Anza kutumia YouTube VR

Programu ya YouTube VR inakuruhusu upate na utazame video zinazozunguka digrii 360 na maudhui ya uhalisia pepe kwa urahisi kupitia vifaa na vifaa fulani vya sauti.

Kuingia katika akaunti

YouTube VR inaruhusu hali ya utumiaji ukiwa umeingia katika akaunti, inayokupa uwezo wa kufikia manufaa kadhaa, kama vile kuona vituo unavyofuatilia.

Kuingia katika akaunti

  1. Kwenye skrini ya kwanza, chagua aikoni ya Akaunti na Mipangilio.
  2. Bofya Ingia katika Akaunti.
  3. Utaona msimbo wa kuanza kutumia.
  4. Kwenye kompyuta au kifaa chako cha mkononi, nenda kwenye https://youtube.com/activate.
  5. Weka msimbo wa kuanza kutumia.
  6. Ingia katika akaunti unapoulizwa. Iwapo una Akaunti kadhaa za Google, chagua akaunti unayotumia kwenye YouTube. Iwapo tayari umeingia katika akaunti, nenda kwenye hatua inayofuata.
  7. Ukishaingia, utaingia kiotomatiki kwenye akaunti katika kifaa chako.
Kumbuka: Katika Hatua ya 3, baadhi ya mifumo itakuruhusu unakili msimbo kwenye ubao wa kunakili, kisha ufungue mfumo wa kivinjari ili uweke msimbo. Shikilia kianzishi kwa muda mrefu ili ubandike msimbo kwenye sehemu.
Kumbuka: Akaunti za Biashara hazitumiki kwa sasa.

Kuondoka kwenye akaunti

  1. Kwenye skrini ya kwanza, chagua aikoni ya Akaunti na Mipangilio.
  2. Chagua akaunti ambayo ungependa kuondoka.
  3. Bofya Ondoka katika akaunti.

Vinjari video

Unaweza kuvinjari video kwenye Skrini ya kwanza au katika orodha za kucheza kwa kwenda juu na chini kwenye padi ya kugusa. Unaweza kufikia Skrini ya kwanza wakati wowote kwa kuchagua nembo ya YouTube.

Kutafuta video

Unaweza kutafuta video katika YouTube VR kwa njia mbili: Kutafuta kwa Kutamka au utafutaji wa kibodi. Utafutaji unapatikana katika Menyu ya vidhibiti vya kichezaji au kwenye Skrini ya kwanza.

Kutafuta kwa Kutamka

  1. Bofya Tafuta Tafuta .
  2. Chagua aikoni ya Maikrofoni.
  3. Sema hoja yako ya utafutaji kwa sauti.


Utafutaji wa kibodi

  1. Bofya Tafuta Tafuta .
  2. Weka hoja yako ya utafutaji ukitumia kibodi.

Unaweza kuchuja matokeo yako ya utafutaji kwa kuchagua kutoka chaguo moja au zaidi zifuatazo: 360°, VR180, 4K, 3D na CC.

Vidhibiti vya kichezaji

Unapocheza video, bofya popote kwenye skrini.

Vidhibiti vya kichezaji vinakuruhusu ufanye vitendo vingi ikiwa ni pamoja na:

  • Kucheza/kusitisha video.
  • Kuongeza au kupunguza sauti.
  • Kuenda kwenye video ya awali.
  • Kuenda kwenye video inayofuata.
  • Kubadilisha mipangilio ya utazamaji.

Kuwasha au kuzima manukuu

  1. Bofya Mipangilio Settings .
  2. Bofya Manukuu.
  3. Chagua lugha unayopendelea.

Badilisha ubora wa video

  1. Bofya Mipangilio Settings .
  2. Bofya Ubora.
  3. Chagua ubora unaopenda wa video.

Washa au uzime Skrini iliyopinda (kwa matangazo na video ambazo hazizunguki digrii 360)

  1. Bofya Mipangilio Settings .
  2. Chagua Skrini iliyopinda kisha Uwashe au Uzime.

Ili uondoe vidhibiti vya kichezaji, bofya popote kwenye video au subiri hadi vitakapoondolewa kiomatiki.

Kuweka upya mwonekano wako katikati

Unaweza kuona kuwa kiteuzi au mwonekano unaenda upande mmoja. Kiteuzi na mwonekano vinaweza kurejeshwa katikati kwa haraka kwa kutumia kidhibiti.
  1. Lenga kidhibiti mbele.
  2. Shikilia Kitufe cha ukurasa wa mwanzo kwenye kidhibiti chako.

Kuripoti video, chaneli na maudhui mengine ambayo hayafai

Ikiwa unatumia kifaa cha VR, unaweza kufuata maagizo yaliyo hapa chini ili uripoti maudhui yasiyofaa moja kwa moja kutoka kwenye programu ya YouTube VR.

Kuripoti video

YouTube hukagua video zilizoripotiwa saa 24 kwa siku, siku 7 za wiki. Video inaweza kuripotiwa wakati wowote baada ya kupakiwa kwenye YouTube. Ikiwa timu yetu ya ukaguzi haitapata ukiukaji wowote, video itasalia katika hali ya kupakiwa na ripoti za ziada hazitabadilisha hali yake.
Ili uripoti video:
  1. Fungua programu ya YouTube .
  2. Nenda kwenye video ambayo ungependa kuiripoti.
  3. Bonyeza kianzishi (au ubane ikiwa unatumia mikono) ili uonyeshe sehemu ya kucheza.
  4. Katika upande wa kulia wa sehemu ya kucheza, chagua Mipangilio  kisha Ripoti .
  5. Chagua sababu inayoeleza vyema zaidi ukiukaji ulio kwenye video.
  6. Thibitisha kuwa ungependa kutuma kwa kuchagua Sawa.

Kumbuka: Ili uangalie hali ya video uliyoripoti, kwenye kompyuta, tembelea ukurasa wako wa Historia ya Kuripoti. Pata maelezo zaidi kuhusu Historia yako ya Kuripoti.

Kuripoti Video fupi

YouTube hukagua video zilizoripotiwa saa 24 kwa siku, siku 7 za wiki. Video inaweza kuripotiwa wakati wowote baada ya kupakiwa kwenye YouTube. Ikiwa timu yetu ya ukaguzi haitapata ukiukaji wowote, video itasalia katika hali ya kupakiwa na ripoti za ziada hazitabadilisha hali yake.
Unaweza kuripoti Video Fupi za YouTube kutoka kwenye Kichezaji cha Video Fupi:
  1. Ingia katika akaunti kwenye YouTube.
  2. Nenda kwenye Video fupi ambayo ungependa kuiripoti.
  3. Bonyeza kianzishi (au ubane ikiwa unatumia mikono) ili uonyeshe sehemu ya kucheza.
  4. Katika upande wa kulia wa sehemu ya kucheza, chagua Mipangilio  kisha Ripoti .
  5. Chagua sababu inayoeleza vyema zaidi ukiukaji ulio kwenye video.
  6. Thibitisha kuwa ungependa kutuma kwa kuchagua Sawa.

Kumbuka: Ili uangalie hali ya video unayoripoti, kwenye kompyuta, tembelea ukurasa wako wa Historia ya Kuripoti. Pata maelezo zaidi kuhusu Historia ya Kuripoti.

Kuripoti chaneli

Unaweza kuripoti watumiaji, picha za mandharinyuma zisizofaa au avata za wasifu zisizofaa. Ili uripoti chaneli:
  1. Fungua programu ya YouTube .
  2. Nenda kwenye ukurasa wa chaneli ambayo ungependa kuripoti.
  3. Katika sehemu ya juu kulia, chagua Zaidi '' kisha Ripoti mtumiaji .
  4. Chagua sababu inayoeleza vyema zaidi ukiukaji ulio kwenye chaneli.
  5. Chagua Ripoti.
    • Si lazima: Dirisha litakalofunguka linaweza kukuomba uweke maelezo zaidi. Weka maelezo mengine yoyote ambayo ungependa kutuma.

Kumbuka: Unaporipoti chaneli, hatukagui video za chaneli. Tunatumia video ambazo huenda umeambatisha kwenye ripoti yako ili tuelewe zaidi kuhusu chaneli, lakini hatukagui video ili kubaini ukiukaji. Vipengele vya chaneli ambavyo tunakagua vinajumuisha, lakini si tu, picha ya wasifu, utambulisho na maelezo ya chaneli. Ikiwa unafikiri kuwa video mahususi za chaneli zinakiuka sera zetu, unapaswa kuripoti video hizo mahususi.

Kuripoti orodha ya video

Unaweza kuripoti orodha ya video ikiwa maudhui, jina, maelezo au lebo zake zinakiuka Mwongozo wetu wa Jumuiya:
  1. Fungua programu ya YouTube .
  2. Nenda kwenye orodha ya video ambayo ungependa kuiripoti.
  3. Kwenye sehemu ya kulia ya kitufe cha “Cheza zote”, chagua Zaidi ''  kisha Ripoti     kisha Ripoti.

Kuripoti kijipicha

Unaweza kuripoti kijipicha cha video kinachokiuka Mwongozo wetu wa Jumuiya:
  1. Fungua programu ya YouTube .
  2. Nenda kwenye video ambayo ungependa kuripoti katika ukurasa wako wa kwanza, kwenye video unazopendekezewa au katika matokeo ya utafutaji. Huwezi kuripoti kijipicha kwenye ukurasa wa kutazama wa video.
  3. Katika kona ya juu kulia ya kijipicha, chagua Zaidi  '' kisha Ripoti .
  4. Chagua sababu inayoeleza vyema zaidi kwa nini ungependa kuripoti kijipicha.
  5. Chagua Ripoti.

Kuripoti maoni

Unaweza kuripoti maoni yanayokiuka Mwongozo wetu wa Jumuiya:
  1. Ingia katika akaunti kwenye YouTube.
  2. Nenda kwenye maoni ambayo ungependa kuyaripoti.
  3. Chagua Zaidi  '' kisha Ripoti .
  4. Chagua sera ambayo maoni haya yanakiuka.
  5. Thibitisha kuwa ungependa kutuma kwa kuchagua Sawa.
    • Si lazima: Kama mtayarishi, baada ya kuripoti maoni, unaweza kuzuia maoni ya mtumiaji huyo yasionyeshwe kwenye chaneli yako. Teua kisanduku kilicho karibu na Ficha mtumiaji kwenye chaneli yangu kisha chagua Sawa.

Maoni yangu yamewekewa alama kuwa ni taka kimakosa

Iwapo unaamini kuwa maoni yako yaliwekewa alama kuwa ni taka kimakosa, unaweza kuwasiliana na aliyepakia kisha umwombe arejeshe maoni yako.

Kuripoti tangazo

Iwapo utapata tangazo lisilofaa au linalokiuka Sera za Google Ads, unaweza kuliripoti. Jaza fomu hii kisha uitume.
Ili uripoti tangazo kutoka kwenye video:
  1. Katika sehemu ya chini ya tangazo, chagua 'Kwa nini unaonyeshwa tangazo hili?' .
  2. Chagua Ripoti tangazo .
  3. Jaza fomu kisha uitume. Timu yetu itakagua ripoti yako ya tangazo na itachukua hatua ikiwa inafaa.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
7794763609961654142
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false