Kutunga Chapisho la jumuiya

YouTube Community Posts

Machapisho yanaweza kukuza hadhira yako kwenye YouTube na kuboresha mawasiliano na hadhira yako. Pata maelezo zaidi kuhusu ustahiki na manufaa ya kichupo cha Jumuiya.

Jinsi ya Kutayarisha Maudhui kwenye YouTube: Video, Video Fupi, Utiririshaji Mubashara kwenye Kifaa cha Mkononi na Machapisho kwenye simu yako

Kumbuka: Baadhi ya vipengele vya machapisho kama vile kuratibu, uhariri ulioboreshwa na kubainisha mwisho wa muda wa kuonekana bado havipatikani kwenye vishikwambi vya Android au iPad.

Kutunga chapisho

Ili utunge chapisho:

  1. Gusa Tunga kisha Chapisho.
  2. Weka maandishi.
  3. Chagua picha , kura au swali  kulingana na aina ya chapisho ambalo ungependa kutunga.
  4. Chagua Chapisha.
Kumbuka: Ukitaka kuweka mipangilio ya muda wa chapisho lako kuisha baada ya saa 24, gusa chupa inayopima saa chupa inayopima saa.

Tunadhibiti idadi ya machapisho ambayo chaneli inaweza kutunga katika kipindi cha saa 24 ili kulinda jumuiya ya YouTube. Ikiwa utaona ujumbe kuhusu hitilafu ya “umefikisha kikomo”, jaribu tena baada ya saa 24.

Kuratibu chapisho

Ili uratibu chapisho:

  1. Wakati unatunga chapisho lako, katika kona ya juu kulia, gusa saa.
  2. Chagua tarehe, wakati na saa za eneo za kuchapisha chapisho.
  3. Chagua Nimemaliza.
  4. Kwenye ukurasa wa kutunga chapisho, bofya Ratibu.

Kutuma video kwenye chapisho

Ili utume video kwenye chapisho:

  1. Nenda kwenye video ambayo ungependa kutuma.
  2. Gusa Tuma Share kisha Tuma.
  3. Gusa Tunga chapisho.
  4. Andika ujumbe wako kisha uguse Chapisha au .

Kutuma orodha kwenye chapisho

Ili utume orodha kwenye chapisho:

  1. Fungua orodha ambayo ungependa kutuma.
  2. Chagua Zaidi kisha Tuma.
  3. Gusa Nakili kiungo.
  4. Gusa Tunga kisha Chapisho.
  5. Bandika URL ya orodha ya video kisha uguse Chapisha.

Kutunga chapisho la mtiririko mubashara

  1. Kwenye skrini ya kwanza, gusa Tunga .
  2. Gusa Tiririsha Mubashara kisha Ya umma.
  3. Chagua kichwa, kisha uguse Endelea.
  4. Chagua kijipicha cha chapisho.
  5. Gusa Tuma Share kisha Tunga chapisho.
  6. Weka maandishi ya chapisho, kisha chagua Chapisha.
  7. Gusa Tiririsha Mubashara.
  8. Ili kukamilisha mtiririko, gusa Maliza.

Kutaja chaneli zingine kwenye chapisho

Unaweza kutaja chaneli nyingine za YouTube kwenye machapisho yako kwa kuweka alama ya @ ikifuatiwa moja kwa moja na utambulisho au jina la chaneli husika. Chaneli inaweza kupokea arifa kuwa umeitaja. Watazamaji wanaweza kubofya mtajo huo kwenye kifaa chochote na kwenda moja kwa moja kwenye ukurasa wa chaneli hiyo.

Fahamu kuhusu aina za machapisho

Machapisho ya maandishi

Ili kutunga chapisho la maandishi, andika ujumbe wako kwenye kisanduku cha maandishi kwenye kichupo cha Jumuiya cha chaneli yako. Unaweza kuchapisha maandishi yako peke yake au na video, picha au GIF. Machapisho ya maandishi hayawezi kuchanganywa na kura za maoni.

Machapisho ya orodha

Ikiwa umewasha kichupo cha Jumuiya, unaweza kuchapisha orodha kutoka kwa wasanii unaowapenda. Nakili na ubandike URL ya orodha kwenye chapisho lako.

Machapisho ya picha na GIF

Unaweza kuchagua kupakia idadi ya hadi picha 5 na chapisho lako. Gusa picha ili uchague picha au GIF zilizohuishwa.

Iwapo unafikia kichupo cha Jumuiya, unaweza pia kuweka maandishi, vibandiko na vichujio kwenye chapisho lako la picha kupitia Programu ya YouTube.

Mwongozo

  • Ukubwa: Hadi MB 16
  • Aina za faili: JPG, PNG, GIF au WEBP
  • Uwiano unaopendekezwa: Tunapendekeza uwiano wa 1:1 kwa sababu hivyo ndivyo picha huonyeshwa kwenye mipasho. Watazamaji wanaweza kuona picha yote kwa kubofya ili kuipanua.

Tumia tu picha ambazo una ruhusa ya kuzitumia. Unaweza pia kujumuisha maandishi kwenye chapisho lako la picha. Kumbuka kuwa picha lazima zifuate Mwongozo wa Jumuiya ya YouTube. Ikiwa picha zinakiuka Mwongozo wa Jumuiya, chapisho lako linaweza kuondolewa na chaneli inaweza kupewa onyo.

Machapisho ya video

Iwapo utachagua kuweka video kwenye chapisho lako, unaweza:

  • Kutafuta video ya YouTube
  • Bandika URL ya video ya YouTube
  • Chagua video kwenye chaneli yako ya YouTube

Unapotunga chapisho ambalo linatuma video ya mtayarishi mwingine, arifa inaweza kutumwa kwa mpakiaji halisi wa video hiyo. Arifa hii husaidia watayarishi kuthibitisha wakati watayarishi wengine wanatuma video zao.

Kumbuka: Machapisho kuhusu video ambayo tayari ipo kwenye Mipasho ya Ukurasa wa Kwanza au ya Chaneli Zinazofuatiliwa na mtazamaji huenda yasionekane tena. Mipangilio hii inazuia watazamaji wako kuona video moja mara kwa mara.

Kura

Ikiwa utachagua kuweka kura kwenye chapisho lako:

  1. Chagua kura ya MAANDISHI au PICHA.
  2. Kwa kura za maoni za MAANDISHI:
    1. Weka swali kwenye sehemu ya maandishi.
    2. Weka majibu kwenye sehemu za "Chaguo". Haya yanaweza kuwa na idadi ya hadi herufi 65 kila moja.
    3. Ikiwa unahitaji sehemu zaidi za kuweka majibu, gusa ONGEZA CHAGUO.
  3. Kwa kura za maoni za PICHA:
    1. Weka swali kwenye sehemu ya maandishi.
    2. Pakia picha kama majibu.
    3. Iwapo unahitaji picha zaidi, gusa ONGEZA CHAGUO ili uongeze idadi ya hadi picha 4.

Kumbuka: Upeo wa chaguo za kura za picha sasa umeongezeka hadi herufi 36. Chaguo za kura za matini zinaweza kuwa na upeo usiozidi herufi 65.

Maswali

Ukichagua kuweka maswali  kwenye chapisho lako:

  1. Weka swali kwenye sehemu ya maandishi.
  2. Weka majibu kwenye sehemu za "Jibu". Upeo wa majibu unaweza kuwa na hadi idadi ya herufi 80 kwa kila jibu.
  3. Ukihitaji sehemu zaidi za kuweka majibu, gusa Ongeza jibu. Unaweza kuwa na hadi majibu 4.
  4. Chagua jibu sahihi. Unaweza kuweka maelezo ambayo si ya lazima ya kwa nini jibu hili ni sahihi katika sehemu ya maandishi. Maelezo hayapaswi kuzidi herufi 350.
Kumbuka: Unaweza kuwa na jibu moja tu ambalo ni sahihi kwenye maswali.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
3776214864315772563
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false