Manukuu ya kiotomatiki kwenye video za maudhui marefu na Video Fupi
Tunawahimiza watayarishi waweke manukuu ya kitaalamu kwanza. Ikiwa manukuu ya kiotomatiki yanapatikana, yatachapishwa kwenye video kiotomatiki. Huenda manukuu ya kiotomatiki yasiwe tayari wakati unapakia video. Muda wa uchakataji unategemea kiwango cha uchangamano wa sauti ya video.
YouTube inaboresha teknolojia yake ya utambuzi wa matamshi mara kwa mara. Lakini, huenda manukuu ya kiotomatiki yakawakilisha visivyo maudhui yaliyozungumzwa kutokana na matamshi yasiyofaa, lafudhi, lahaja au kelele za mazingira. Kagua manukuu ya kiotomatiki kila wakati na uhariri sehemu zozote ambazo hazijanukuliwa vizuri.
Hivi ndivyo unavyoweza kukagua manukuu ya kiotomatiki na kufanya mabadiliko, panapohitajika:
- Ingia katika akaunti kwenye Studio ya YouTube.
- Kwenye menyu ya kushoto, chagua Manukuu.
- Bofya video unayotaka kuweka manukuu.
- Kwenye sehemu ya “Manukuu”, bofya Zaidi karibu na manukuu unayotaka kuhariri.
- Kagua manukuu ya kiotomatiki na uhariri au uondoe sehemu zozote ambazo hazijanukuliwa vizuri.
Kutatua matatizo ya manukuu ya kiotomatiki
Ikiwa video yako haizalishi manukuu ya kiotomatiki, huenda ikawa kutokana na sababu moja au zaidi kati ya zifuatazo:
- Manukuu bado hayapatikani kwa sababu ya uchakataji wa sauti changamano kwenye video.
- Manukuu ya kiotomatiki hayapatikani kwa lugha iliyo kwenye video.
- Video ni ndefu mno.
- Video ina ubora wa chini wa sauti au YouTube haitambui matamshi husika.
- Kuna kipindi kirefu cha kimya mwanzoni mwa video.
- Kuna wazungumzaji wengi ambao matamshi yao yanafanyika kwa wakati mmoja au lugha nyingi kwa wakati mmoja.
Kwa sasa manukuu ya kiotomatiki ya mitiririko mubashara yanasambazwa kwenye vituo vya Kiingereza. Vituo hivi vinatiririsha katika "muda wa kawaida wa kusubiri" na manukuu ya kitaalamu hayapatikani. Tunawahimiza watayarishi watumie manukuu ya kitaalamu kwanza. Pata maelezo kuhusu masharti ya manukuu papo hapo.
Mtiririko mubashara ukiisha, manukuu ya kiotomatiki ya papo hapo hayatasalia kwenye video. Manukuu mapya ya kiotomatiki yatazalishwa kulingana na mchakato wa Mfumo wa Kufikia Video Unapohitaji (VOD) na huenda yakawa tofauti na yale yaliyoonekana wakati wa mtiririko mubashara.
Kuweka manukuu ya kiotomatiki ya papo hapo
Hivi ndivyo unavyoweza kuwasha kipengele cha manukuu ya kiotomatiki (Kiingereza peke):
- Nenda kwenye YouTube.
- Upande wa juu kulia, bofya Anzisha Tiririsha mubashara.
- Chagua Tiririsha kwenye menyu ya kushoto.
- Kwenye mipangilio ya mtiririko, washa Manukuu.
- Chagua “Manukuu ya kiotomatiki” kama chanzo cha manukuu.
- Chagua lugha ya video yako (Kiingera pekee)
Kutatua matatizo ya manukuu ya kiotomatiki ya papo hapo
Ikiwa mtiririko mubashara hauzalishi manukuu ya kiotomatiki, huenda ikawa ni kutokana na sababu moja au zaidi kati ya zifuatazo:
- Kipengele hicho hakijawashwa kwenye kituo kwa vile kunasambazwa polepole kwenye vituo vinavyofuatiliwa na zaidi ya watu 1,000.
- Kituo kinatiririsha katika muda mfupi au muda mfupi zaidi wa kusubiri (kama vile mtiririko mubashara kwenye kifaa cha mkononi). Manukuu ya kiotomatiki ya papo hapo yanapatikana tu kwenye utiririshaji wa muda wa kawaida wa kusubiri.
- Manukuu ya kiotomatiki hayapatikani kwa lugha iliyo kwenye video.
- Video ina ubora wa chini wa sauti au YouTube haitambui matamshi husika.
- Kuna wazungumzaji wengi ambao matamshi yao yanafanyika kwa wakati mmoja au lugha nyingi kwa wakati mmoja.
Mipangilio ya kina ya manukuu ya kiotomatiki
Maneno ambayo huenda hayafai kwenye manukuu ya kiotomatikiKwa chaguomsingi, mipangilio ya “Usionyeshe maneno ambayo huenda hayafai” kwenye Studio ya YouTube huondoa maneno ambayo huenda hayafai na kuweka bano la kufungua, mistari chini miwili na bano la kufunga “[ __ ]” kwenye manukuu ya kiotomatiki. Mipangilio hiyo haiathiri nyimbo zozote za sauti au manukuu uliyohariri mwenyewe. Inakusudiwa kusaidia kuzuia maneno ambayo huenda hayafai yasionekane kimakosa kwenye manukuu ya kiotomatiki. Pia haiathiri hali ya uchumaji wa mapato ya video yako.
Manukuu ya kiotomatiki hutumika kwenye video zilizopakiwa na mitiririko mubashara.
Bado tunahimiza watayarishi wakague manukuu yao yote yaliyozalishwa kiotomatiki huku tukiendelea kuboresha programu yetu ya utambuzi wa matamshi na kupunguza makosa kwenye manukuu ya kiotomatiki.
Hivi ndivyo unavyoweza kuzima mipangilio ya “Usionyeshe maneno ambayo huenda hayafai”, panapohitajika:
- Ingia katika akaunti kwenye Studio ya YouTube.
- Kwenye menyu ya kushoto, chagua Mipangilio .
- Chagua Kituo Mipangilio ya kina.
- Kwenye sehemu ya "Manukuu yanayozalishwa kiotomatiki," acha kuchagua Usionyeshe maneno ambayo huenda hayafai.