Kuomba wataalamu wetu wakague video iliyoainishwa kuwa "Haifai watangazaji wengi"

Iwapo video yako haifai kwa watangazaji wengi, aikoni ya ishara ya dola ya manjano itawekwa karibu na video hiyo: . Makala haya yanaeleza jinsi video inavyobainishwa kuwa “imedhibitiwa” na jinsi ya kuomba ukaguzi mwingine.

Video hubainishwa kuwa "Haifai kwa watangazaji wengi" ikiwa:

Jinsi hali ya uchumaji wa mapato inavyotekelezwa

Katika mchakato wa kupakia, tunatumia teknolojia ya mashine kujifunza ili kutambua iwapo video inatii mwongozo wetu wa maudhui yanayofaa watangazaji. Pia tunakagua mitiririko mubashara iliyoratibiwa. Kabla ya kutiririshwa mubashara, mifumo yetu hukagua jina, maelezo, kijipicha na lebo.

Ikiwa huna uhakika kwa nini video yako ina aikoni ya manjano, soma mwongozo wetu wa maudhui yanayofaa watangazaji. Hakikisha unakagua jina, maelezo, kijipicha na lebo za video. Video zisizo na jina au metadata huenda zisiwe na muktadha wa kutosha kusaidia mifumo yetu kuelewa ikiwa maudhui yanafaa kwa watangazaji wote.

Wakati unaofaa kuomba ukaguzi

Kagua video kwa kulinganisha na vigezo vilivyoorodheshwa kwenye mwongozo wetu wa maudhui yanayofaa watangazaji. Ikiwa video yako inatimiza vigezo vyote vya “Maudhui haya yanaweza kuchuma mapato ya matangazo,” unapaswa kuomba ukaguzi. Pata maelezo zaidi kuhusu utaratibu wa ukaguzi wa kubaini ikiwa umetimiza masharti ya uchumaji wa mapato.

Kukata rufaa dhidi ya kizuizi cha ufaafu kwa matangazo

Tunafahamu kuwa mifumo yetu si sahihi kila wakati. Ukiona aikoni ya manjano na unafikiri kuwa mifumo yetu ilikosea, basi unaweza kuomba ukaguzi ufanywe na watu wanaokagua. Maoni yako hutumwa kwa mtaalamu na uamuzi wake husaidia kuboresha mifumo yetu kadiri muda unavyosonga.

Kumbuka: Kufuta au kupakia upya video si suluhisho

Ili ukate rufaa:

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, bofya Maudhui .
  3. Nenda kwenye video ambayo ungependa kukatia rufaa.
  4. Karibu na video, katika safu wima ya Vizuizi , wekelea kiashiria juu ya Ufaafu kwa matangazo.
  5. Bofya OMBA UKAGUZI. Fuata maagizo yaliyo kwenye skrini.

Kumbuka: Unaweza tu kupata chaguo la kukata rufaa ikiwa video yako imetimiza masharti. Baada ya kukata rufaa, maelezo kuhusu video yako yatasasishwa ili kuonyesha hali ya rufaa yako.

Omba ukaguzi wa ziada wa vikwazo vya ufaafu kwa matangazo

Huenda video yako ikastahiki kupata hatua moja zaidi ya uhakiki unaofanywa na binadamu. Ili kupata maelezo iwapo video yako inastahiki, tumia mwongozo huu wa kujisaidia mwenyewe.

Angalia ustahiki wa ukaguzi wa ziada

Utaratibu wa mchakato wa kukata rufaa

Unapotuma ombi ili ukaguzi ufanywe na binadamu, mtaalamu huangalia video. Anatumia muda wake kutazama na kukagua maudhui, jina na metadata ya video akilinganisha na mwongozo wetu wa maudhui yanayofaa watangazaji. Pata maelezo zaidi kuhusu utaratibu wa ukaguzi wa kubaini ikiwa umetimiza masharti ya uchumaji wa mapato.

Uamuzi wa mwisho unapofanywa kuhusu video yako, utaarifiwa kupitia barua pepe.

Kumbuka: Usisahau kwamba hali ya aikoni ya video inaweza kubadilika baada ya wewe kuwasilisha video yako ili ifanyiwe ukaguzi. Mifumo yetu huendelea kufanya uchanganuzi wake hadi ukaguzi ukamilike.

Muda ambao unatumika kufanya ukaguzi

Tunafahamu kuwa ukaguzi huu ni muhimu kwako na unaathiri mapato yako. Ukaguzi unaofanywa na watu unaweza kuchukua hadi siku 7. Baada ya ukaguzi kukamilika, utapokea barua pepe iliyo na uamuzi kuhusu uchumaji wa mapato. Baada ya ukaguzi mmoja wa ziada, uamuzi wa mkaguzi ni wa mwisho na hali ya uchumaji wa mapato kutokana na video haitabadilika.

Kusaidia kuepuka vizuizi vya ufaafu kwa matangazo siku zijazo

Ikiwa ungependa kuepuka vizuizi siku zijazo, katika mchakato wa kupakia, unaweza kutumia zana ya uthibitishaji unaojifanyia. Pata maelezo zaidi kuhusu ukurasa wa “Ukaguzi” katika muhtasari wa Uthibitishaji Unaojifanyia kwenye YouTube.
Kumbuka: Matokeo ya ukaguzi wa hakimiliki na Ufaafu kwa matangazo si ya mwisho. Kwa mfano, madai ya baadaye ya Content ID unayofanya mwenyewe, maonyo ya hakimiliki na mabadiliko kwenye mipangilio ya video yako yanaweza kuathiri video yako. Metadata ya video yako ikibadilika baada ya video kuchapishwa na hivyo kufanya isifae kwa matangazo, huenda orodha yako ya video ikawa na vizuizi vipya vya uchumaji wa mapato.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
2604124711316438391
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false