kuwafahamu watayarishi wanaowapenda. Watazamaji wanapopata arifa nyingi kupita kiasi, kwa kawaida huzima kabisa arifa, hali inayowaathiri watayarishi wote. Kudhibiti arifa ziwe arifa 3 mpya za video katika kila kituo kwa kipindi cha saa 24 huwasaidia watazamaji kuendelea kutazama maudhui katika YouTube kwa muda mrefu.

Kwa nini baadhi ya wanaofuatilia wanapata arifa saa kadhaa baada ya kuchapisha video yangu?

Arifa zilizowekewa mapendeleo hutumwa kwa wakati unaofaa kwa kila mfuatiliaji mahususi. Mipangilio hii humaanisha kuwa baadhi ya wafuatiliaji ambao arifa zao zimewekwa kuwa “Zilizowekewa Mapendeleo” wanapata arifa saa kadhaa baada ya kuchapisha video yako. Tumeweka muda wa kuwasilisha uwe pale tunapofikiria mfuatiliaji ana uwezekano mkubwa wa kutazama video yako baada ya kuona arifa.
Kwa kawaida, wafuatiliaji wanaochagua kupokea arifa zote huambiwa ndani ya dakika chache baada ya kuchapisha video mpya.

Je, nini maana ya arifa "Zilizowekewa Mapendeleo"?

Maana ya “Zilizowekewa Mapendeleo” hutofautiana kulingana na mtu. Zimewekewa mapendeleo kwa kila mtazamaji kulingana na historia yake ya video alizotazama, wakati anaotazama video kwenye kituo, jinsi video fulani zilivyo maarufu na anapofungua arifa.

Kwa nini YouTube ina mipangilio “Iliyowekewa Mapendeleo”? Kwa nini msitume arifa zote?

Watazamaji wengi hawapendi kupokea arifa zote. Ikiwa wafuatiliaji wanahisi kuchoshwa na idadi ya arifa wanazopokea, wanaweza kuzima arifa kabisa. 
Arifa zilizowekewa mapendeleo husaidia kuzuia watumiaji kuzima arifa zote za kituo chako au za vituo vyote. Husaidia kuwafanya watazamaji kuchangamkia maudhui yako kupitia arifa kwa muda mrefu.
Wafuatiliaji “Mahususi” bado wana thamani kwenye kituo chako. Wafuatiliaji hawa wataona kila video uliyopakia kwenye mipasho yao ya vituo wanavyofuatilia. Mipangilio hii inazitofautisha video zako na mamilioni ya video zingine kwenye YouTube.

Je, arifa za mtiririko mubashara zinafanyaje kazi?

Sawa na upakiaji wa video, arifa za mtiririko wako mubashara hutumwa kwa wafuatiliaji ambao:
  1. Wamewasha “Arifa zote” za kituo chako na
  2. Wamewasha arifa za YouTube kwenye akaunti na vifaa vyao

Ikiwa unatumia programu ya kusimba, arifa hutumwa kwa wafuatiliaji hawa baada ya mtiririko wako mubashara kuwekwa hadharani na tunapotambua kuwa unarusha maudhui Moja kwa Moja. Kwa mfano, ikiwa mtiririko wako mubashara unapatikana hadharani lakini hatujapata uingizaji wa data kwenye programu yako ya kusimba kuwa unatiririsha Mubashara, hatutatuma arifa.

Pata maelezo zaidi kuhusu kutiririsha moja kwa moja kwenye YouTube.

Kwa nini kuna mipangilio mingi ya arifa za watazamaji?

Arifa zinawasaidia watazamaji kuwafahamu watayarishi wanaowapenda. Tunataka kuwapa watazamaji chaguo la kuziwekea mapendeleo arifa zao kulingana na kituo mahususi au kwa ajili ya akaunti za kwa ujumla.
Baadhi ya mipangilio ya arifa iko nje ya udhibiti wa YouTube. Kwa mfano, mipangilio ya kifaa cha mfuatiliaji inaweza kubatilisha YouTube na kuzuia arifa kuwafikia wafuatiliaji.
Je, mipangilio ipi inaweza kuathiri arifa?
Mabadiliko kwenye mipangilio ifuatayo haionekani kwenye ukurasa mahususi wa kituo mahususi.

Kwenye programu au tovuti ya YouTube:

  • Mipangilio ya arifa za akaunti kwenye kompyuta: Kwenye kompyuta, watazamaji wanaweza kudhibiti ikiwa wapokee arifa kwa barua pepe na arifa za kompyuta kwenye YouTube kwa kwenda kwenye Mipangilio kisha Arifa. Wanaweza kuchagua iwapo watapokea arifa kutoka kwenye vituo mahususi kama arifa kwa barua pepe, arifa zote au la.
  • Mipangilio ya arifa za akaunti kwenye kifaa cha mkononi: Kwenye kifaa cha mkononi, watazamaji wanaweza kudhibiti ikiwa wapokee arifa kwa barua pepe na arifa za kompyuta kwenye YouTube kwa kwenda kwenye Mipangilio kisha Arifa.
  • Kidhibiti cha usajili kwenye kompyuta: Wafuatiliaji wanaweza kuzima arifa za vituo mahususi kwenye kidhibiti cha usajili kwenye kompyuta.
  • Mipangilio ya kituo kwenye kifaa cha mkononi: Kwenye kifaa cha mkononi, watazamaji wanaweza kutumia ukurasa wa mipangilio ya Kituo chini ya Mipangilio kisha Arifa kisha Mipangilio ya kituo ili kuzima arifa kwenye vituo mahususi.

Muda uliotumia kifaa chako:

  • Mipangilio ya arifa za kifaa: Kwenye kifaa cha mkononi, watazamaji wanaweza kuzima arifa za YouTube kwenye mipangilio ya vifaa vyao. Mipangilio hii hubatilisha mipangilio ya akaunti na programu ya YouTube.
  • Mipangilio ya arifa za Chrome: Kwenye kompyuta, watumiaji wa Chrome wanaweza kuzima arifa za Chrome kwenye mipangilio yao. Mipangilio hii hubatilisha mipangilio ya YouTube ya arifa za Chrome.
Kwa muhtasari wa mipangilio hii yote, tazama video hii kutoka TeamYouTube.

Kwa nini arifa huzimwa kwenye maudhui “yanayolenga watoto”?

Ili kutii Sheria ya Kulinda Faragha ya Watoto Mtandaoni (COPPA) na sheria zingine, tunaweka mipaka ya ukusanyaji data kwenye maudhui yaliyobainishwa kuwa yanalenga watoto. Vipengele fulani vinaweza kudhibitiwa au kuzimwa kwenye maudhui haya, ikiwa ni pamoja na arifa na wafuatiliaji wako hawataweza kupata arifa kuhusu kituo chako. Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu kuweka hadhira ya kituo au video hapa.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
7946086773850027099
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false