Maswali Yanayoulizwa Sana kuhusu video za YouTube nje ya mtandao

Katika maeneo mahususi, unaweza kupakua video fulani kutoka kwenye programu ya YouTube ya vifaa vya mkononi ili uzicheze nje ya mtandao. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kupakua video ili uzitazame nje ya mtandao.

Vipengele vinavyofafanuliwa kwenye makala haya vinapatikana katika maeneo yaliyoorodheshwa hapa. Iwapo YouTube Premium inapatikana katika eneo uliko, unaweza kupakua video kwenye kompyuta au kifaa chako cha mkononi ukiwa mwanachama wa YouTube Premium. Iwapo wewe ni mwanachama wa YouTube Premium, pata maelezo kuhusu jinsi ya kudhibiti mipangilio yako ya kupakua.

 

Upakuaji wa video unapatikana wapi?

Kutazama video nje ya mtandao kwenye kifaa cha mkononi katika nchi au maeneo mahususi. 

Huenda YouTube isipatikane katika maeneo yote, kwa hivyo huenda isifanye kazi katika maeneo haya. Tunajitahidi kuizindua katika maeneo zaidi na kuleta toleo lililojanibishwa la YouTube kwenye nchi au maeneo zaidi.

Ninawezaje kupakua faili za sauti, muziki, au MP3 kutoka kwenye programu ya YouTube?

Unaweza kupakua faili ya video ya muziki, iwapo inapatikana, kwa kufuata hatua za kupakua video.  

Huwezi kupakua faili za sauti, muziki au MP3 kutoka kwenye programu ya YouTube.

Ninawezaje kupakua video kutoka YouTube niweke kwenye kompyuta yangu?

Unaweza kupakua video ambazo tayari umepakia.

Iwapo hujapakia video mwenyewe, unaweza kuihifadhi kwenye kompyuta. Unaweza kupakua video kutoka kwenye programu ya YouTube na kuziweka kwenye kifaa cha mkononi pekee.

Kwa nini video nilizopakua za YouTube hazipo katika matunzio yangu?

Video huhifadhiwa zikiwa zimesimbwa kwenye kifaa na zinaweza tu kutazamwa katika programu ya YouTube.

Ninawezaje kushiriki video kwenye YouTube?

  1. Gusa Shiriki  chini ya video husika.
  2. Teua chaguo linalofaa la kushiriki.

Je, video hupakuliwa kiotomatiki?

Iwapo umepakua orodha yote ya kucheza, video zinaweza kupakuliwa kiotomatiki. Hata hivyo, ukipakua video mahususi, hupaswi kuona maudhui yanayopakuliwa kiotomatiki.

Inategemea pia mara ya mwisho ulipotumia orodha ya kucheza. Iwapo umetazama video kwenye orodha ya kucheza katika siku 30 zilizopita na video mpya imewekwa kwenye orodha hiyo ya kucheza, video hiyo mpya itapakuliwa kiotomatiki. Iwapo umepakua orodha hiyo ya kucheza katika siku 30 zilizopita, video pia inaweza kupakuliwa kiotomatiki.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
8595459537635381069
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false