Vipindi vya malipo kwenye AdSense

Tunakuletea toleo jipya la beta linaloleta maelezo ya malipo kwenye kichupo cha 'Chuma mapato' cha programu ya vifaa vya mkononi ya Studio ya YouTube. Toleo hili la beta litawapatia watayarishi wanaostahiki mbinu rahisi ya kuelewa jinsi mapato yao yanavyobadilika kuwa malipo. Kwa kutumia toleo hili la beta, unaweza kuangalia:
  • Hatua ulizopiga kuelekea malipo yako yanayofuata
  • Historia yako ya malipo ya miezi 12 iliyopita ikijumuisha tarehe, kiasi ulicholipa na uainishaji wa malipo
Pata maelezo zaidi kwenye chapisho letu la jukwaa .

Kipindi cha malipo kwenye AdSense ni kila mwezi. Utafikisha mapato yaliyokadiriwa katika kipindi cha mwezi mmoja, kisha mwanzoni mwa mwezi unaofuata mapato yako yatakamilishwa na kuchapishwa kwenye salio lako katika ukurasa wako wa Malipo. Ikiwa salio lako linazidi kima cha malipo na huna malipo yoyote yaliyoahirishwa, utatumiwa malipo kati ya tarehe 21 na 26 ya mwezi husika. Kumbuka kwamba wakati halisi utakapopokea malipo yako utategemea saa za eneo uliko, iwapo tarehe 21 itakuwa wikiendi au sikukuu na njia ya malipo uliyoichagua.

Note: If you have separate payments accounts for AdSense and YouTube, each payments account needs to reach the payment threshold to be paid out.
Note: Finalized YouTube earnings for the previous month are added to your YouTube payments account balance in AdSense between the 7th and 12th of the month. For example, if you’re in the United States and you earn $100 in June, you'll find this balance in your AdSense for YouTube homepage between July 7th-12th. To learn more about receiving earnings through the YouTube Partner Program, see the YouTube partner earnings overview.

Kufuatilia utaratibu wa malipo yako

Ukurasa wako wa Malipo husasishwa ili kuonyesha utaratibu wa malipo yako. Utaona vipengee vinavyowekwa na kusasishwa mwezi mzima huku mapato yako yakikamilishwa na malipo yako kutumwa. Huenda pia ukaona vipengee vingine vya salio na malipo mbalimbali. Bofya njia yako ya malipo hapo chini ili uangalie ratiba yako ya malipo iliyowekewa mapendeleo.

Panua yote  Kunja yote

Mfumo wa Malipo wa Kielektroniki (EFT)
An example of an AdSense payments calendar
  • Tarehe 3: Makadirio ya mapato yako ya mwezi uliotangulia hukamilishwa na kuchapishwa kwenye ukurasa wako wa Malipo. Kwenye ukurasa wako wa Malipo, utaona kipengee kilicho na jumla ya mapato yako kikiwa kimeongezwa kwenye miamala ya mwezi uliotangulia.

    Ukurasa wako wa Malipo utaonyesha pia makato yoyote yanayohusiana na marekebisho au ada. Kumbuka kwamba huenda usione vipengee vya makato ya shughuli isiyo sahihi yaliyofanywa wakati wa mchakato wa kukamilisha. Pata maelezo zaidi kuhusu makato ya shughuli isiyo sahihi.

  • Tarehe 20: Ni lazima mabadiliko kwenye maelezo ya malipo (ikiwa ni pamoja na kuondoa malipo yaliyoahirishwa) yakamilishwe mnamo tarehe 20 au kabla ya tarehe hiyo. Mabadiliko yanayofanywa baada ya tarehe 20 ya mwezi wowote hayatatekelezwa hadi kipindi cha malipo cha mwezi unaofuata.

    Ni lazima jumla ya salio lako la tarehe 20 lifikie kima cha malipo. Ikiwa salio lako halifikishi kima cha malipo au ikiwa una malipo yaliyoahirishwa, hutalipwa mwezi huo na salio lako litasogezwa mwezi unaofuata.

  • Tarehe 21-26: Kati ya tarehe 21 na 26 ya mwezi, utaona mstari wa "Malipo yanasubiri kushughulikiwa" kwenye ukurasa wa Malipo, kuashiria kuwa mapato yamechakatwa na kutumwa kwenye benki unayoitumia. 

Utapokea malipo yako ndani ya hadi siku saba za kazi baada ya kutumwa. Ikiwa hujayapokea kufikia mwisho wa mwezi, fuatilia na benki yako.

Kumbuka: Tarehe 21 ikiwa wikiendi au sikukuu, malipo yanaweza kutumwa siku ya kwanza ya kazi inayofuata tarehe 21 ya mwezi huo.

Cheki

Malipo ya cheki ya mapato yako ya mwezi uliotangulia hufanywa kati ya tarehe 21 na 26 ya mwezi na yanaweza kuchukua hadi wiki nne kufika kwenye anwani yako ya malipo.

  • Tarehe 3: Makadirio ya mapato yako ya mwezi uliotangulia hukamilishwa na kuchapishwa kwenye ukurasa wako wa Malipo.
  • Tarehe 20: Ni lazima mabadiliko kwenye maelezo ya malipo (ikiwa ni pamoja na kuondoa malipo yaliyoahirishwa) yakamilishwe mnamo tarehe 20 au kabla ya tarehe hiyo. Mabadiliko yanayofanywa baada ya tarehe 20 ya mwezi wowote hayatatekelezwa hadi kipindi cha malipo cha mwezi unaofuata. Pia, ni lazima jumla ya salio lako la tarehe 20 lifikie kima cha malipo. Ikiwa salio lako halifikishi kima cha malipo au ikiwa una malipo yaliyoahirishwa, hutalipwa mwezi huo na salio lako litasogezwa mwezi unaofuata.
  • Tarehe 21 hadi 26: Cheki za akaunti zinazotimiza masharti hutumwa kwa njia ya barua. Kipengee cha "Malipo yanasubiri kushughulikiwa" huonekana kwenye ukurasa wako wa Malipo.

Subiri wiki mbili hadi nne ili cheki yako ifike kwenye kisanduku chako cha barua. Nyakati za kuwasili zinaweza kutofautiana kulingana na huduma ya posta ya eneo lako.

Malipo ya Haraka ya Western Union

Malipo ya Haraka ya Western Union hutumwa kati ya tarehe 21 na 26 ya mwezi na yatapatikana katika eneo lolote la Western Union katika nchi unakoishi siku moja ya kazi baada ya kutumwa.

  • Tarehe 3: Makadirio ya mapato yako ya mwezi uliotangulia hukamilishwa na kuchapishwa kwenye ukurasa wako wa Malipo.
  • Tarehe 20: Ni lazima mabadiliko kwenye maelezo ya malipo (ikiwa ni pamoja na kuondoa malipo yaliyoahirishwa) yakamilishwe mnamo tarehe 20 au kabla ya tarehe hiyo. Mabadiliko yanayofanywa baada ya tarehe 20 ya mwezi wowote hayatatekelezwa hadi kipindi cha malipo cha mwezi unaofuata. Pia, ni lazima jumla ya salio lako la tarehe 20 lifikie kima cha malipo. Ikiwa salio lako halifikishi kima cha malipo au ikiwa una malipo yaliyoahirishwa, hutalipwa mwezi huo na salio lako litasogezwa mwezi unaofuata.
  • Tarehe 21 hadi 26: Malipo hutumwa kwenye Western Union. Kipengee cha "Malipo yanasubiri kushughulikiwa" huonekana kwenye ukurasa wako wa Malipo.

Ni lazima uchukue malipo yako ndani ya siku 60 baada ya kutumwa, la sivyo, kiasi hicho kitarejeshwa kwenye akaunti yako ya AdSense.

Hawala ya fedha ya kielektroniki
  • Tarehe 3: Makadirio ya mapato yako ya mwezi uliotangulia hukamilishwa na kuchapishwa kwenye ukurasa wako wa Malipo.
  • Tarehe 20: Ni lazima mabadiliko kwenye maelezo ya malipo (ikiwa ni pamoja na kuondoa malipo yaliyoahirishwa) yakamilishwe mnamo tarehe 20 au kabla ya tarehe hiyo. Mabadiliko yanayofanywa baada ya tarehe 20 ya mwezi wowote hayatatekelezwa hadi kipindi cha malipo cha mwezi unaofuata. Pia, ni lazima jumla ya salio lako la tarehe 20 lifikie kima cha malipo. Ikiwa salio lako halifikishi kima cha malipo au ikiwa una malipo yaliyoahirishwa, hutalipwa mwezi huo na salio lako litasogezwa mwezi unaofuata.
  • Tarehe 21 hadi 26: Hawala ya fedha ya kielektroniki huanzishwa. Kipengee cha "Malipo yanasubiri kushughulikiwa" huonekana kwenye ukurasa wako wa Malipo.

Subiri hadi siku 15 za kazi kabla ya uhamishaji kukamilika. Kipindi cha muda unaosubiri kabla ya malipo kuwasili kwenye akaunti yako ya benki kupitia hawala ya fedha ya kielektroniki kinaweza kutofautiana kulingana na benki unayotumia.

Kumbuka: Tarehe 21 ikiwa wikiendi au sikukuu, malipo yanaweza kutumwa siku ya kwanza ya kazi inayofuata tarehe 21 ya mwezi huo.

Kumbuka: Ikiwa akaunti ya mchapishaji itapatikana kuwa imekiuka Sheria na Mashari au Sera zetu za mpango, tunaweza kuzuilia malipo wakati wowote (kuanzia wakati Google imeanzisha uchunguzi wa ukiukaji husika), kukata mapato kwenye akaunti ya mchapishaji na/au kurejeshea watangazaji pesa kwa ajili ya mibofyo iliyopokelewa kwenye tovuti ya mchapishaji au AdSense kwenye ukurasa wa matokeo ya utafutaji.

Zaidi ya hayo, ikiwa mchapishaji amechelewa kufanya malipo yoyote kwa Google kuhusiana na mpango wa Google Ads, tunahifadhi haki ya kuzuilia malipo hadi atakapomaliza kulipa kiasi husika. Ili upate maelezo kamili ya masharti ya kulipa, rejelea Sheria na Masharti ya AdSense.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
17694458830119828631
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false