Programu ya YouTube VR inakuruhusu upate na utazame video zinazozunguka digrii 360 na maudhui ya uhalisia pepe kwa urahisi kupitia vifaa na vifaa fulani vya sauti.
Kuingia katika akaunti
Kuingia katika akaunti
- Kwenye skrini ya kwanza, chagua aikoni ya Akaunti na Mipangilio.
- Bofya Ingia katika Akaunti.
- Utaona msimbo wa kuanza kutumia.
- Kwenye kompyuta au kifaa chako cha mkononi, nenda kwenye https://youtube.com/activate.
- Weka msimbo wa kuanza kutumia.
- Ingia katika akaunti unapoulizwa. Iwapo una Akaunti kadhaa za Google, chagua akaunti unayotumia kwenye YouTube. Iwapo tayari umeingia katika akaunti, nenda kwenye hatua inayofuata.
- Ukishaingia, utaingia kiotomatiki kwenye akaunti katika kifaa chako.
Kuondoka kwenye akaunti
- Kwenye skrini ya kwanza, chagua aikoni ya Akaunti na Mipangilio.
- Chagua akaunti ambayo ungependa kuondoka.
- Bofya Ondoka katika akaunti.
Vinjari video
Kutafuta video
Kutafuta kwa Kutamka
- Bofya Tafuta .
- Chagua aikoni ya Maikrofoni.
- Sema hoja yako ya utafutaji kwa sauti.
Utafutaji wa kibodi
- Bofya Tafuta .
- Weka hoja yako ya utafutaji ukitumia kibodi.
Unaweza kuchuja matokeo yako ya utafutaji kwa kuchagua kutoka chaguo moja au zaidi zifuatazo: 360°, VR180, 4K, 3D na CC.
Vidhibiti vya kichezaji
Unapocheza video, bofya popote kwenye skrini.
Vidhibiti vya kichezaji vinakuruhusu ufanye vitendo vingi ikiwa ni pamoja na:
- Kucheza/kusitisha video.
- Kuongeza au kupunguza sauti.
- Kuenda kwenye video ya awali.
- Kuenda kwenye video inayofuata.
- Kubadilisha mipangilio ya utazamaji.
Kuwasha au kuzima manukuu
- Bofya Mipangilio .
- Bofya Manukuu.
- Chagua lugha unayopendelea.
Badilisha ubora wa video
- Bofya Mipangilio .
- Bofya Ubora.
- Chagua ubora unaopenda wa video.
Washa au uzime Skrini iliyopinda (kwa matangazo na video ambazo hazizunguki digrii 360)
- Bofya Mipangilio .
- Chagua Skrini iliyopinda kisha Uwashe au Uzime.
Ili uondoe vidhibiti vya kichezaji, bofya popote kwenye video au subiri hadi vitakapoondolewa kiomatiki.
Kuweka upya mwonekano wako katikati
- Lenga kidhibiti mbele.
- Shikilia Kitufe cha ukurasa wa mwanzo kwenye kidhibiti chako.
Kuripoti video, chaneli na maudhui mengine ambayo hayafai
Ikiwa unatumia kifaa cha VR, unaweza kufuata maagizo yaliyo hapa chini ili uripoti maudhui yasiyofaa moja kwa moja kutoka kwenye programu ya YouTube VR.
Kuripoti video
- Fungua programu ya YouTube .
- Nenda kwenye video ambayo ungependa kuiripoti.
- Bonyeza kianzishi (au ubane ikiwa unatumia mikono) ili uonyeshe sehemu ya kucheza.
- Katika upande wa kulia wa sehemu ya kucheza, chagua Mipangilio Ripoti .
- Chagua sababu inayoeleza vyema zaidi ukiukaji ulio kwenye video.
- Thibitisha kuwa ungependa kutuma kwa kuchagua Sawa.
Kumbuka: Ili uangalie hali ya video uliyoripoti, kwenye kompyuta, tembelea ukurasa wako wa Historia ya Kuripoti. Pata maelezo zaidi kuhusu Historia yako ya Kuripoti.
Kuripoti Video fupi
- Ingia katika akaunti kwenye YouTube.
- Nenda kwenye Video fupi ambayo ungependa kuiripoti.
- Bonyeza kianzishi (au ubane ikiwa unatumia mikono) ili uonyeshe sehemu ya kucheza.
- Katika upande wa kulia wa sehemu ya kucheza, chagua Mipangilio Ripoti .
- Chagua sababu inayoeleza vyema zaidi ukiukaji ulio kwenye video.
- Thibitisha kuwa ungependa kutuma kwa kuchagua Sawa.
Kumbuka: Ili uangalie hali ya video unayoripoti, kwenye kompyuta, tembelea ukurasa wako wa Historia ya Kuripoti. Pata maelezo zaidi kuhusu Historia ya Kuripoti.
Kuripoti chaneli
- Fungua programu ya YouTube .
- Nenda kwenye ukurasa wa chaneli ambayo ungependa kuripoti.
- Katika sehemu ya juu kulia, chagua Zaidi Ripoti mtumiaji .
- Chagua sababu inayoeleza vyema zaidi ukiukaji ulio kwenye chaneli.
- Chagua Ripoti.
- Si lazima: Dirisha litakalofunguka linaweza kukuomba uweke maelezo zaidi. Weka maelezo mengine yoyote ambayo ungependa kutuma.
Kumbuka: Unaporipoti chaneli, hatukagui video za chaneli. Tunatumia video ambazo huenda umeambatisha kwenye ripoti yako ili tuelewe zaidi kuhusu chaneli, lakini hatukagui video ili kubaini ukiukaji. Vipengele vya chaneli ambavyo tunakagua vinajumuisha, lakini si tu, picha ya wasifu, utambulisho na maelezo ya chaneli. Ikiwa unafikiri kuwa video mahususi za chaneli zinakiuka sera zetu, unapaswa kuripoti video hizo mahususi.
Kuripoti orodha ya video
- Fungua programu ya YouTube .
- Nenda kwenye orodha ya video ambayo ungependa kuiripoti.
- Kwenye sehemu ya kulia ya kitufe cha “Cheza zote”, chagua Zaidi Ripoti Ripoti.
Kuripoti kijipicha
- Fungua programu ya YouTube .
- Nenda kwenye video ambayo ungependa kuripoti katika ukurasa wako wa kwanza, kwenye video unazopendekezewa au katika matokeo ya utafutaji. Huwezi kuripoti kijipicha kwenye ukurasa wa kutazama wa video.
- Katika kona ya juu kulia ya kijipicha, chagua Zaidi Ripoti .
- Chagua sababu inayoeleza vyema zaidi kwa nini ungependa kuripoti kijipicha.
- Chagua Ripoti.
Kuripoti maoni
- Ingia katika akaunti kwenye YouTube.
- Nenda kwenye maoni ambayo ungependa kuyaripoti.
- Chagua Zaidi Ripoti .
- Chagua sera ambayo maoni haya yanakiuka.
- Thibitisha kuwa ungependa kutuma kwa kuchagua Sawa.
- Si lazima: Kama mtayarishi, baada ya kuripoti maoni, unaweza kuzuia maoni ya mtumiaji huyo yasionyeshwe kwenye chaneli yako. Teua kisanduku kilicho karibu na Ficha mtumiaji kwenye chaneli yangu chagua Sawa.
Maoni yangu yamewekewa alama kuwa ni taka kimakosa
Iwapo unaamini kuwa maoni yako yaliwekewa alama kuwa ni taka kimakosa, unaweza kuwasiliana na aliyepakia kisha umwombe arejeshe maoni yako.
Kuripoti tangazo
- Katika sehemu ya chini ya tangazo, chagua 'Kwa nini unaonyeshwa tangazo hili?' .
- Chagua Ripoti tangazo .
- Jaza fomu kisha uitume. Timu yetu itakagua ripoti yako ya tangazo na itachukua hatua ikiwa inafaa.