Machapisho yanaweza kukuza hadhira yako kwenye YouTube na kuboresha mawasiliano na hadhira yako. Pata maelezo zaidi kuhusu ustahiki na manufaa ya kichupo cha Jumuiya.
Kutunga chapisho
Ili utunge chapisho:
- Ingia kwenye YouTube.
- Katika sehemu ya juu ya ukurasa, chagua Tunga Tunga chapisho.
- Kwenye kisanduku cha juu:
- Andika ujumbe ili utunge chapisho la maandishi au uweke maandishi kwenye chapisho la picha, GIF au video.
- Chagua kutunga chapisho la video , kura , maswali au picha.
- Chagua Chapisha.
Tunadhibiti idadi ya machapisho ambayo chaneli inaweza kutunga katika kipindi cha saa 24 ili kulinda jumuiya ya YouTube. Ikiwa utaona ujumbe kuhusu hitilafu ya “umefikisha kikomo”, jaribu tena baada ya saa 24.
Kuratibu chapisho
Ili uratibu chapisho:
- Ingia kwenye YouTube.
- Katika sehemu ya juu ya ukurasa, chagua Tunga Tunga chapisho.
- Kwenye kisanduku cha juu:
- Andika ujumbe ili kutunga chapisho la maandishi au weka maandishi kwenye chapisho la picha, GIF au video.
- Chagua kutunga chapisho la video , kura , maswali au picha.
- Bofya kishale cha chini karibu na sehemu ya Chapisha kisha chagua Ratibu Chapisho.
- Chagua tarehe, wakati na saa za eneo za kuchapisha chapisho.
- Chagua Ratibu.
Kutaja chaneli zingine kwenye chapisho
Unaweza kutaja chaneli nyingine za YouTube kwenye machapisho yako kwa kuweka alama ya @ ikifuatiwa moja kwa moja na utambulisho au jina la chaneli husika. Chaneli inaweza kupokea arifa kuwa umeitaja. Watazamaji wanaweza kubofya mtajo huo kwenye kifaa chochote na kwenda moja kwa moja kwenye ukurasa wa chaneli hiyo.
Fahamu aina za machapisho
Machapisho ya maandishi
Ili kutunga chapisho la maandishi, andika ujumbe wako kwenye kisanduku cha maandishi kwenye kichupo cha Jumuiya cha chaneli yako. Unaweza kuchapisha maandishi yako peke yake au na video, picha au GIF. Machapisho ya maandishi hayawezi kuchanganywa na kura.
Machapisho ya orodha
Ikiwa umewasha kichupo cha Jumuiya, unaweza kuchapisha orodha kutoka kwa wasanii unaowapenda. Fungua orodha ambayo ungependa kutuma kisha unakili URL. Bandika URL ya orodha kwenye sehemu ya maandishi unapotunga chapisho lako.
Machapisho ya picha na GIF
Unaweza kuchagua kupakia idadi ya hadi picha 5 na chapisho lako. Bofya picha ili uchague picha au GIF zilizohuishwa kwenye kompyuta yako.
Iwapo unafikia kichupo cha Jumuiya, unaweza pia kuweka maandishi, vibandiko na vichujio kwenye chapisho lako la picha kupitia Programu ya YouTube.
Mwongozo
- Ukubwa: Hadi MB 16
- Aina za faili: JPG, PNG, GIF au WEBP
- Uwiano unaopendekezwa: Tunapendekeza uwiano wa 1:1 kwa sababu hivyo ndivyo picha huonyeshwa kwenye mipasho. Watazamaji wanaweza kuona picha yote kwa kubofya ili kuipanua.
Kumbuka kuwa picha lazima zifuate Mwongozo wa Jumuiya ya YouTube. Ikiwa picha zinakiuka Mwongozo wa Jumuiya, chapisho lako linaweza kuondolewa na chaneli inaweza kupewa onyo.
Machapisho ya video
Iwapo utachagua kuweka video kwenye chapisho lako, unaweza:
- Kutafuta video ya YouTube
- Bandika URL ya video ya YouTube
- Chagua video kwenye chaneli yako ya YouTube
Unapotunga chapisho ambalo linatuma video ya mtayarishi mwingine, arifa inaweza kutumwa kwa mpakiaji halisi wa video hiyo. Arifa hii husaidia watayarishi kuthibitisha wakati watayarishi wengine wanatuma video zao.
Kura
Ikiwa utachagua kuweka kura kwenye chapisho lako:
- Chagua angalau kura ya Maandishi au Picha.
- Kwa kura za Maandishi:
- Weka swali kwenye sehemu ya "Uliza jumuiya yako...".
- Weka majibu kwenye sehemu za "Weka chaguo" yasiyozidi herufi 65.
- Bofya Weka chaguo lingine ili uweke hadi majibu 4.
- Kwa kura za Picha:
- Weka swali kwenye sehemu ya "Uliza jumuiya yako...".
- Pakia picha kama majibu na uweke manukuu yasiyozidi herufi 36 katika sehemu ya “chaguo”.
- Bofya Weka chaguo ili uweke hadi picha 4.
Maswali
Ukichagua kuweka maswali kwenye chapisho lako:
- Weka swali kwenye sehemu ya maandishi.
- Weka majibu kwenye sehemu za "Jibu". Upeo wa majibu unaweza kuwa na hadi idadi ya herufi 80 kwa kila jibu.
- Ukihitaji sehemu zaidi za kuweka majibu, gusa Ongeza jibu. Unaweza kuwa na hadi majibu 4.
- Chagua jibu sahihi. Unaweza kuweka maelezo ambayo si ya lazima ya kwa nini jibu hili ni sahihi katika sehemu ya maandishi. Maelezo hayapaswi kuzidi herufi 350.
Kudhibiti shughuli zako
Unaweza kufikia na kudhibiti historia ya shughuli zako kwenye machapisho. Kipengele hiki kinapatikana tu kwenye kompyuta.
- Nenda kwenye YouTube.com.
- Kwenye upande wa kushoto, bofya Historia.
- Kwenye upande wa kulia, bofya Machapisho.
- Ili ubadilishe au ufute shughuli, wekelea kiashiria juu yake, bofya Zaidi Badilisha au Futa.