Kuongeza vijipicha vya video kwenye YouTube

Vijipicha vya video huruhusu hadhira yako kuona muhtasari wa haraka wa video yako. Unaweza kuchagua vijipicha vilivyozalishwa kiotomatiki kwenye YouTube au unaweza kupakia vyako mwenyewe ikiwa akaunti yako imethibitishwa. Hakikisha kuwa kijipicha chako kinafuata Mwongozo wetu wa Jumuiya.

Kuweka vijipicha maalum au vya kiotomatiki

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui.
  3. Bofya video ambayo ungependa kuhariri.
  4. Chagua kijipicha kilichozalishwa kiotomatiki au uguse pakia Kijipicha ili ubuni kijipicha maalum cha video kutoka kwenye picha katika kifaa chako.
  5. Bofya HIFADHI.
Dokezo: Huenda ikachukua muda kabla ya mabadiliko ya kijipicha chako kuonekana kwenye YouTube.

Tazama jinsi ya kuweka kijipicha maalum cha video

Tazama video ifuatayo kwenye chaneli ya Watayarishi wa Maudhui ya YouTube ikiwa ungependa mafunzo kuhusu kuweka kijipicha maalum cha video kwenye YouTube.

How to Add Custom Thumbnails to Your YouTube Videos

Pata vidokezo vya watayarishi kuhusu vijipicha vya video.

Desturi bora kuhusu vijipicha maalum

 

Ukubwa na ubora wa picha

Kijipicha chako maalum kinapaswa kuwa kikubwa kadri iwezekanavyo. Kitatumika kama picha ya onyesho tangulizi katika kichezaji kilichopachikwa. Tunapendekeza yafuatayo kuhusu vijipicha vyako maalum:

  • Viwe na ubora wa 1280x720 (na upana wa angalau pikseli 640).
  • Uvipakie katika miundo ya picha kama vile JPG, GIF, au PNG.
  • Viwe chini ya MB 2 kwa video au MB 10 kwa podikasti.
  • Jaribu kutumia uwiano wa 16:9 kwa kuwa ndio unaotumika zaidi katika vichezaji na maonyesho tangulizi kwenye YouTube.
  • Kwa orodha za kucheza za podikasti, pakia kijipicha kilicho na uwiano wa 1:1 badala ya 16:9 (pikseli 1280 x 1280).

Sera kuhusu vijipicha

Vijipicha vyote maalum sharti vizingatie Mwongozo wetu wa Jumuiya. Huenda vijipicha vyako vikakataliwa na akaunti yako ikapokea onyo ikiwa kijipicha kina:
  • Maudhui ya uchi au yanayochochea ngono
  • Matamshi ya Chuki
  • Vurugu
  • Maudhui yenye madhara au hatari
Ukiukaji unaojirudia unaweza kusababisha kuondolewa kwa ruhusa yako ya kutumia vijipicha maalum kwa siku 30 au hata kufungwa kwa akaunti. Pata maelezo zaidi kuhusu kupewa onyo kwa Kukiuka Mwongozo wa Jumuiya.
Ukipewa onyo, utaarifiwa kupitia barua pepe na utaona arifa katika Mipangilio ya Kituo chako utakapoingia tena katika akaunti kwenye YouTube. Unaweza kukata rufaa dhidi ya onyo iwapo unaamini vijipicha vyako havikiuki Mwongozo wa Jumuiya ya YouTube. Rufaa yako ikikubaliwa na bado hujaweka kijipicha kingine, huenda tukakirejesha.

Vikomo vya vijipicha maalum

Kuna kikomo cha idadi ya vijipicha maalum ambavyo chaneli inaweza kupakia kila siku. Ukiona hitilafu inayosema “Umefikisha kikomo cha kila siku cha vijipicha maalum” unapojaribu kupakia kijipicha, jaribu tena baada ya saa 24. 
Vikomo vinaweza kutofautiana kulingana na nchi au eneo au historia ya chaneli. Maonyo ya hakimiliki yanaweza kuathiri historia ya chaneli kutimiza masharti. Maonyo kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya yataathiri idadi ya vijipicha maalum unavyoweza kupakia.
Kumbuka: Huwezi kupakia kijipicha maalum kwenye Video Fupi kama unavyoweza kufanya katika video ndefu. Unaweza kuchagua fremu kutoka kwenye Video yako fupi ili kutumia kama kijipicha kinachoonekana katika matokeo ya utafutaji, alama ya reli na kurasa viini za sauti pamoja na ukurasa wa chaneli yako. Baada ya kuchagua, huwezi kubadilisha kijipicha baada ya kupakia video.

Je, kwa nini kipengele changu cha vijipicha maalum kimezimwa?

YouTube inaweza kuzima vijipicha maalum katika matokeo fulani ya utafutaji vinapobainishwa kuwa havifai kwa watazamaji.
Vijipicha vyote maalum sharti vizingatie Mwongozo wetu wa Jumuiya.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
2118412415780963300
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false