Kupakua video za YouTube kwenye kadi ya SD

Ili utazame video nje ya mtandao, ipakue kwenye kadi ya SD (kadi ya hifadhi) au kwenye hifadhi ya ndani ya simu yako. Unaweza kupakua video iwapo:

Ili uhifadhi video za kutazama nje ya mtandao, gusa Pakua Kipengele cha nje ya mtandao kimezimwa kwenye ukurasa wa kutazama video.


Jinsi ya kupakua video kwenye kadi ya SD | Masharti yatatumika

Fuatilia chaneli ya Watazamaji ya YouTube ili upate habari, taarifa na vidokezo vipya.

Kupakua video kwenye kadi ya SD ya simu yako

Iwapo simu yako haina kadi ya SD, isakinishe ili video unazopakua zihifadhiwe hapo.

Kuhifadhi kwenye kadi ya SD kwa chaguomsingi

  1. Gusa picha yako ya wasifu .
  2. Gusa Mipangilio .
  3. Gusa Chinichini na vipakuliwa.
  4. Washa kipengele cha Tumia kadi ya SD (Hifadhi video kwenye kadi ya SD).

Iwapo hutawasha kipengele cha matumizi ya kadi ya SD, video zako zitahifadhiwa kwenye hifadhi ya ndani ya simu.

Hakikisha kuwa kuna nafasi ya kutosha kwenye kadi ya SD ili uhifadhi video yako.

Kupakua video kwenye kadi ya SD

  1. Nenda kwenye video ambayo ungependa kuhifadhi kwenye kadi yako ya SD.
  2. Gusa Pakua Kipengele cha nje ya mtandao kimezimwa chini ya video husika.

Iwapo kifaa chako kitapoteza muunganisho wakati wa kupakua video au orodha ya kucheza, shughuli ya kupakua itaendelea kiotomatiki utakapounganisha tena kwenye intaneti.

Maswali Yanayoulizwa Sana kuhusu Kadi ya SD

Ninawezaje kuhamisha video nilizopakua kwenye hifadhi ya ndani ya simu na kuziweka kwenye kadi ya SD?

Huwezi kuhamisha video moja kwa moja kutoka eneo moja hadi jingine. Ili uhamishe video uliyopakua kutoka hifadhi ya ndani ya simu uiweke kwenye kadi ya SD:

  1. Futa video kwenye hifadhi ya mfumo.
  2. Badilisha eneo la kuhifadhi video liwe SD.
  3. Pakua video tena.

Ninawezaje kuhamisha video nilizopakua kutoka kadi ya SD na kuziweka kwenye hifadhi ya ndani ya simu?

Huwezi kuhamisha video moja kwa moja kutoka eneo moja hadi jingine. Ili uhamishe video uliyopakua kutoka kwenye kadi ya SD uiweke kwenye hifadhi ya ndani ya simu:
  1. Futa video husika kwenye kadi yako ya SD.
  2. Badilisha eneo la kuhifadhi video liwe hifadhi ya ndani ya simu.
  3. Pakua video tena.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
2083508385146486192
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false