Ukipoteza muunganisho wako wa intaneti wakati unatumia programu ya YouTube kwenye iPhone au iPad, utapokea ujumbe kuhusu hitilafu katika kicheza video. Huenda pia ukapata ujumbe kuhusu hitilafu katika vichupo vya Ukurasa wa Kwanza, Zinazovuma, Vituo Unavyofuatilia au Wasifu.
Ili uendelee kutumia programu
- Hakikisha kuwa umeunganisha kifaa chako kwenye intaneti.
- Iwapo hujaunganisha kifaa chako kwenye Wi-Fi:
- Nenda kwenye programu ya Mipangilio katika kifaa chako.
- Hakikisha kuwa Data ya Mtandao wa Simu imewashwa kwa ajili ya YouTube.
- Anzisha upya muunganisho wa mtandao wako kwa kuuzima na kuuwasha tena.
- Katika programu ya YouTube, telezesha kidole chini ili skrini ipakie upya.
- Funga kisha ufungue programu ikihitajika.
Kutazama nje ya mtandao ukitumia YouTube Premium
Iwapo umeingia katika akaunti ya YouTube Premium kwenye kifaa cha mkononi, unaweza kutazama video ambazo ulipakua awali. Utapata video hizi katika kichupo cha Wasifu. Baadhi ya vitendo, kama vile kutoa maoni na kuweka alama za imenipendeza, vinapatikana tu wakati kifaa chako kimeunganishwa mtandaoni.
Kupakua video za kutazama nje ya mtandao katika nchi mahususi
Katika maeneo mahususi, video fulani kwenye programu ya YouTube ya vifaa vya mkononi zinaweza kupakuliwa kwa ajili ya uchezaji nje ya mtandao. Video hizi zinaweza kutazamwa wakati kuna muunganisho hafifu au wakati hamna muunganisho wa intaneti. Utapata video hizi katika kichupo cha Wasifu.
Lazima uwe umeingia katika akaunti ili utumie kipengele cha Pakua. Baadhi ya vipengele, kama vile kutoa maoni na kupenda, vinapatikana tu wakati kifaa chako kimeunganishwa mtandaoni.
Video zilizopakuliwa zinaweza kuchezwa nje ya mtandao kwa hadi saa 48. Baadaye, utahitaji kuunganisha upya kifaa chako kwenye mtandao wa simu au Wi-Fi kila baada ya saa 48 ili kuruhusu programu ikague mabadiliko kwenye video au upatikanaji wake.
Maeneo ambako upakuaji unapatikana
Aljeria
Angola
Antatika
Armenia
Azabajani
Benini
Butani
Botswana
Kisiwa cha Bouvet
Himaya ya Uingereza katika Bahari Hindi
Brunei Darussalam
Bukinafaso
Burundi
Kameruni
Kepuvede
Jamhuri ya Afrika ya Kati
Chadi
Komoro
Kongo (Brazzaville)
Kongo (Kinshasa)
Visiwa vya Cook
Kodivaa
Ginekweta
Eritrea
Ethiopia
Fiji
Guyana ya Ufaransa
Polinesia ya Ufaransa
Gambia
Jojia
Ghana
Grenada
Gine
Ginebisau
Indonesia
Irani
Iraki
Kiribati
Kirigizistani
Lebanoni
Lesoto
Liberia
Libya
Madagaska
Malawi
Malesia
Maldova
Mali
Visiwa vya Marshall
Moritania
Morisi
Mayote
Moldova
Mongolia
Moroko
Msumbiji
Myanmar
Nauru
Nepali
New Caledonia
Naija
Naijeria
Visiwa vya Mariana Kaskazini
Palau
Palestina
Papua
Ufilipino
Rwanda
Saint Pierre na Miquelon
Samoa
Sao Tome na Prinsipe
Senegali
Ushelisheli
Sieraleoni
Visiwa vya Solomoni
Somalia
Afrika Kusini
Sudani Kusini
Srilanka
Sudani
Visiwa vya Svalbard na Jan Mayen
Eswatini
Tanzania
Tailandi
Togo
Tonga
Tunisia
Turkmenistani
Tuvalu
Uzibekistani
Vietnamu
Zimbabwe