Baadhi ya watangazaji na wamiliki wa maudhui hutaka kuelewa utendaji wa maudhui yao kwenye YouTube na YouTube TV.
Ili kutoa maelezo haya, YouTube hushirikiana na Nielsen ili kupima utendaji wa maudhui. Utafiti wa Nielsen wa masoko ya TV hupima mwenendo wako wa utazamaji.
- Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi maelezo haya hukusanywa na kutumika au ubadilishe mapendeleo yako kwenye tovuti ya Nielsen.
- Pata maelezo kuhusu jinsi matumizi hupimwa na sera ya faragha inayolingana katika Sheria na Masharti ya Huduma za YouTube Zinazolipiwa.
Fuata hatua zilizo hapa chini ili ujiondoe au uangalie hali yako ya kujiondoa, kulingana na sera na tovuti ya Nielsen:
Unaweza kujiondoa kwenye mapendeleo ya matangazo ndani ya ukurasa wa mipangilio wa kifaa chako cha Android. Ili ujiondoe, gusa Mipangilio Google Matangazo Jiondoe kwenye uwekaji wa Mapendeleo ya Matangazo.
Mara tu ukijiondoa, data yako ya demografia ya watazamaji haitajumuishwa tena kwenye upimaji wa utendaji wa TV unaofanywa na Nielsen. Tunaweza kuwasiliana na Nielsen mara kwa mara ili tuthibitishe hali ya kujiondoa kwa mwanachama.
Vifaa vya TV
Unaweza kujiondoa ili matangazo yako yasiwekewe mapendeleo kwa kutembelea Mipangilio ya Matangazo kutoka Google.