Zinazovuma kwenye YouTube

Kipengele cha zinazovuma huwasaidia watazamaji kuona kinachoendelea kwenye YouTube na ulimwenguni. Kipengele cha zinazovuma hulenga kuonyesha video na Video Fupi zinazowavutia watazamaji wengi. Baadhi ya maudhui yanayovuma yanaweza kutabirika, kama vile wimbo mpya wa msanii maarufu au kionjo cha filamu mpya. Mengine ni ya kushangaza, kama vile video inayovuma.

Kipengele cha zinazovuma hakijawekewa mapendeleo na huonyesha orodha ile ile ya video zinazovuma kwa watazamaji wote katika nchi moja, ndiyo maana huenda ukaona video na Video Fupi katika kipengele cha Zinazovuma ambazo zina lugha tofauti na inayotumika kwenye kivinjari chako. Hata hivyo, nchini India, kipengele cha Zinazovuma huonyesha matokeo kwa kila mojawapo ya lugha 9 za Kihindi zinazozungumzwa sana na wakaazi.

Katika nchi fulani, huenda Video Fupi maarufu zikaangaziwa kwenye rafu au kichupo ndani ya ukurasa wa zinazovuma au unaweza kuona Video Fupi zimeorodheshwa kama Zinazovuma kwenye mipasho yako au katika kurasa viini. 

Orodha ya video zinazovuma husasishwa takribani kila baada ya dakika 15. Kila mara orodha inaposasishwa, video inaweza kusonga juu, chini, au kusalia ilipo kwenye orodha.

Je, nini hupelekea video kuorodheshwa kwenye Zinazovuma?

Kati ya video nyingi nzuri mpya kwenye YouTube siku yoyote ile, Zinazovuma inaweza kuonyesha video chache tu. Zinazovuma inalenga kuonyesha video ambazo:

Zinazovuma inalenga kuzingatia vigezo hivi vyote kwa usawa. Ili kutimiza hili, Zinazovuma huzingatia viashirio vingi, ikijumuisha, (lakini siyo tu):

  • Mara ilizotazamwa
  • Kasi ya video kutazamwa (yaani “umaarufu”)
  • Watazamaji waliko, ikijumuisha nje ya YouTube
  • Muda wa video kwenye YouTube baada ya kupakiwa
  • Utendaji wa video ikilinganishwa na video zingine zilizopakiwa majuzi kwenye kituo hicho

Tunazingatia viashirio hivi vyote kupata orodha ya video zinazoangazia kinachoendelea kwenye YouTube, zenye kuwafaa watazamaji wetu na zinazodhihirisha hali ya maudhui kwenye mfumo wetu. Hii inamaanisha kuwa video inayotazamwa zaidi siku yoyote ile huenda isiwe nambari 1 katika Zinazovuma, na video zilizotazamwa mara chache huenda zikawa juu ya zile ambazo zimetazamwa zaidi.

Tumemakinika kabisa kuhusu usalama wa video Zinazovuma, hivyo tuna vichujio ili kuhakikisha hatuonyeshi video zenye lugha chafu iliyokithiri, maudhui ya watu wazima, au vurugu, au video ambazo hazifai, kama vile zinazowadhalilisha wengine kwenye jumuiya. Nchini Marekani na kwingineko, tuna wahudumu wanaochuja maudhui ili kuhakikisha video tunazoonyesha zinafaa na ni usalama.

YouTube haikubali malipo ili kuorodhesha maudhui katika Zinazovuma na haipendelei watayarishi wowote. Tunapochagua video Zinazovuma, hatutumii kigezo cha mara ambazo video imetazamwa katika Matangazo ya YouTube. Katika masoko mengi makuu, tunahakikisha kuwa angalau nusu ya video zinazovuma ni za watayarishi ambao huchapisha sana maudhi kwenye YouTube.

Mipangilio ya faragha ya video zinazovuma

Video inaweza tu kuonekana kwenye kichupo cha Zinazovuma iwapo mipangilio yake ya faragha imewekwa kuwa ya umma. Baadhi ya video huenda zisionekane kwenye ukurasa wa zinazovuma ikiwa Hali yenye mipaka imewashwa. Pata maelezo zaidi kuhusu Hali yenye mipaka hapa

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
13973553615926128547
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false